Tujifunze jinsi ya kuandaa Unga wa lishe hadi jinsi ya kuupika uji huu

Thanks The secretary. Ukishachemsha kwa dakika kumi na kutoa maganda, unaroweka tena for 24-48 hours. kwanini? je nikiroweka moja kwa moja bila kuchemsha kwa dakika 10?
Please nikisie muda mrefu. Dakika/Masaa karibia mangapi?

ili kuondoa sumu iliyopo kwenye maganda
 
Last edited by a moderator:
Naomben mnifundishe jinsi ya kuweka ufuta kwenye uji Wa lishe. Vipi, unakaangwa kwanza?
 
Naomben mnifundishe jinsi ya kuweka ufuta kwenye uji Wa lishe. Vipi, unakaangwa kwanza?

Hodi kwenye jukwaa hili. Mimi ufuta huwa nausafisha, kisha nauanika ukishakauka naukaanga kwa moto mdogo na kwa muda mfupi kisha nachanganya na nafaka zingine tayari kwa kusaga.

Ila karanga hazishauriwi sana kwa lishe ya mtoto maana hutengeneza fangasi mapema zikiwa zimechanganywa. Mimi huandaa karanga pembeni na kuweka kwenye uji wakati wa kuupika. ( KAMA TUNAVYOUNGA MBOGA)
 
"Hatari ya unga wa lishe ya watoto

Mchanganyiko usiozingatia makundi matano ya vyakula, unaotengenezwa na wajasiriamali au nyumbani kwa ajili ya unga wa watoto maarufu ‘Lishe’, una athari za kiafya kwa watoto wachanga na walio chini ya miaka mitano.

Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Augustine Massawe, amesema unga huo ni hatari kwa sababu mchanganyiko wake si muafaka kwa watoto.

Dk Massawe alikuwa akitoa mada kwenye semina ya waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama.

Alisema kwanza utengenezaji wa unga huo hauzingatii vipimo maalumu, wala makundi ya virutubisho anavyopaswa kupata mtoto katika mlo mmoja, ambavyo ni wanga, protini, vitamini, mafuta na madini.

Massawe alikosoa utengenezwaji wa unga unaochanganywa mahindi, mchele, ulezi, soya, mtama,
karanga na dagaa.
“Mchanganyo kama huu haukubaliki kwa sababu katika mchanganyiko wa aina hii, kuna orodha ya nafaka ambazo zina kirutubisho kimoja cha wanga na haziongezi virutubisho vingine.

“Mbaya zaidi katika mchanganyo kama huu, kila aina ya nafaka inayowekwa, ina muda wake wa kuiva na hautakuwa na ladha kwa mtoto zaidi ya kuleta ugumu katika mmeng’enyo wa chakula tumboni kwa mtoto,”
alisema Dk Masawe.

Wataalamu wanashauri muandaaji wa chakula cha mtoto, kupika unga wa aina moja ya nafaka, ukishaiva ndio aweke unga wa karanga ambazo zimesafishwa, ili kuondolewa fangasi zinazoleta sumu ya toxin inayoambukiza saratani ya ini.

Kwa mujibu wa ushauri huo, endapo karanga zitawekwa kwenye mchanganyo wa nafaka kama ilivyo kwa baadhi ya unga wa lishe, zina tabia ya kupungua katika kila hatua.

Karanga zimetajwa kupungua wakati wa kusaga mchanganyiko huo, ambapo hunata katika mashine, pia wakati wa kuchekecha unga, karanga hubaki katika kichekecho na wakati wa kupika, kutokana na kuwa na hulka ya kuungua kabla uji haujaiva, hubakia katika sufuria na hivyo kumkosesha mtoto protini na mafuta.

Baadhi ya athari ya mchanganyiko huo, ni watoto kufunga choo kutokana na chakula kushindwa kumeng’enywa, kuhara na kukosa vitamini.

Athari nyingine mbaya ni mtoto kuwa hatarini kupata saratani ya ini, kama karanga zilizochanganywa katika lishe, hazikuoshwa vizuri.

