kyagata
JF-Expert Member
- Oct 18, 2016
- 10,406
- 19,892
Leo nimeamka nikiwa sina hata mia mbovu mfukoni,kila mshikaji niliyekua namuomba aniazime hata elfu 10 tu wote wakawa wananikataa.nikapekua simu yangu nikakuta jina la ex wangu ofcoz huyu dada tuliachana tu coz ya harakati za maisha na huwa tunachat mara moja moja tu kupeana salamu na vitu kama hivyo.nikajisemea ngoja nimtest huyu aniazime kama laki 2 hivi,aise dada wa watu hata hakua na maswali mengi alichoniuliza tu ni kuwa nikutumie kwenye number ipi?kwa kweli pesa nishatumiwa na hapa nilipo nipo nakarangiza mahanjumati ghetto,nimepata funzo kuwa karne hii ya 21 hakuna haja ya kuachana na mtu kwa maugomvi,bila huyu dada kuokoa jahazi leo ningeshinda na njaa aisee.