Tujikumbushe Makamanda wa Polisi waliovuma enzi hizooo...

Tujikumbushe Makamanda wa Polisi waliovuma enzi hizooo...

Hao wote walikuwa wezi maana uwazi na utawala bora haukuwepo,
 
kumbukumbu nzuri mkuu,tusiwakumbuke wakubwa tu,na hapa magomeni makuti yule askari maarufu alikuwa naitwa nani vile?
Huyo simkumbuki mkuu!maeneo ya kino kuna bonge mmoja linaitwa KABILA na mwenzake MAKOMEO hawa bado wanasumbua ila hawana bei wakikutia mikononi sometimes hata sound wanaweza kukuachia...
 
Hivi Tibasana nae alikuwa kitengo hapo makao makuu
 
kuna makamanda wa polisi wa mikoa waliovuma sana enzi zao za utumishi Jeshini kwa kupambana na uhalifu. Mmoja wapo ni, Venance Tossi.
Tukumbushe wengne unaowajua.

So,Tossi ni wa enzi hizoooo....
 
simjui hata mmoja kwasababu sio mtu wa karibu nao sana
 
Tiba jembe!ila kuna viaskari vidogo vilitisha sana uswahilini!!!MKAMASHAPU,TEKELO na JITI LA MUHOGO!pande za DSM,pale ujiji m'nyamala kulikuwa na DAVE!sasa hivi kuna pimbi mmoja Kinondoni wa kuitwa SWAI!

Muuza Sura,

Umenikumbusha mbali sana kwa huyo Mkama Sharp alikuwa anatupa raha sana uwanja wa Taifa.....Kwa tulioishi Dar ya Zamani tunamkumbuka sana....Pia Mwanzoni mwa miaka ya Tisini kulikuwa na yule Trafik Mayenu sijui alishastaafu yule...?Pia kulikuwa hadi na vichaa waleta burudani kama Kejeli na Mapisto.
 
Tiba jembe!ila kuna viaskari vidogo vilitisha sana uswahilini!!!MKAMASHAPU,TEKELO na JITI LA MUHOGO!pande za DSM,pale ujiji m'nyamala kulikuwa na DAVE!sasa hivi kuna pimbi mmoja Kinondoni wa kuitwa SWAI!
MkamaShapu huyu wa JF ama?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom