Tujifunze machache kuhusu umeme wa mwilini unavyoweza kukusaidia kuishi au kukuharibu mazima

Tujifunze machache kuhusu umeme wa mwilini unavyoweza kukusaidia kuishi au kukuharibu mazima

Na pia ulichoeleza
Kuna sehemu ingine inaeleza uhusiano kati Ya Light and Frequency produced by Human

Human
Hue means different Colors
God said let there be light
Vibrating light turns into matter
Vibrating matter turns into light

Mind have light
Thoughts are produced by frequency where mind is set to
Mind tune it’s frequency to match with thoughts
Example you think about Wealth
Your mind tune into frequency of Wealth

Different wavelengths of light and frequency have different colors

View attachment 3429382

View attachment 3429383
That's not true.

Human si Hue-Man ni Tafsiri tu ya watafiti ila haina maana hiyo uliyoisema hata kwa tafsiri ya biblia ya mwanzo.

Binadamu Linatokana na neno la Kiebrania adamah (×Ö²×“Öø×žÖø×”) — maana yake ni udongo au ardhi.

Hasa udongo mwekundu kwa sababu mizizi ya neno inahusiana na rangi ya udongo dam (×“ÖøÖ¼×) = damu - nyekundu.

Mwanzo 2:7 Biblia ya Kiebrania:
Vayyitzer Adonai Elohim et-ha'adam afar min-ha'adamah…
Naye BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi…

Hakuna rejea yoyote inayotaja mwanga -light, hue - rangi, au frequency ila udongo, pumzi ya uhai, na nafsi.

Kwahiyo kama unamuelezea binadamu kusayansi muelezee kisayansi, Kama kidini muelezee kidini, Ukichanganya unaleta uongo.
 
Si useme tu unataka akwambie chanzo ni Mungu? Bahati akikujibu hivo hutahoji chanzo cha Mungu
Huyu jamaa anaona 10 next moves kuliko unavyoona wewe mkuu.
That's why kasema atakuja na uzi mwingine.
Ameshajua alikuwa na kibarua kingine cha kuelezea Chanzo cha huyo muasisi wa hizo nguvu iwe Mungu au Lah.
 
That's not true.

Human si Hue-Man ni Tafsiri tu ya watafiti ila haina maana hiyo uliyoisema hata kwa tafsiri ya biblia ya mwanzo.

Binadamu Linatokana na neno la Kiebrania adamah (×Ö²×“Öø×žÖø×”) — maana yake ni udongo au ardhi.

Hasa udongo mwekundu kwa sababu mizizi ya neno inahusiana na rangi ya udongo dam (×“ÖøÖ¼×) = damu - nyekundu.

Mwanzo 2:7 Biblia ya Kiebrania:
Vayyitzer Adonai Elohim et-ha'adam afar min-ha'adamah…
Naye BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi…

Hakuna rejea yoyote inayotaja mwanga -light, hue - rangi, au frequency ila udongo, pumzi ya uhai, na nafsi.

Kwahiyo kama unamuelezea binadamu kusayansi muelezee kisayansi, Kama kidini muelezee kidini, Ukichanganya unaleta uongo.
Nimeelezea kiroho

Matthew 5:14 (KJV):
ā€œYe are the light of the world. A city that is set on an hill cannot be hid.ā€

Ephesians 5:8 (KJV):
ā€œFor ye were sometimes darkness, but now are ye light in the Lord: walk as children of light.ā€
 
Sisi sio watoto wadogo.
Nuru hapo amemaanisha maisha yenye haki, upendo, ukweli, na mwanga wa tabia njema

Sio mwanga wa fizikia, hue, wala wavelength.

Kwahiyo kusema We are light because our minds vibrate at frequency of wealth or peace ni tafsiri isiyo ya kibiblia ni ya kisayansi.
 
Ndugu karibuni katika mada hii japo nitasema kwa uchache.

