Tujikumbushe enzi za ufalme wa Inspector Haroun

Kwenye album ya kwanza umesahau ngoma inaitwa MTU BEE. Iyo ngoma wakati inalekodiwa mi nilikuwepo ndani ya studio imefanyika kwa mastar j. Na tukachukua ngoma aliyofanya na mr. Poo inatwa buzi.

Hiyo MTU BEE ya kitambo sana na ndio iliyowatambulisha Gangwe Mob ilitoka 1999,
"Mtu bee chelea pina"
 
Hahaha upo kama mimi bro,

Kwa mara ya kwanza nakanyaga ardhi ya Mbagala viwanja vya Dar live ilikua sababu ya show ya Nature, aiseee kuna mjinga akatangaza eti Nature hayupo basi ilitokea bonge la fujo mpaka akapanda jukwaani kabla ya muda wake kusalimia mashabiki ndio watu wakatulia.

My fav artist of all the time.
 
Hivi kuna mtu mwenye wimbo Wa simulizi za ufasaha Wa gangwe mobb?
 
Kuna nyimbo moja ya kibabe sana inaitwa "bunda siliga"
japo nimeisahau kidogo.

Chorus:
Bunda siliga kiatu mtu
Hima saka mpira usijitusu
Huu thubutuu
 
Liongo wewe, hata aibu hauna.
Inspector alikua TMK wanaume???
Ndege tunduni walimtungia Inspector????
Sema jamaa kachanganya mafaili...Inspector alisikika kwenye ngoma ya ndege tunduni..mi mwenyewe sikumbuki ilikuwaje mpaka akaibukia TMK wanaume Halisi..
 
Nature alishiriki chorus nyingi zikafanya vizuri ndio maana watu waliamini yeye ndio king wa chorus. Q Chief alipita fresh pia kwenye 'kama unataka dem' wa Mo, watu wengi walikuwa wanasema kaimba demu
 
Ana nyimbo alitoa mwaka juzi kamshirikisha j moo bonge moja la nyimbo inaitwa january to december,humo anachambua hali ya kipato na matumizi ya mtanzania wakawaida kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa kuminambili,kuanzia aina ya milo mpaka matanuzi.Namkubali sana jamaa anapozungumzia misosi.pia kuna nyimbo nimeisikia juzi kati sijui inaitwaje,jamaa bado ni msanii mzuri,amekosa tu management na promo

 
Sema jamaa kachanganya mafaili...Inspector alisikika kwenye ngoma ya ndege tunduni..mi mwenyewe sikumbuki ilikuwaje mpaka akaibukia TMK wanaume Halisi..
Alijiunga Wanaume Halisi japo hakukaa mda mrefu, Nature na wenzake baada ya kujitenga na Fella baadaye wakaamua kumtafuta na Inspekta kuunganisha nguvu wapambane na TMK ya Fella, kwenye wimbo wa tatu bila Inspekta anasema 'Pumzika pema babu kitambi....' Akimchana Fella
 
Ila jamaa naye katudanganya, kwenye yale mashindano Inspector hakuwa na influence yoyote, maana kulikuwa na vichwa vinaandika hatari sio mistari yake ya kuungaunga. Watu waliokuwa tishio ni Profesa Jay, SoloThang na Afande mwenyewe
Nikweli mkuu nafasi ya inspector kwenye yale mashindano ilikua ni ndogo
 
Demu mmoja ana rangi 6 ana urefu wa saiz tofauti ana maumbo 2 tofauti [emoji3][emoji16][emoji16][emoji16]yaani alikuwa anarudia rudia maneno tu....ila dude tamu
 
Kweli,waliona mbali sana na pamba zao "gangwe gear" nadhani walikuwa wanasimamiwa na Sebastian Maganga
 
Ila jamaa naye katudanganya, kwenye yale mashindano Inspector hakuwa na influence yoyote, maana kulikuwa na vichwa vinaandika hatari sio mistari yake ya kuungaunga. Watu waliokuwa tishio ni Profesa Jay, SoloThang na Afande mwenyewe
Upo RIGHT kwa 100%!! Wana Kiumeni (TMK in general) tulikuwa tunamtegemea Nature na sio Inspector ambae by the time alishaanza kuzimika kutokana na nguvu ya TMK Wanaume ambayo ndo kwanza ilikuwa inakuja juu kwa kasi!

Tulimtegemea (Remember, deep inside my heart nilijua hatutoki mbele ya Darubini Kali) Nature kwa sababu, kama kumbukumbu zangu zipo sawa; shindano la Mkali wa Rhymes lilikuja muda mfupi baada ya uzinduzi wa Ugali pale Diamond Jubilee huku Sitaki Demu na Inaniuma sana zikiwa zinasumbua kitaa!
 
Nikweli mkuu nafasi ya inspector kwenye yale mashindano ilikua ni ndogo
Aliingia kujaza nafasi tu, maana mule ndani kuna vichwa vilikuwa vinaandika kweli kama Prof Jay, SoloThang,JayMo,Afande,Mwanafalsafa,Soggy, sasa hapo angetoboaje?[emoji16], sema kwa rap katuni hakuwa na mpinzani. Nature alilalamika kwakuwa hakuingizwa kwenye mashindano, nikamshangaa aingizwe kwa mistari ipi?[emoji16][emoji16][emoji16]. Nakumbuka mwaka uliofatia walijaribu kutafuta Mkali wa Rhymes tena ila ikafeli za chini chini zilisema alipangwa mshindi washiriki wakajitoa, sema Fid alikuwa na nafasi ya kuchukua ndio alikuwa kwenye peak kwa wakati huo. Kwenye mistari yake anakwambia 'Washanitabiri watu wangu wa mtaani, mi ndio mfalme nitayefuata baada ya Suleiman...'
 
Kwenye album ya kwanza umesahau ngoma inaitwa MTU BEE. Iyo ngoma wakati inalekodiwa mi nilikuwepo ndani ya studio imefanyika kwa mastar j. Na tukachukua ngoma aliyofanya na mr. Poo inatwa buzi.
[emoji116][emoji116] [emoji121][emoji121]
Hiyo MTU BEE ya kitambo sana na ndio iliyowatambulisha Gangwe Mob ilitoka 1999,
"Mtu bee chelea pina"
 
Yule alikuwa KING haijapata kutokea!
Km kutamba enzi zile basi nature na wanaume tmk walitisha!ndo zetuuuuuu wanaume ndo zetuuu we ukitaka tende chukua ila babu kundu panua
 
Hata Nature asingetoboa, kumbuka Mkali wa Rhymes walikuwa wanaangalia sana kigezo cha uzito wa mashairi na sio performance tu jukwaani. Nature na Inspekta hicho kigezo hawana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…