Tujifunze pamoja na tuelimishane kuhusu program ya Excel

Urban Edmund

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2018
Posts
2,250
Reaction score
3,607
Katika programu nzuri na tamu katika ukokotoaji, uchambuzi, uwasilishaji wa data zilizopo katika namba na kupanga mambo mbalimbali ya kihesabu tunajua Excel Ina fanya yote hayo, Excel imekua ikitumika karibia Kila professional ikiwemo Engineering, Accounting, Medical professions na nyingine nyingi.

Hivyo basi sababu tunajua Excel ni pana sana na haiwezekani mtu kujua Kila kitu naomba tupia ukijuacho kuhusu Excel ili tupate elimu ya programu hii tamu ambayo inatumiwa na kila wataalamu katika kufanya kazi zao "kivyao" kama unaijua formula usiache kutujuza Kwa mfano mi naanza na hizi chache Hapo chini
 
=LOOKUP(N19,{0,11,21,31,41},{"'E'","'D'","'C'","'B'","'A'"}) hapo maana yake Nini nimeweka vigezo vya seli yangu kama imefikia 0-10 maana yake itaonyesha kapata E, aliepata 11-20 itaandika D nk kumbuka kile kigezo kinachotokana na namba ulizopanga kukiwekea hizi sign" "
Nimemaanisha seli ya N19 kama imefikia vigezo inabadilika na kuwa hizo herufi

Au

=Lookup(N19,{0,10000,100000,1000000,10000000,100000000},{"HANA HELA","ANA HELA YA MAJI","HELA ANGALAU YA SUPU","ANAJITAHIDI ANAWEZA ANGALAU KUHONGA","ANAJITAHIDI NA ANAWEZA KUHESHIMIWA MTAANI","KAPAMBANA SANA NA YUKO VIZURI SANA"})
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…