Pamoja na kwamba mimi ni fundi umeme na ujenzi lakini hapa kwa leo nitazungumzia zaidi umeme ambao upo ndani ya miili yetu zaidi.
Nikiwa nafanya kazi zangu za kiufundi umeme huu tunaotumia majumbani nilikuja kubaini kuna uhusiano mkubwa sana wa umeme na maisha ya viumbe.

Hii ikanikumbusha mambo machache niliyokuwa nayafanya zamani pasipokujua!

Zamani nilipokuwa mdogo nilikuwa nikisugua karamu kichwani kwenye nywele halafu kisha nikiiweka chini kwenye mchanga ilinasa chembe chembe zilizo kwenye mchanga!..(nitafafanua mbele)

Kitu cha pili nilichokumbuka ni baada ya kumaliza msingi na kufaulu vizuri kwenda Moshi technical, katika kuweka mambo sawa nikaenda kwanza kutafta kibarua cha kuchunga ng'ombe huko hanang.
Nidhamu yangu ya uchungaji ilinitofautisha pakubwa sana, nakumbuka Mifugo wangu niliwaelekeza kwa sauti, ishara na majina,

Baada ya kuona mifugo wamenielewa nilibaini hata nikiwa porini na wafugaji wenzangu mifugo wangu walijitenga na makundi wao wenyewe wakati wa marisho;

Niliwafundisha mifugo kipi ni halali kwao kula na kipi hakifai kwao kula!
Ilifika wakati nilikuwa na uwezo wa kupita na ng'ombe kwenye mipaka ya shamba na shamba nikiwa nimenyoosha mkono wangu na fimbo juu nikiwa mbele na mifugo wakinifuata kwa nyuma na hakuna aliyekula mahindi ya mtu hadi tukivuka nakushusha mkono ndipo wanaanza kula majani.

Baadhi ya wachungaji wenzangu waliamini tunatumia uchawi!

Jambo la ajabu zaidi ni pale ng"ombe walipochungwa na mwingine walionekana kuwa hawakushiba tofauti na ninavyo wachunga mimi!
Hata maziwa alipokamua mtu mwingine hayakupatikana mengi kama nilivyokamua mimi!..(nitafafanua baadae)

Kitu cha tatu ninachokikumbuka; Baba angu alinionya kwa picha kipindi hiko magonjwa ya kaswende yalivyosumbua siku moja alinionesha picha ya uume uliooza na akaniambia Tazama, Huyu alivyojaribu kufanya mchezo mchafu kilichomkuta, kwahiyo kuwa makini wanawake wanaweza kukubana hadi hiko kidude chako cha mkojo kikakatika, Niliishi kwa hofu nikikumbuka picha na maneno ya mzee!

Sasa nikiwa huko marishoni kuna mama mmoja alikuwa akishi huko shambani alitengwa na familia yake kwasababu mimba yake iliharibika" Zamani makabila ya huko yaliamini mimba kutoka ni laana, na ili laana itoke mwanamke anatengwa inje ya nyumba hadi atakapo pata mimba ndipo anaweza kurudi nyumbani!

Sasa swali nani wa kumpa mimba mwingine inje ya nyumbani kwake?
Maanake Watu wa kuja kutoka mikoani ndio walitumika maana hawajui;
Sasa basi akawa ananiita, Ila kuna siku akaniita nikakuta yupo uchi Aisee nilitoka nduki nilijua yale mambo ya kukatwa kikojoleo niliyoambiwa na mzee wangu ndo yalifika.
Cha ajabu zaidi nilipoondoka mbio nikaona na kundi la mifugo likinifuta mbio hadi tulipofika mbali tukasimama na mifugo nao wakasima (tuweke pozi hapa)

SASA TURUDI KWENYE MADA RASMI

Matukio haya machache hapo juu yalinifanya nidadisi sana (kwanini?) Nimekuja kubaini kwamba,

Huu ulimwengu tunaoishi unaongozwa na nguvu kuu 4 Sizizoonekana kirahisi kwa macho ya binadamu
  1. Nguvu mvutano (Gravitational)
  2. Nguvu ya charge (Electric Field)
  3. Nguvu ya atomiki
  4. Nguvu ya mionzi
Mambo yote haya hayaonekani kwa macho lakini yana mchango mkubwa wa viumbe kuwepo.

