Tujikumbushe mabeki hodari waliochezea timu zetu Tanzania miaka ya 90

1. Ruben Mgaza
2. Bakari Malima "jembe ulaya"
3. Anwar Awadhi "Kaito"
4. David Mwakalebela "Ninja"
 
Huyo Deo Njohore Ni Mtanzania Kweli au Ni Mghana? Naomba Ufafanuzi!

Mtanzania mkuu,kuna kakayao Bonifase Njohore nae alicheza Simba kitambo alikuwa kiungo matata Sana,na mdogowao wa mwisho aliyecheza miaka ya 90,anacheza mpira wa kulipwa Ulaya...
 
Wewe Umeambiwa Utaje Beki Bora Wa Enzi Hizo Unatuletea Upuuzi Wako Huu Wa Kututajia Kikosi Cha MAPOPOMA Wenzio Yanga. Umeniboa!

wewe ndio Popoma kweli....hivi kwani hapo hamna mabeki? au waliotajwa hapo wote ni makipa na washambuliaji?

Namba 2,3 Na 4 Ndiyo Waliokuwa Mabeki Wakali Na Huyo Aliyebaki Alikuwa Ni POPOMA Tu.
yaani wewe Gentamucine Akili zako nafananisha na akili za Ndezi au Samaki aina ya Pono.

Hapo Wenye AKILI Na Mabeki Imara Walikuwa Ni Pawasa Na Modest Peke Yao Waliobaki Walikuwa Ni Makatuni Tu Uwanjani Nikimaanisha Hawajui.
wewe ni Popoma sana.... yaani unamtosa mtu kama Chibe Chibindu ?
 
Last edited by a moderator:
Marehemu Kizota alitoka kucheza senta fowadi mpaka senta hafu. Kwakweli jamaa alikuwa na kipaji sana.

Alikuwa na kipaji cha hali ya juu sana, uhuni wake ndani ya uwanja ulimfanya ashindwe kucheza ulaya.
 
George Magere Masatu
Said Mwamba Nassoro Kizota
Alphonce Modest
Bakari Malima
David Mwakalebela
 
Alikuwa na kipaji cha hali ya juu sana, uhuni wake ndani ya uwanja ulimfanya ashindwe kucheza ulaya.

Hahahaha,jamaa alikuwa mbaya sana kwa Viwiko a.k.a Vipepsi,ilikuwa ukienda nae juu kuwahi mpira wa juu ukishuka chini lazima ndio iwe mwisho wako wa Game. Na kitu kingine kilichomuharibu jamaa ni Masanga,jamaa alikuwa mnywaji mzuri sana wa Bia.
 
Mustafa Hoza.
 
Ebwana Nimecheka Mpaka Basi! Yaani Leo Msamiati Wangu Nilioutoa Wa POPOMA Umenirudia? Umenivunja Mbavu Zangu Sana Mkuu.
 
Huyu alikuwa andunje kiasi fulani kwa vimo vya mabeki wa kati, ila kama ana springi miguuni vile.

Huyu alivyokuja Popadic pale Simba alishangaa kuona stopper ambae ni mfupi.. Alichofanya alimrudisha Masha kati, Hoza akapewa namba 4 na Masatu akapewa beki wa pembeni.. Kwenye timu ya taifa Mustafa Hoza akawa ndo stopper na Masatu akawa anacheza namba 4.. Zamani Stopper alikuwa ni beki wa kumaliza na ambae hakabi.. Namba 4 ndo aliekuwa na shughuli ya kufa mtu pale..
 
Hapo Wenye AKILI Na Mabeki Imara Walikuwa Ni Pawasa Na Modest Peke Yao Waliobaki Walikuwa Ni Makatuni Tu Uwanjani Nikimaanisha Hawajui.
chibe chibindu ilikuwa mpira unaenda wewe unabaki au wewe unaenda mpira unabaki
 
Mohammed Bakari Tall
Elisha John
Ahmad Amasha
Constantine Kimanda
Method Mogella
Said Kolongo
Kasongo Athumani
Jembe Ulaya
 
Hahahaha,jamaa alikuwa mbaya sana kwa Viwiko a.k.a Vipepsi,ilikuwa ukienda nae juu kuwahi mpira wa juu ukishuka chini lazima ndio iwe mwisho wako wa Game. Na kitu kingine kilichomuharibu jamaa ni Masanga,jamaa alikuwa mnywaji mzuri sana wa Bia.

apumzike kwa amani
 
mbona sijamuona hapo JELA MTAGWA?LEODGAR TENGA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…