Naikumbuka game ya Romania vs Colombia
Walikutana mafundi wawili
Romania alikuwepo Haghi Colombia alikuwepo Valderama
Mafundi hatari haooo
Mkuu yule mtu alikua ni shujaa asiyeimbwa, jamaa ana mi control kama yoteNamkumbuka fundi wa mpira dutch master, a non flying dutchman! Lile goli lake anawafunga argentina! Kwangu mimi ni moja kati ya magoli bora ya michuano ya kombe la dunia. Bonge moja la goli, control murua halafu finishing ya kibabe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nedved...Kabla ya michuano kuanza kitaa Mimi na wanangu tulikuwa tuna madaftari yamejaa picha za wachezaji Wa nchi mbalimbali. Na ilikuwa ukipata picha Kali unalingishia kichizi kwa wenzako. Mfano nlikuwaga na mipicha ya kutisha ya kina Davor suker,George Haggi, Gabriel Batistuta, Ariel Otega, Diego Simione, Michael Owen, Jay jay Okocha, Rashid Yekin,Daniel Amokachi, Alessandro Del Piero, Giafranco Zola,Carel Pobosky, Pavel Nedvid,David Beckham, Jugen Klinsman, nk
jamaa alikua mbaya sana wa header asee.Kile kichwa cha KLUIVERT jamani nusu fainali against BRAZIL......ilikuwa balaa
Commentator alisema "three touches, control, turn, finish"Namkumbuka fundi wa mpira dutch master, a non flying dutchman! Lile goli lake anawafunga argentina! Kwangu mimi ni moja kati ya magoli bora ya michuano ya kombe la dunia. Bonge moja la goli, control murua halafu finishing ya kibabe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Na mimi nilitaka kuzungumzia hili hili goli jamaa alipiga mpira toka katikati na kitu kikaitika da ilikua balaaa siku ile sitakuja kusahauMahaba tu. Hilo shoot alilopiga Carlos halifikii lile alilopiga Sunday Oliseh dhidi ya Spain. Japo mazingira ni tofauti.
Sunday Oliseh alitandika mpira uliokuwa rebound sisi tunaita lose ball, karibu mita 35. Mkwaju wa maana. Mkwaju uliowapa Nigeria ushindi wa 3-2.
Mwenye uwezo wa kuattach anaweza kuweka hapa tukalinganisha.
Sent using Jamii Forums mobile app
Alafu utakuta kuna wahuni wanakua wanaliwinda sana daftari wakuibie picha zakoKabla ya michuano kuanza kitaa Mimi na wanangu tulikuwa tuna madaftari yamejaa picha za wachezaji Wa nchi mbalimbali. Na ilikuwa ukipata picha Kali unalingishia kichizi kwa wenzako. Mfano nlikuwaga na mipicha ya kutisha ya kina Davor suker,George Haggi, Gabriel Batistuta, Ariel Otega, Diego Simione, Michael Owen, Jay jay Okocha, Rashid Yekin,Daniel Amokachi, Alessandro Del Piero, Giafranco Zola,Carel Pobosky, Pavel Nedvid,David Beckham, Jugen Klinsman, nk
KLUIVERT alikua ana mbinu yake mpira wa kona ukipigwa yeye haruki wakati wenzake wanaruka ile wakitua chini yeye ndio ananyanyuka anakutana na mpira kitu nyavuni yule jamaa alikua mbaya sana kila kona ikipigwa anapata goli ha ha ha ha ha haKile kichwa cha KLUIVERT jamani nusu fainali against BRAZIL......ilikuwa balaa
Yaani balaa,au wabandue baadhi ya picha ili wwkabandike kwaoAlafu utakuta kuna wahuni wanakua wanaliwinda sana daftari wakuibie picha zako
Commentator alisema "three touches, control, turn, finish"
Moja ya tukio la kukumbukwa kabla ya mechi za Ufaransa kuanza ni pale beki Laurent Blanc kubusu upara wa Fabian BarthezView attachment 1304557
Mkuu yule mtu alikua ni shujaa asiyeimbwa, jamaa ana mi control kama yote
Mtoe credit mnapokopi kazi za watu ..... Yaani umeichukua kama ilivyo kwa @zakazakazi instaSHUTI LILIKOKIUKA KANUNI ZA MWENDO ZA KISAYANSI
Kuelekea Kombe la Dunia la 1998, wenyeji Ufaransa waliandaa mashindano maalumu ya kupima maandalizi yao.