Yanafanyaje kazi?

Iko hivi, huu ulimwengu kama ambavyo maji yalivyo ungana na samaki viumbe wa baharini

Ndivyo hata anga hili lilivyoungana na viumbe wote akiwemo binadamu kwa njia ya chaji ya magnetiki.

Ngoja nifafanue hiki hapa
Tangu ulimwengu ulipoanza, ulikuja ukiwa kamili na mifumo yake ya umeme!

Charge ya umeme dunia unasafiri kwa mawimbi kutoka incha ya kaskazini kwenda incha ya kusini kwa kuzunguka kwa frequency maalum!

Kule shule ya msingi tulijifunza mzunguko wa chaji ya sumaku kutoka KAS kwenda KUS unavyozalisha mkondo wa chaji ( Magnetic field)

Ndivyo ilivyo huu ulimwengu ulivyo!
Kuna charge zinatembea ambazo huwezi kuziona kwa macho ila zipo kwa kazi maalum kama GRIDI YA MAISHA!

Je binadamu zinamsaidiaje?

Mwili wa binadamu na viumbe nao umeumbwa kwa sura na mfano wa ulimwengu (the Master)

Mwanadamu kaumbwa akiwa na mishipa ya damu ambamo husafirisha chaji za umeme kutoka kwenye moyo na ubongo kwa mtindo uleule wa kuzunguka (Magnetic field)

Binadamu katika ubongo wake kuna mzunguko wa mawimbi ya charge yanayoshabihiana na mzunguko wa frequency za ulimwengu!

Na endapo ikitokea jambo lolote likafanyika kupishanisha mawimbi binadamu anaanza kuwa kichaa.

Je Hizo chaji za binadamu zinaunganishwaje na ulimwengu?

Kumbuka huu ni umeme usioonekana! na katika kuweka sawa ni kwamba Umeme siyo waya, umeme siyo nguzo, umeme siyo mtu!

Bali umeme ni nguvu isiyoonekana inayosafiri kupitia mambo hayo!

Kwa maana rahisi ni kwamba Umeme kwenye mwili wa binadamu unaposafiri kama chaji kwenye damu ndiyo huamua yote afanyayo mwanadam.

Kwa maana rahisi kama umeme huwezi kuuona maana yake umeme unaweza kupenya kama roho ndani ya mwili kwa mtindo wa mawimbi.

Binadamu anaunganikaje?

Nimesema hapo mwanzo, Mzunguko wa chaji za ulimwengu kutoka KASKAZINI kwenda KUSINI zimeunda frequency ya ulimwengu kama GRIDI, na ulimwengu umejaa njia nyingi za chaji (magnetic fields line)

Binadamu anapoishi anaungana na hizo line ili kupata chaji ya uhai

Kwa lugha rahisi ulimwengu ni kama Tanesco ya ulimwengu ! Na kila nyumba imechota umeme kwenye nguzi iliyokaribu!

Chaji za umeme ndani ya mtu zinatokaje kuungana na ulimwengu?

Kumbuka hazionekani lakini zipo mwilini zinatembea! Sasa iko milango inayoingiza au kutoa umeme ndani ya mwili.

Milango yote ya fahamu inatumika kuingiza umeme au kutoa ndani ya mwili.

Lakini mwili unaweza kutoa chaji au kupokea chaji haswa kwa maeneo ya Pua-mdomo, mikono, miguu, kichwa na kifua.

Ngoja nilifupishe somo hili kwa kurejea wanyama hawa.

