Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
1. Watuhumiwa watatu kwenye hii walikamatwa mwaka 2020 na kuhojiwa Kisha kufunguliwa mashtaka yasiyo ya Ugaidi.
2. Watuhumiwa watatu baada ya kutoa maelezo Yao mwaka 2020 walipokamatwa awakuwahi kurejea uraiani walipelekwa mahakamani Kisha mahabusu,hivyo awajawahi kupata dhamana Wala kuhojiwa Tena.
3. Hadi watuhumiwa wanakamatwa Polisi walijua kwamba zipo Tuhuma za Ugaidi Kwa sababu Kwa mujibu wa Shahidi wa Jamhuri Denis Urio alishafikisha taarifa Polisi. Hivyo Polisi walikwenda kuwakamata watuhumiwa wa makosa ya Ugaidi Kwa mujibu wa Informer wao Be. Denis Urio
4. Polisi haohao ambao tayari walikuwa na taarifa zote awakumkamata mfadhili wa Ugaidi na kumweka mahabusu pamoja na watuhumiwa wengine,walimwacha.
5. Huku wakijua wazi wahusika wa uhalifu na uhalifu uliofanyika na madhara yake Kwa nchi hakuna hatua zozote zilizofanyika za kumamata mfadhili wa Ugaidi lakini pia Bado watuhumiwa waliendelea kukosa dhamana
6. Kwa kipindi Cha mwaka mzima hakuna popote kwenye maelezo ya mashahidi akiwemo mpelelezi wa shauri anaeleza kwamba alifanya upelelezi wa ziada uliopelekea watuhumiwa kuendelea kushikiliwa. Fact zilezile zilizoandikwa kwenye maelezo 2020 zilibaki zile zile ikiwemo, hakuna aliyekwenda hoteleni Aishi, hakuna aliyekwenda hoteli palipofanyika kikao Cha kwanza, hakuna aliyekwenda kufanya upekuzi Kwa mfadhili wa Ugaidi kuzuia asiwe na vilipuzi, hakuna aliyefanya chochote tofauti na kuandika maelezo ya watuhumiwa. Means upelelezi ulikamilika na kufungwa siku tu watuhumiwa watatu walipokamatwa na kuhojiwa.
7. Mfadhili aliendelea kufanya kampeni, akasafiri nje, akarudi akaendelea kufanya siasa na kukutana na makundi makubwa ya watu lakini hakuna aliyechukua taadhari mfadhili wa Ugaidi asitekeleze azma yake.
8. Kiongozi anayedaiwa kupata ya ugaidi ni mhalifu ambaye serikali hiyohiyo iliyosema alitegemewa kudhuriwa ndiyo hiyo imempeleka mahakamani kwamba alifanya uhalifu na kuendelea na uhalifu kabla Mbowe ajaajiri walinzi na baada ya kuajiri walinzi. Kwa maana nyingine Polisi waliaminishwa muhalifu anatarajia kufanyiwa uhalifu kipindi ambacho yeye Mwenyewe alikuwa anafanya uhalifu.
9. Kiongoz aliyepangwa kupata madhara akiwa DC ajawahi kuandikwa maelezo ya aina yoyote hata kuhusiana na uhusiano wake na shahidi aliyedai alikuwa anafanya kazi kwake. Hakuna ushahidi wowote unaoonyesha shahidi Kaaya alikuwa na mahusiano ya kikazi na DC Sabaya. Katika USO wa mahakama nivigumu kusema amewahi kuwa rafiki au hata mfanyakazi wa kiongoz mfungwa Sabaya
10. Hakuna chochote kilichokamatwa kinachothibitisha uwepo wa uhalifu. Si kwa mawasiliano Wala kwenye maelezo ya mashahidi.