Asante! Umenisemea 75%. Kujikumbusha tu majina ni sawa na kusema "watoto waliozaliwa usiku wa Pasaka wako kadhaa, data hiyo inasaidia nini katika maendeleo ya nchi hii?
Wenzetu wanakusanya data za watoto waliozaliwa kila mwaka na wanawanawandalia mipango mbalimbali kama vile madarasa ya kila level watakayopitia kitaaluma pamoja na mahitaji mengine yatakayohitajika kila hiyo level kama madawati, vitabu, walimu, n.k.
Hata hivyo uzi huu umenifanya ni mkumbuke mbunge wangu Tuntemeke Nnungwa Sanga (R.I.P.) wa wilaya ya Makete kwa wazo lake la ku-pack maji katika chupa na kushauri maji hayo hata ikiwezekana yauzwe katika nchi ambazo hawana maji safi ya kunywa. Wabunge wenzake wengi walimcheka sana kama walivyomcheka Mh. Mbatia na hoja yake ya mitaala ya elimu, wakimwambia amefilisika kisiasa.
Kile kilichoshauriwa wakati huo na kuchekwa, leo kinatekelezeka tena kwa ufanisi mkubwa! Natamani angekuwapo ili aone mawazo yake yakifanya kazi. Leo angekuwepo angekuwa mwana-CHADEMA bila shaka, ni mawazo yangu!