Kwanini paka au mbwa anaona mtu anaekaribia kufa?

Baadhi ya wanyamakama PAKA wanauwezo mkubwa wa kuona chaji za umeme kama sisi tunavyoona nguzo na nyaya za umeme majumbani.

Paka au mbwa ana uwezo wa kuona mgongano au mdororo wa frequency zinazokatika kwa binadamu.

Yaani kama vile ukipita usiku watu wamelala halafu inje kwenye nguzo walipochukulia umeme kuna cheche au shoti zinavyoaashilia nyimba itazima umeme!

Ndivyo wanyama huweza kuona muelekeo wa mtu anaekaribia kutengana na frequency za ulimwengu hapi ndipo huanza kusononeka usiku kabla ya watu kujua kuna msiba!

Je frequency za ulimwengu ni ngapi na za binadamu ni ngapi?

Huu ulimwengu una unazungusha chaji kwa frequency za wastani wa (7Hz hadi 14Hz) inategemea sehemu na sehemu!

Lakini katika dunia hii frequency za umeme zilizopo ni 7.83Hz ambazo zinafanya liwe ni eneo salama kwa viumbe.

Maana binadamu ndani ya damu mzunguko wa umeme ndani ya mwili unatembea kwa frequency ya wastani wa 1Hz na ule wa ubongo unatembea kwa kwa wastani wa frequency za umeme wa 4-7Hz.

Utagundua mtu akituliza kichwa sawa sawa anaweza kuzisawazisha frequency zake zikasomana kabisa na frequency za ulimwengu ambazo ni 7.83Hz

Sasa mambo gani huchangia binadamu tupishane na frequency hadi kutoka kwenye Grid ya Kufa mapema?

Iko hivi binadamu ambaye aweza kutembea sawasawa na gridi ya umeme ananafasi kubwa sana ya mafanikio!
Mambo yafuatayo yanachangia sana kuharibu frequency za maisha ya kila mtu.
1. HASIRA Yaani katika mambo yanayochangia uanze kutembea inje ya frequently zako ni Hasira.
Yaani ukiwa una hasira unahamishwa fasta kutoka kwenye njia zako bila kujua maana ubongo utabadili mapigo na moyo pia hubadili na kupishana na frequently za ulimwengu.
2. NGONO; Hili eneo peke yake linahitaji mada yake nitafafanua siku nyingine; lakini tambua unapojamiiana unakuwa unazungusha chaji za umeme mnabadilishana, kuna baadhi huingia kwenye damu zingine hubakia mwilini (kuna njia zake za kuziondoa nitafafanua katika ma yake)
3. KUBADILISHWA NA WENYE UJUZI
Hapa nazungumzia wenye maarifa wanaweza kukutoa kwenye frequency zako na kukuvika frequency mbovu ambayo nyie mmezoea kuita mapepo ingawa kiuhalisia siyo mapepo bali Kubadilishwa ueleko wako wa umeme unakuja kukuletea cheche za shoti ( Ni kama dishi likichezewa unavyoona tv inaonesha chenga chenga)

Michezo ya kupasua nazi njia panda ni ishu za umeme!

Makutano ya njia wanapopita watu huunda njia za magnetic za watu wengi! Hapo ni pazuri sana kumhamisha mtu njia kama vile makutano ya reli ambavyo ni rahisi kubadilisha treni njia.

Nimefupisha ili nisiwachoshe lakini katika yote hayo zipo njia za kufanya kusawazisha frequency ambazo mnapigwa pesa na waganga kumbe mnaweza kujifanyia wenyewe katika maisha yenu.

Natoa mfano mdogo!

Watu wengi wakienda bichi huamini kule bichi kuna mazingaombwe!

Ukweli ni kwamba unapokwenda beach mtu unakuwa unavua viatu!
Kile kitendo cha kuvua viatu na kukanya mchanga na maji unakuwa unafanya DISCHARGE ya umeme Usiofaa ndani ya mwili kuelekea ARDHINI. tukio hilo husawazisha Frequency zako zitulie.