Wakati huo Kombe la Mabara lilikuwa halijaanza kutumika kupima maandalizi ya Kombe la Dunia. Lilikuja kuanza 2001.
Mashindano hayo yaliyoitwa Tournoi de France yalifanyika 1997 na kushirikisha timu 4; wenyeji Ufaransa, Brazil, England na Italia.
Mechi zilichezwa kwa mtindo wa ligi, kwamba mwenye pointi nyingi ndiyo bingwa. England wakawa Mabingwa.
Mechi ya ufunguzi ilifanyika Juni 3, 1997 dimbani Stade de Gerland mjini Lyon, na kuwakutanisha wenyeji na Brazil.
Ni kupitia mchezo huu uliomalizika kwa sare ya 1-1, ndipo Roberto Carlos alifunga bao la mkwaju wa adhabu ndogo, linalosemekana kukiuka kanuni za mwendo za kisayansi na hadi sasa wanasayansi duniani bado wanaendelea na utafiti kujua mpira uliwezaje kwenda kama ulivyoenda.
Wanasayansi wanne wa Ufaransa; Guillaume Dupeux, Anne Le Goff, David Quere na Christophe Clanet wa taasisi ya utafiti wa kisayansi ya Ecole Polytechnique, walifanya utafiti ambao matokeo yake yalichapishwa kwenye jarida la New Journal of Physics la Septemba 2010.
Wanasayansi hawa walifanya uchambuzi wa majaribio kadhaa ya kimaabara yaliyozaa mlinganyo unaofafanua mwendo wa mpira na nguvu zilizokuwemo ndani yake katika muda wa kitendo.
Wakahitimisha kwa kusema endapo hesabu zitapigwa vizuri, katika umbali ule ule na nguvu ile ile ya shuti, mtu yeyote anaweza kurudia na mpira ukaenda vile vile.
Lakini mwanasayansi wa Brazil, Prof. Luis Fernando Fontanari anasema hiyo haiwezekani. "Hali ya wakati wa tukio kama nguvu ya upigaji, kishindo cha makutano ya mguu wa Roberto Carlos na mpira, na umbali hadi golini, vilikuwa vya nadra sana kiasi kwamba tunaweza kuita miujiza", anasema Profesa huyo wa chuo kikuu cha Sao Paulo -- kinachoheshimiwa zaidi Brazil.
Fontanari ni mmoja wa wahariri wa majarida ya "Physics of Life Reviews" na "Theory in Biosciences," ambayo ni miongoni mwa majarida muhimu zaidi ya kisayansi duniani.
Mwanasayansi mwingine kutoka Israel, Erez Garty, alifanya utafiti wake na kuhitimisha kwa kusema alichofanya Roberto Carlos ni mazingaombwe. Kazi yake iko YouTube.
Sent using Jamii Forums mobile app
Shuti la Oliseh lilikuwa limenyooka ...tofauti na hili acha upan africanismMahaba tu. Hilo shoot alilopiga Carlos halifikii lile alilopiga Sunday Oliseh dhidi ya Spain. Japo mazingira ni tofauti.
Sunday Oliseh alitandika mpira uliokuwa rebound sisi tunaita lose ball, karibu mita 35. Mkwaju wa maana. Mkwaju uliowapa Nigeria ushindi wa 3-2.
Mwenye uwezo wa kuattach anaweza kuweka hapa tukalinganisha.
Sent using Jamii Forums mobile app