Tujikumbishe kidogo maisha ya vijijini

Mie nakumbuka raha ya kunya polini,
Pia kuna siku tukiwa wadogo tulienda kucheza mpila kijiji cha jirani wakatufunga goli kumi na mbili kwa moja niliumia sana mpaka nikamwambia rafiki yangu tuwaache wenzetu watangulie nyumbani sisi tubaki mpaka usiku tukaenda kunya mavi ndani ya kisima cha kijiji kisha tukasepa mpaka leo hii hatujawahi kutoa siri nahisi hata rafiki yangu alishaga sahau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahah we jamaa barna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha ya kinyama nyama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kama kuna hatua niliyoruka katika michezo ya utotoni.

Nimecheza michezo mingi sana ya utotoni

Michezo kipindi sijaanza kusoma shule,
Michezo wakati wa kuchunga ng'ombe
Michezo kipindi nasoma shule ya msingi
Aina mbalimbali za kutega ndege(kwa urimbo, upinde na Mshale, mpira kama wakufungia mizigo kwenye baiskeli au pikipiki, kutega ndege kwa kutumia maboga, n.k)

Nimewinda ndege, sungura, digidigi, pimbi kwa kutumia Upinde na Mishale, Marungu, Mbwa.

Mpira ndio nimecheza sana.
 
Ki baba babaa je?
 
Ki baba babaa je?
Huko ndio usiseme sasa, nimecheza sana.

Nimecheza rede(nilikuwa napenda kuingia kama mtu wa kotekote), mchezo mmoja sisi tunauita IKHALU( upo kwenye picha hapo juu watoto wanarusha kajiwe juu huku wakiingiza vijiwe vingine kwenye kashimo kadogo chini), mwingine tulikuwa tunauiya CHAILETI (tunachora madrafti chini makubwa halafu unachukua kajiwe unaanza kukasukuma kiruke hayo madrafti kwa mguu mmoja huku mwingine ukiwa umeukunja usiguse chini), mchezo wa kushika kamba watu wawili halafu mmoja akiwa katikati anarukaruka.

Hiyo ni baadhi tu ambayo tulikuwa tunacheza tukiwa mix na wasichana
 
Hadi rede duuh
 
Atasahauje kunya porini nakati alijichamba kwenye miamba ya mawe au kupitia vibunzi vya mahindi?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…