Massawe alipendekeza wazazi watumie aina moja ya nafaka kama mahindi ambayo yanatoa wanga, mafuta na nyuzi.

Aidha Mtaalamu kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Neema Joshua alisema taasisi yake imekuwa ikifanya juhudi za kutoa elimu kwa jamii kuachana na aina hii ya michanganyo.

Alisema changamoto wanayokutana nayo katika kupambana na hali hiyo, inatokana na wajasiriamali kukwepa sheria kwa kutambulisha kuwa mchanganyiko huo ni muafaka kwa watoto, wagonjwa na wazee.

Neema alisema kumekuwapo na ongezeko la utapiamlo kwa watoto, unaosababishwa na vyakula vya aina moja na visivyokuwa na virutubisho kama wanga, protini, vitamini na mafuta.

Naye Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza, alisema Taasisi yake imekuwa ikifanya juhudi za kutoa elimu kwa wajasiriamali, ili watengeneze unga unaojumuisha makundi hayo matano ya vyakula.

“Tumekuwa tukitoa elimu kwa wajasiriamali na baada ya hapo, tunasajili bidhaa zao kwa wale wanaozingatia muongozo wa TFDA na Taasisi ya Chakula na Lishe,” alisema.

Haya sio maneno yang, nimeyapata mahali nikaona niyadondoshe humu tujadiliane.
 
Angry Bird,
Madaktari nao wabatuchanganya mnooo tunashindwa hata kujua lipi tuchukue lipi tuache

Nasikia mtoto anatakiwa kula yai moja kwa siku ila pia yasizidi matatu kwa wiki.
Kuna Dr alinambia haina shida hata mawili akitaka mtoto nimpe tu, pia kwakua hapendi msosi anapenda uji tu, basi nitengeneze lishe inamtosha sasa sijui nifate lipi
 
kwa nini ulezi kilo moja na siyo 2?
Kwa nini soya isiyobanguliwa? what about protein inhibitor kwenye ganda la soya? Kwa nini aranga mbichi etc?

Toa maelezo ya kutosha ya vipimo ulivyoainisha. What you've written hata bibi yangu kule namanyere anafanya hivyo.
 
gfsonwin,
Hapa Hakuna haja ya kuweka Mchele?

Na hii lishe inaweza kutumiwa na mtu mzima? Au kwa Ajili ya watoto?
 
Karucee,
Sio lazima kuchemsha, cha muhimu Isha vizuri soy zako kwa maji masafi ukiwa umesha zichambua nakuitia zilizooza na uchsfu kisha loweka kwenye maji ya kawaida tu yani room temperature kwa muda usiopungua masaa mawili mpaka Sita ukipenda mimi huloweka Lisaa kimoja mpaka matatu,

kisha anzakuzifikinya soy zako, yani maganda yote yanatoka, utamwaga maji taratibu kutoa makali, kisha weka maji tena fikicha soy zako huku ukimwaga makapi/maganda mpaka uridhike kisha chuja maji na uanike mpaka soy zikauke kabisaaa haina haja ya kuchemsha na kukaanga tena baada ya hapo. Hizo zingine ni mbwembwe tu.
 
Write your reply...Mwanangu hataki uji anataka papati (chapati) na nziwa(maziwa) akiumwa ndo anasema uji nampikia anakunywa, akipona hataki.
 
Mkuu kama ni kupika tu we chukua maharage, kunde, njegere, mbaazi, mchicha pori, kisamvu, dagaa, kambare, perege, nguruwe, kiti moto, mkuu wa meza, bia tatu, halafu changanya vyote katupe.

Yaan kwa hoja yako ni kua tiari una unga wa lishe alafu kupika ndio huwezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbaazi zinaandaliwaje hapo mkuu
 
dagaa wapi huwa wanafaa au dagaa wowote
 
Enheeeee!
Utu uzima dawa!
 
Nimeandaa unga wa lishe nimechanganya mahindi ya njano, choroko, karanga, soya, dengu, ufuta, mtama, ngano, mbegu za maboga na ulezi
 
Jee hii ration anaweza tumia ata mama aliejifungua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…