Msifanye watu wawe na taharuki zisizo na msingi hapo tu Ukraine vs urusi vp ikija ya china , USA,ujeruman,na mataifa makubwa yote, ndio maana tuna ambiwa kila siku kutegemea cha ndugu lazima utakufa maskini, hiyi nchi sio ya kuhaha kama mnavyotuaminisha , ni uongo na kupika data za hovyo , na sijui mnafanya kwa nia ipi
Uchumi unajengwa na mambo makuu mawili tu uuzaji na ununuaji iwe bidhaa au huduma( Demand and Supply). Mnyororo huu ukiyumba wa uuzaji na ununuaji tegemea maafa makubwa sana kwenye uchumi wa nchi
Hali mbaya ya maisha ilishaonekana hata kabla ya vita na niliandika uzi huu
Members, Hili ni swali ambalo linaangazia uchumi halisi wa watu binafsi kwenye mitaa yaani uwezo wa Mtu mmoja mmoja kumudu maisha yake ya kila siku (Micro enonomics) kutoka oktoba mwaka 2020 mpaka oktoba mwaka huu 2021 Uchumi wa Mtu binafsi tutaupima kwa vigezo vifuatavyo ndani ya mwaka mmoja...
www.jamiiforums.com
Madhara ya uchumi huwa yanachukua muda mrefu sana kuonekana kuanzia miezi sita na kuendelea, Ongezeko la bei za mafuta na bidhaa kwa sasa hii ni rasha rasha tu, Vita ikiendelea ya Russia na Ukraine kila kitu kitaongezeka bei kwa asilimia mia moja (100%)
Nchi za ulaya na Marekani ndio watoa misaada mikubwa Africa, Hizi nchi za ulaya na Marekani ndio wanaotusaidia pesa za kigeni kwa utalii na kutupatia mikopo na misaada mbalimbali kama wakati wa korona, Hizi nchi kwa sasa wanapambana na hali zao za maisha kudhibiti mfumuko wa bei
Tanzania tutapata wapi pesa za kigeni ili kuweza kudhibiti thamani yetu ya shilingi?
Ni watalii gani wana raha ya kuja Afrika wakati gharama zao za kumudu maisha ulaya zinazidi kuongezeka?
Mafuta ya ndege bei zimepanda, Nauli zitaendelea kupanda Katika sekta ya usafirishaji na hii itazifanya bidhaa zetu tutakazo uza nje kuonekana ni ghali sana
Malengo ya Putin bado hayajulikani na mwisho wa vita hii hakuna anayejua lengo lake kiuchumi, zimebaki Propaganda tu lakini uhalisia na mwisho wa hii vita ni siri kubwa
Athari za uuzaji na ununuaji bidhaa tayari Tanzania umeshaanza kuonekana kwa kasi ya ajabu sana
Serikali ijitahidi kutoa ruzuku kwa Makampuni ya uagizaji wa mafuta ili kufidia gharama zao za usafirishaji
Serikali isipoingilia kati tutegemee maisha màgumu zaidi miezi mitatu ijayo,
Midomoni wanaendelea kusema wanafungua nchi lakini kimsingi hapa ndani hali ya mwananchi wa kawaida inazidi kuwa mbaya.
Nashindwa kuelewa kama kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kasi ya kufungua nchi na hali ya maisha kuzidi kuwa mbaya, kama uhusiano huo upo basi bora nchi ifungwe tu.
Bidhaa mbalimbali zinazidi kupanda bei sokoni, huku namsikiliza Waziri Mkuu anawaambia wafanyabiashara wasipandishe bei kwasababu ya mfungo, anasahau bosi wake alishatuambia tukae sawa vita ya Ukraine na Urusi haita tuacha salama.
Naona kwa sasa nchi yetu iko kama inaongozwa na serikali mbili tofauti, serikali moja inajaribu kuzuia tatizo, nyingine inakuza tatizo, mpaka pale watanzania tutakapoamka na kusema sasa basi... wacha tuendelee kuteseka.
Binafsi nashukuru Mungu kuwa tatizo hili limetokea kipindi bwana yule alishatwaliwa na Muumba, maana tatizo lingekuwa kubwa zaidi na hakuna mtu yeyote angefungua mdomo wake.
Hii sio serikali ya kuchukua hatua kwa chochote, hii ni serikali ya kutafta wa kumtupia lawama.
Rais ambae anaitwa mfariji mkuu wa nchi anasimama na kusema vitu vyote vitapanda bei na hii ni hali ya Dunia. Kwa maana nyingine anasema msiniulize wala kulalamika kwa chochote sio mimi ninaehusika.
Nchi nyingine hata zilizoendelea wanatoa ruzuku kupunguzia wanachi maumivu yeye anasema ruzuku haisaidii kitu chochote hivyo wananchi tukubali kukabiliana na hali yoyote inayokuja.
Sasa hivi kila kitu huyo mama anawalaumu warusi na Ukraine ndio wamesababisha, iwe mafuta ya magari, mafuta ya mboga, simenti, mabati, vioo vya madirisha, nondo, ushuru wa magari na bidhaa nyingine zote yeye anataka tuwalaumu Ukraine na vita yao.
Ccm walishafeli kitambo sana, sema wanalazimisha tu kutawala, imagine waliruhusu mtu kama Jiwe kushika madaraka makubwa vile. Sema Mungu anatulinda na kutupenda sana.
Ccm walishafeli kitambo sana, sema wanalazimisha tu kutawala, imagine waliruhusu mtu kama Jiwe kushika madaraka makubwa vile. Sema Mungu anatulinda na kutupenda sana.
Umetoa jibu jepesi kwenye jambo kubwa.Inaonekana wewe nikati ya watu ambao hawana uwezo wakutafuta altenative kwasababu tu jirani nayeye anatatizo kama lako.Huu sio wakati wakujilinganisha na mtu kwasababu kila nchi ina uchumi wake na mazingira yake.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.