Tujifunze jinsi ya kuandaa Unga wa lishe hadi jinsi ya kuupika uji huu

Tujifunze jinsi ya kuandaa Unga wa lishe hadi jinsi ya kuupika uji huu

gfsonwin ukiweka kg 1 moja ya ulezi kwa ratio ya vitu ulivyovitaja hapo itakuwa inazidi cha muhimu ulezi uwe kg 2 na vinavyofata viwe katika ratio ya robo kg.

mfano: ulezi kg 2,uwele,ufuta,soya.karanga,na ngano isiyokobolewa mi huwa sipendelei kuwaeka mahindi ikiwa nafaka za aina nyingine nikiwa nimezitumia kwa sababu mahindi hufanya uji kuwa mzito pindi utakapo wekwa kwenye chupa na vilevile huwa na chenga kubwa kwa mtoto anayeanza lishe.

Pia karanga huwa natumia zilizokaangwa na kumenywa ili kufanya unga uwe mlaini na huwa ni vizuri kwa kuwa soya imetumika pia ikiwa na kiwango kikubwa cha protini. Soya inatakiwa ukisha chemsha loweka kwa masaa 24 hadi 48 kabla ya kuanika ikiwa pamoja na kuondolewa maganda.

Ulezi kwa umakini zaidi unaweza kuubuluza kwenye kinu kwa kiwango kidogo kwa sababu kuna ulezi mwingine unakuta hauja pwaguliwa vizuri unakuwa umeshikana na mapumba.kwa wanaopenda kuweka na dagaa wale ambao hawawa kauzu ni vizuri zaidi na huwa una harufu nzuri.

cc: Karucee na Erickb52
Huu mchanganyiko anaweza tumia hata mama alie jifungua?
 
mimi nimeandaa mwezi uliopita
karanga robo kilo
ulezi dumla 1 (kilo 3 kama na robo hivi)
mchele kilo 1
mahindi yasiyokobolewa kilo 1
ngano kilo 1
dagaa nusu kikombe
soya zilizochemshwa zikaanikwa na kubanduliwa maganda nusu dumla
mbegu za maboga nilizikaanga kikombe kidogo kimoja
viazi nilivimenya nikakata slices ndogondogo nikakausha kwenye jua then mechanganya
 
Back
Top Bottom