Kama bahari peke yake ni tiba mbona mabaharia hujitupa kwa stress baharini?

Jibu ardhi ukiikanyaga pekupeku unaruhusu umeme mchafu utoke mwili na kubalance Frequency zirudi normally.

Sijui sana kuandika vizuri mtanivumilia kwa mwandiko nyie wasomi lakini kwa leo nishie hapa nitafafanua tena tena baadae!

Note; Ukiweza kutuliza Frequency zako zikawa sawia kabisa na zile za ulimwengu unaweza hata kutembea juu ya maji na usizame!
Unaweza kunyoosha mikono kwa mtu na mtu huyo akapigwa shoti kama shoti ya umeme wa majumbani, unaweza kupita popote na kufanya lolote.

Zipo njia ukiweza kuzijua unaweza kujitibia hata wewe kwa kusawazisha Frequency hata yale mambo sijui ya PRESHA, sijui HORMONE IMBALANCE, yaani takataka zote haziwezi kutokea maisha yako yote

Kama kuna swali nitafafanua mbele au wakati ujao.
Hii mada nimeipenda maana imegusa vitu vingi kwa wakati mmoja ambapo kila kimoja kina ufafanuzi wake mkubwa tu lakini chanzo cha yote ni uhusiano wa mnyama na nguvu za asili za ulimwengu. It's like a TOPIC WITH ITS SUBTOPICS
Cheers mkuu
 
Kuna kipindi enzi hizo nilikuwa nikivua vest Ile inavyonivuka inatoa cheche balaa, Jana nilikuwa namfunika shuka Binti yangu kitandani kwake nilivyogusa Sweta lake nikapigwa shoti nilishituka
 
Uwe unachanganya Konyagi na Soft drinks mfano Tangawizi Stoney, Cocacola na Sprite mkuu.

Hiyo mixer ya Energy drink ni kitu Danger sana mkuu, Unakua umelewa ila Energy inakupa nguvu so inakudanganya hujalewa, Hapo lazima ufanye mambo ya kisuper Hero šŸ˜‚
Haha kwahiyo hapo ubongo ndio unapata kazi ya ziada ku equalize mambo ndani ya mwili. Kama hauli vizuri mwili unadhoufika na mikunyanzi kwenye ngozi. Tunajitesa sana bila kujijua aiseešŸ˜€
 
Kwahiyo kusema We are light because our minds vibrate at frequency of wealth or peace ni tafsiri isiyo ya kiBiblia ni ya kisayansi.
i mean
Genesis 1:3 ā€œLet there be light.ā€ We live inside of a lightwave universe where all things are created out of light. Low vibrating light turns into matter, high vibrating matter turns back into light.

ā€œGod is thinking mind. The substance or body of God is light.ā€
The one universal substance, a thinking substance, comprehensive and describable and possessed of principles which are familiar to man through man's observation of the one universal substance in created things.

The substance of all created things is light.

The one substance of thinking mind is all that exists.
Mind is expressed in light.
As a hue man, we are an attribute of a colour that permits them to be classed that specific colour.

Each individual is the mind, not the physical body. Without the mind the physical body/world would cease to exist. The mind is spirit.

The mind is the intellect that manipulates the physical body and the world around us.

The mind is like a frequency tuner, tuning itself into different frequencies.

The mind exists within the mental plane, which is shared between all the minds of the universe.

Thoughts are not created by the individual; they are received based on what frequency our mind is set to.

If we set our mind to a specific topic, like generating wealth, for example, we tune into that frequency in the mental plane, and we will receive thoughts on how to generate wealth.

Our mind is generally operating off one specific frequency based upon our daily thinking patterns.

Every frequency is a colour. Therefore, our mind is manifesting colours within the astral plane based upon what frequency our mind is generally operating off.
C900DA94-8338-4562-8C92-EFE52FD170C1.jpeg

If we are carrying hate in our mind, we will be generating reddish colours. This is why the word human means an attribute of a colour.

