Tujikumbushe Majina ya wabunge wa zamani


Misigalo TABORA ndiye aliyeanzisha kutoa shilingi kwenye baudget
Bakampenja ni kati ya wabubge wa bukoba kukataa kuhamia kwenye vijiji vya ujamaa
Zimbihile alikuwa anaongea zaidi ya lugha kumi mojawapo ni kijerumani
Ndimara Tegambwage mwandishi wa habari ambaye ashikiki kwa uhodari wake wa kuandika
 

Austin Shaba- Mtwara Mjini
Edgar Maokola Majogo
 


Kwa kuongezea pia kulikuwa na:

Ibrahim Kaduma - (Taifa)
Balozi Nicholas Kuhanga - (Taifa)
Agustine Mwingira
Seif Bakari
Bhoke Munanka
Peter Kisumo
Wilbert Chagula
Frederick Nteminyanda Fumbuka - (Shinyanga Mjini)
Mujengi Mange Gwao - (Singida Vijijini)
Anna Kabati -(Kuteuliwa)
Filbert Bashiganye Kapunda - (Magu)
Ali Mwinyigogo
Balozi Mustafa Nyang'a nyi -(Kondoa)
Major General(rtd) Mrisho Sarakikya - (Meru)
Simenti Constantine Shillingi - (Maswa)
David Bakanyoma Simeo Zimbihile -(Muleba)
 
Ilikuwa ni G55 na sio G48. waliongozwana Njelu Kasaka wakati huo Mhe. Sitta alikuwa ni waziri wa Sheria akipambana moja kwa moja na G55 na alisaidiwa na Mhe. Damian Lubuva aliyekuwa AG

Mawazo huru ya kwanza kuirudisha Tanganyika yetu yalianzishwa na G55!Wabunge mahiri kama vile Jared Ghachocha;Francis Mwaduma;Kuwayawaya S Kuwayawaya na Lumuli Kasyupa walitishwa na Mwl Nyerere kuwa wasipo ondoa hoja ya Utanganyika mezani tusije kulaumiana baadae!

Huwa namtembelea mara kwa mara Mzee Lumuli Kasyupa kijijini kwake Ndandalo!Mzee huyu aliyewahi kuwa Naibu waziri wa Kilimo kwenye utawala wa Nyerere ana mengi sana ya kutufunza
 

Ukiondoa hao waliosema Muungano una matatizo bila kung'ata maneno, naambiwa kuna wabunge fulani walisema kusini ijitenge, sina uhakika sana. Ila yafaa tuseme hapa kuwa kupishana fikra bungeni kulikuwepo tangu enzi za mfumo wa chama kimoja.
 
Enzi hizo mawaziri hawakuwa na majibu ya kipuuzi kama wa sasa eti serikali inatarajia,,,,,kulikuwepo na dead line.....vinginevyo shilingi moja ilikuwa inachomolewa kwenye bajeti na kuirudisha ilikuwa shughuli......bunge la zamani lilikuwa na utamu wake
 
Mujuni Kataraiya,huyu alikua mbunge wa bukoba mjini,baadae mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza.sasa hivi ni hohehahe,analelewa na ndugu zake,huwezi kuamini kama ni yeye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…