Tujikumbushe Majina ya wabunge wa zamani

Tujikumbushe Majina ya wabunge wa zamani

Baadhi ya Wabunge wa Mwanzo baada ya Uhuru (miaka ya 1960 na 1970): Mwakitwange, Jeremia Bakampeja, Edwin Allan Gakobe Nyamubi, Paul Bomani, Madoshi Fung'ho, Rashid Kawawa, Frederick Nteminyanda Fumbuka, Said Ngw’anangw’alu, Leons Ngalai Silayo, Eliufoo, Said Maswanya, Chief Adam Sapi Mkwawa, Chief Erasto Mang'enya, Chief Abdallah Fundikira, Chief Humbi Ziota, Chief Stanslaus Kasusura, Chief Abuu T Kiwanga, David Zimbihile Bakanyoma, Julie Manning, Chief Herman Elias Sarwat, Nsiro Swai, Henry Mnyetoi Limihagati, Nangwanda Sijaona, Oscar Kambona, Peter Kisumo, Kitwana Kondo, Elinawinga, Thabitha Siwale, Joseph Kaselabantu, Richard Saimora Wambura (Baadae China), Edward Barongo, Joseph K. Nyerere, Daniel Machemba, Dr. Wilbert Chagula, Hussein Shekilango, Alphonse Rulegura na Derek Bryson.
 
Wabunge wakongwe wa bunge la kwanza la Tanzania (1965-1969):
Hawa ndio walikuwa the big 8 wa enzi hizo
(1) Lwantyantika Masha(Geita Mashariki)
(2) Joseph Kaselabantu (Nzega Mashariki)
(3) Wilfred Mwakitwange (Taifa)
(4) Stephen Kibuga (Mufindi)
(5) Modestus Chogga (Iringa Kusini).
(6) Eli Anangisye (Rungwe Kaskazini)
(7) Gervas Kaneno (Karagwe)
(8) Jeremiah Bakampeja (Ihangiro, Bukoba).
Kuna baadhi ya wabunge wa zamani (wengine washatangulia mbele ya haki) ambao kusikia au kutamka majina yao kulileta burudani ya aina yake miaka hiyo. Majina machache niliyoweza kukumbuka ni:

Kuwayawaya S. Kuwayawaya
Tuntemeke Sanga
Njelu Kasaka
Stephen Salum Nandonde
Semindu Pawa
Lepilal ole Moloimet
Benito Malangalila
Frederick Nteminyanda Fumbuka
Felix Tadeo Mwanambilimbi
Said Ngwanangwalu
Chrisant Majiyatanga Mzindakaya
Omar Kwaangw
 
Naomba mtu anijibu WILLIAM MWAGAMALINGO MPILUKA alikuwa mbunge wa wapi?! wa kwanza kutoa jibu sahihi namrushia vocha ya 5000

Mbunge wa Mufundi na kwa sasa ingekuwa Mufundi Kusini akichuana ktk jimbo hilo kila uchaguzi na Mzee Mungai!

Alikuwa jirani yetu Dar na tafadhali naomba vocha yangu
 
Mbunge wa Mufundi na kwa sasa ingekuwa Mufundi Kusini akichuana ktk jimbo hilo kila uchaguzi na Mzee Mungai!

Alikuwa jirani yetu Dar na tafadhali naomba vocha yangu
Ha ha mzee umepata, vocha yako nitakupa kuwa mvumilivu tumalizie kwanza SGR na Stiglers Gorge...ha ha
 
Leons Ngalai wa Rombo , alienda na bia chafu mbungeni ili kumuwajibisha waziri wa viwanda wakati huo
Mheshimiwa Leons Ngalai Silayo vs Basil Pesambili Mramba enzi zao miaka ya 70 mwishoni na mwanzoni mwa miaka ya themanini Rombo palikuwa hapatoshi, Mramba akiwa mwanasiasa mashuhuri anayeibukia na Ngalai akiwa mwanasiasa mkongwe jimbo la Rombo
 
Miaka inaenda jamani Twaha Ulimwengu, Mohamed Seif Hatibu na Anna Makinda walikuwa wabunge kundi la vijana! Duuh eti saa hivi vijana wa ccm ni kina Makonda, Happi, Slow slow, Mnyeti.......!
Polepole anapaswa kuwa kundi moja na wale wazee washauri wa Chaka kuna Mkapa,Malecela sio vijana. Hana ukijana wowote hata jumuiya ya wazazi kapitiliza we muangalie vizur sura yake
 
Kuwayawaya Stephene Kuwayawaya, Sebastian Kinyondo, Severine Supa, Sara Mwenge,
 
Back
Top Bottom