Tujenge utamaduni wa kuwapa thamani wachezaji wazawa

Labda utoe mfano mwingine siyo Feitoto huyu hana body language nzuri,(how do you support him),
Halafu unakuta mbongo kama wewe eti unachukizwa na drama za Feitoto lakini hauchukizwi hata kidogo na zile dramas za morison na si ajabu hata ulikuwa unamtetea kisa tu huyobMorison anatoka huko West Africa wakati Fei ni mbongo mwenzio.... najua sana akili zenu wabongo
 
Ni kuendelea kuelimishana, kidogo kidogo watu watabadilika.

Unajua kasumba na mazoea ni kitu kibaya sana. Mtu kwa kuwa amezoea na ameishi akiona jambo fulani linafanyika hivi au jamii ina mtazamo fulani kuhusu jambo fulani, basi yeye akili yake itafungwa akiamini hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa hata kama jambo hilo lina kasoro. Inachukua muda mrefu na mpaka labda muhusika apate exposure fulani kidogo ndiyo akili yake inafunguka.

Huwa sichoki kuleta mada kama hizi mara kwa mara kwa vitu ambavyo nimeona vimeota mizizi katika jamii pamoja na kwamba vina kasoro, ukimgusa mtu mmoja ukabadilisha mtazamo wake inatosha.
 
Wachezaji wazawa hawajipi thamani wenyewe,mfano ukilinganisha uwezo wa maamuzi na usahihi wa matendo kiwanjani unaona kabisa wageni wametuacha mbali hivyo thamani yetu lazima iwe ya kawaida,wazaawa wanaripuka msimu mmoja kisha wanapotea mazima mfano George mpole,Mbaraka yusuph,Malimi busungu,Abrahman Mussa,Eliud Ambokile na wengine wengi. japokuwa sikatai swala la media na wadanganyika kuwashobokea wageni.

Tumekuwa tunasikia majina ya kina Sande Manara,Mohamed mwameja,Nteze John,Peter Manyika,Peter Tino,Lunyamila n.k hawa ni wazawa ambao walitamba na kutawala soka na kupewa thamani.....wahezaji wazawa wajitathmini wanafeli wapi.......kingine hizi timu mbili kubwa ndio wanaoshusha thamani za wahezaji mhezaji akitakiwa na timu hizi haangalii thamani yake.
 
Soma uzi unasemaje hata hivyo mimi siyo mashabiki kwa wanaojiitoa ufahamu , (am not in favor of unbecoming behavior). I call a spade a spade not a big spoon
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…