We should aim to become violet, the highest vibrational colour within the light spectrum. Which is highest Frequency

We are light beings manifested into physical form.

Do you know why Jesus walked on Water?
 
Kuna kipindi enzi hizo nilikuwa nikivua vest Ile inavyonivuka inatoa cheche balaa, Jana nilikuwa namfunika shuka Binti yangu kitandani kwake nilivyogusa Sweta lake nikapigwa shoti nilishituka
Alf kwenye giza unaona vishot
 
i mean
Genesis 1:3 ā€œLet there be light.ā€ We live inside of a lightwave universe where all things are created out of light. Low vibrating light turns into matter, high vibrating matter turns back into light. ā€œGod is thinking mind. The substance or body of God is light.ā€
The one universal substance, a thinking substance, comprehensive and describable and possessed of principles which are familiar to man through man's observation of the one universal substance in created things.

The substance of all created things is light.

The one substance of thinking mind is all that exists.
Mind is expressed in light.
As a hue man, we are an attribute of a colour that permits them to be classed that specific colour.

Each individual is the mind, not the physical body. Without the mind the physical body/world would cease to exist. The mind is spirit.

The mind is the intellect that manipulates the physical body and the world around us.

The mind is like a frequency tuner, tuning itself into different frequencies.

The mind exists within the mental plane, which is shared between all the minds of the universe.

Thoughts are not created by the individual; they are received based on what frequency our mind is set to.

If we set our mind to a specific topic, like generating wealth, for example, we tune into that frequency in the mental plane, and we will receive thoughts on how to generate wealth.

Our mind is generally operating off one specific frequency based upon our daily thinking patterns.

Every frequency is a colour. Therefore, our mind is manifesting colours within the astral plane based upon what frequency our mind is generally operating off.
View attachment 3429424

If we are carrying hate in our mind, we will be generating reddish colours. This is why the word human means an attribute of a colour.

We should aim to become violet, the highest vibrational colour within the light spectrum. Which is highest Frequency

We are light beings manifested into physical form.
Is this article Religious or Scientific? Or both?
Do you know why Jesus walked on Water?
From what I know, Never happened.
No man ever walked on water.
Water holds on no man.

Can tell me how He did it?
What really happened out there?
 
Haha kwahiyo hapo ubongo ndio unapata kazi ya ziada ku equalize mambo ndani ya mwili. Kama hauli vizuri mwili unadhoufika na mikunyanzi kwenye ngozi. Tunajitesa sana bila kujijua aiseešŸ˜€
Pombe kali.
Msosi kiganja kimoja.
Bibi zee.
Ganja.
Kamari.

Noma mkuu!!
 
Both
Can tell me how He did it?
What really happened out there?

Jesus was walking on top of the veil of the ether (astral projecting).
E325D151-8AB5-42C8-AA60-7681D3C51C03.jpeg

For leaving the physical body. The water is the etheral plane, which is the veil between the physical world and the astral world.

Jesus was walking on top of the veil of the ether (astral projecting).

When Jesus teaches Peter to ā€œwalk on water,ā€ he is teaching him not to be scared or else you will fall back into the water.
This is symbolic of when you are astral projecting. When you start to fear when you're projecting, you will be sucked back into your body.

Anxiety lowers you into lower dimensions
Peter was returned into Physical Plane

Mathew 14:29
ā€œhe was afraid and, beginning to sink, cried out, ā€œlord, save me!

That’s why Witches , Demons and Satan use ways to create Anxiety to a person in order to lower them into lowest dimensions
But God says

2 Timothy 1:7
ā€œFor God hath not given us the spirit of fear; but of power, and of love, and of a sound mind.ā€

Do you know why during night hours our spirits are active and easy to ascend into spiritual realm?
 
Back
Top Bottom