Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Lugha yoyote hunakshiwa kwa maneno ya kudumu na yale ya muda mfupi. Lugha ya Kiswahili imekuwa na bahati ya kupata maneno mengi ya misimu na baada ya muda hutokomea kusiko julikana.
Kupitia uzi huu tukumbushane maneno mbalimbali ambayo yanapotea kwa kasi hivi sasa.
Kupitia uzi huu tukumbushane maneno mbalimbali ambayo yanapotea kwa kasi hivi sasa.
- Kula jiwe- kukaa kimya
- Kujikata kisilesi- kuondoka
- Kishtobe- mlimbwende myange
- Lofa- masikini
- Lodi- tajiri
- Wakuja- mshamba
- Njenge- nyumba
- Njelii- Mwanjelwa
- Mkoko- gari
- Kala kidato- msomi