Tujikumbushe maneno mazito ya Godbless Lema alimwambia Rais Samia, Nilinusurika kuuawa zaidi mara 3

Tujikumbushe maneno mazito ya Godbless Lema alimwambia Rais Samia, Nilinusurika kuuawa zaidi mara 3

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mwanasiasa wa muda mrefu katika siasa za Tanzania kutoka ndani ya CHADEMA Godbless Lema aliwahi kuzungumza mambo mazito sana kuhusu uongozi wa Rais Samia huku akimsii sana kwenye kauli zake na namna ya kuliongozo taifa zima la Tanzania

Mh Rais wetu nimekusikiliza zaidi ya mara 20, Mh Rais wewe ni Amri Jeshi Mkuu wa Nchi mood yako kwenye puplic kauli yako kwenye puplic na kwa viongozi wa ulinzi na usalama inamaana kubwa sana juu ya maisha ya watu na maisha ya wanasiasa.

Mh Rais nimekusikia ukiwa unasema ya kwamba kuna wengine uliwaruhusu wakarejea nchini walikuwa wameshakimbia nchi lakini unaona wameota mkia na hao watu uliwaruhusu kurudi nchini mimi miongoni mwao.

Mh Rais nilifikiri jambo la msingi kwako watu walikimbia nchi walipata kujiamini kurudi nyumbani. Mh Rais wakati nakimbia nchi nimekoswa kuuwawa zaidi ya mara 3 nishawahi kutekwa bahati nzuri Mungu mkubwa watekaji hawakufanikiwa kuniua

 
Back
Top Bottom