Hiyo ya matairi sie tulikua tunayaendesha kwa kutumia miti. Unakua na miti yako miwili ya kama mita moja moja hivi unaingiza ndani ya tairi kila upande unaanza kuendesha. Sasa ili miti kule ndani ya tairi iteleze vizuri bas inabidi umiminie maji, oil chafu ya magari, mafuta ya kula, etc. Hata na sie "magari" yetu yalikua yakitumia "Wese"
MachoweraMkuu huo mchezo kwenye picha ya pili unaitwaje kwa lugha yenu? Sisi tunaita mgabo
Sent using Jamii Forums mobile app
Huo wa madraft tuliuita tikiriHuko ndio usiseme sasa, nimecheza sana.
Nimecheza rede(nilikuwa napenda kuingia kama mtu wa kotekote), mchezo mmoja sisi tunauita IKHALU( upo kwenye picha hapo juu watoto wanarusha kajiwe juu huku wakiingiza vijiwe vingine kwenye kashimo kadogo chini), mwingine tulikuwa tunauiya CHAILETI (tunachora madrafti chini makubwa halafu unachukua kajiwe unaanza kukasukuma kiruke hayo madrafti kwa mguu mmoja huku mwingine ukiwa umeukunja usiguse chini), mchezo wa kushika kamba watu wawili halafu mmoja akiwa katikati anarukaruka.
Hiyo ni baadhi tu ambayo tulikuwa tunacheza tukiwa mix na wasichana
Aseeee ni huyo mimiTushaweka sana vioo chini ya madawati kwa ajili ya kuwachungulia dada zetu
Sent from my iPhone using JamiiForums
Una majina kulingana na kabila, sisi tuliuita jinsi nilivyoubainisha
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]Mi nakumbuka mchozo flani wa karata tuliuita KIBOY ni kama last card, yan unacheza anaebak na karata kubwa wa mwisho anapigwa vibao kama thaman ya karata, mfano ukibaki na joker unapigwa vibao hamsini, kuna jamaa alibaki na joker na namba mbili zilikuwa mbili yani hapo anatakiwa vibao mia, asee jamaa alipigwa hadi akaingia chini ya stuli
Sent using Jamii Forums mobile app
Daaaah, nakumbuka darasa la 3 nlimuwekea kioo Dem tukiwa tunafundishwa somo la sayansi,tulipokea kichapo heavy na sitosahau [emoji114]Tushaweka sana vioo chini ya madawati kwa ajili ya kuwachungulia dada zetu
Sent from my iPhone using JamiiForums
Hicho kipande cha chungu kwetu kilikuwa kinaitwa Kimadi...[emoji2]Hahahaaa we nae bwana ulikuwa unacheza michezo ya kike, hapo kwenye kuruka kwenye madrafti chini ndio mchezo nimecheza pengine kuliko yote...ila hapo kwenye jiwe tulikuwa tunatumia kipande cha chungu kilichovunjika tena tulikuwa tunatunza ukimaliza kucheza unarudi nacho nyumbani na kilikuwa na jina lake sema nimesahau
Sent using Jamii Forums mobile app