Raphael Mtui
Member
- Nov 26, 2024
- 78
- 204
Ilikuwa majira ya saa saba usiku na dakika 37, tarehe 31 July 2024, ndani ya jiji la Tehran nchini Iran. Mlipuko mkubwa ulisikika sehemu ambayo daima dumu usingetarajia. Mlipuko ule ukaondoka na maisha ya Ismail Haniyeh, aliyekuwa kiongozi mkuu wa Hamas.
Mgogoro wa Mashariki ya Kati umekuwa ukiingia kwenye sura mpya karibu kila uchwao.
Suala la kushangaza kwenye mauaji ya Ismail Haniyeh sio mauaji yake! La hasha! Suala la kipekee na la kushangaza ni MAHALI ALIPOKUWA WAKATI ANAUAWA!
Israeli iliendelea kuthibitishia maadui zake kwamba wanaweza kuuawa popote walipo, na hawana usalama haijalishi wako wapi.
Israeli inawafanya watu wasishtuke tena inapoua maadui zake, bali watu washtuke kwenye mbinu na weledi unatumika katika 'kudondosha' maadui zake bila hata kujali ni watu 'high profile' kiasi gani.
Twajua vyema kwamba Ismail Haniyeh ndiye alikuwa 'rais' wa Hamas. Hamas unayoijua wewe, ile unayoisikia kila wakati kwenye vyombo vya habari, kelele zote za dunia unazosikia kila uchwao kuhusu Hamas, huyu Ismail Haniyeh ndiye alikuwa kiongozi mkuu wa kundi hilo la Hamas mpaka siku ile alipouawa.
Lakini bado nasema, licha ya kishindo cha kifo cha mtu mzito namna hii, lakini mshtuko mkubwa zaidi upo kwenye swali la; ALIUAWA AKIWA WAPI!
Habari kubwa sana ndio hiyo, ILIWEZEKANAJE AUAWE AKIWA MAHALI ALIPOKUWA.
Sasa tuanze hivi:
Kwa wale ambao hawamjui Ismail Haniyeh, acha tumweleze japo kwa ufupi kabisa.
Ismail Haniyeh kwa kuanzia kabisa aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Wapalestina mwaka 2006 hadi 2007 wakati chama cha Hamas kiliposhinda uchaguzi.
Kumbuka, Waziri Mkuu wa Wapalestina ndiye Mkuu wa 'nchi' ya Wapalestina. Hakuna kiongozi mwenye madaraka mazito kuliko Waziri Mkuu, huyo ndiye 'rais' wao.
Najua unajiuliza kwa nini awe Waziri Mkuu kwa mwaka mmoja tu? Jibu ni rahisi tu. Wote tunajua jinsi ambavyo Wapalestina wa Gaza na wale wa West Bank wanavyochukiana.
Chama cha Fatah cha West Bank na chama cha Hamas cha Gaza kamwe havijawahi kuweza kuvumiliana katika kuijenga Palestina yao.
Na hata hivyo, misimamo mikali kupitiliza ya watu wa Gaza haiwezi kuendana kabisa na ule 'upole' wa Wapalestina wa West Bank. Maisha yenye maana kwa Hamas ni kuona wakirusha makombora kuelekea Israeli, wakati Wapalestina wa West Bank wako tofauti kidogo. Kitendo cha kiongozi wa serikali kutokea ukanda wa Gaza, kinazua swali kwamba hawa watu watafika mbali?
Ndio maana ndani ya mwaka mmoja tu serikali ilivunjika na huo ndio ukawa mwisho wa Ismail Haniyeh kuwa Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Wapalestina.
Uwaziri Mkuu ulipoisha, moja kwa moja au niseme 'automatically' akawa kiongozi mkuu wa Wapalestina wa Gaza.
Tangu wakati huo, Hamas ilijitengenezea serikali yao na kuifanya Gaza kuwa kama nchi huru inayojitawala yenyewe, huku Ismail Haniyeh akiwa kama 'rais' wa Gaza hadi alipouawa.
Sasa, unaweza kuona tunazungumzia mtu mzito kiasi gani.
Jambo lingine muhimu kuhusu Ismail Haniyeh ambalo unapaswa kulikumbuka, yeye alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa hii Hamas tunayoiongelea.
Kundi la Hamas lilizaliwa mwaka 1988. Wakati huo Ismail alikuwa 'kijana barubaru', lakini alionesha juhudi nyingi za 'kufia chama' hadi akakamatwa na Israel na kuwekwa ndani kwa miezi sita.
Mwaka uliofuata 1989 alikamatwa tena na Israeli akashikiliwa hadi mwaka 1992 Israeli ilipoenda 'kumtupa' huko Lebanoni akiwa na wafungwa wenzake kama mia nne hivi.
Hatimaye alirudi Gaza mwaka 1993 kutokea Lebanoni. Tukumbuke jambo muhimu: Ismail alikuwa ametengeneza mahusiano ya karibu na kiongozi mkuu wa kiroho wa Hamas tangu miaka ile Hamas ilipozaliwa.
Kiongozi huyo aliitwa Sheikh Ahmed Yassin. Huyu ndiye aliyekuwa Imamu wa Hamas ambaye kimsingi ndiye aliyeiunda Hamas mwaka 1988 ilipozaliwa.
Kutokana na 'upako' alioupata Ismail kutoka kwa kiongozi wake huyo, alichaguliwa kuwa 'shemasi' wa chuo kikuu cha Uislamu cha pale Gaza mara tu aliporejea kutoka Lebanoni.
Umaarufu wa Ismail uliimarika sana mwaka 1997 wakati Sheikh Ahmed Yassin alipomteua Ismail kuwa sekretari wake binafsi. Hakika hapa alipata heshima kubwa ndani ya Hamas.
Fikiri kuwa msaidizi na msiri binafsi wa imamu na mwanzilishi wa Hamas!
Ismail aliendelea kuwa msaidizi wa Sheikh Yassin hadi mwaka 2004 wakati Israeli ilipomwua Sheikh Yassin.
Hapa nieleze kidogo alivyouawa:
Mwaka 2003 Israeli ilifanya majaribio mawili ya kuwaua Sheikh Yassin na Ismail Haniyeh, lakini majaribio hayo yalishindikana.
Hata hivyo, alfajiri ya 22 March 2004, wakati Imamu Yassin akiwa ametoka msikitini kwa swala ya Fajr, akiwa anatembea kurudi nyumbani kwa kutumia 'wheelchair' yake kutokana na kuwa na ugonjwa wa muda mrefu tangu akiwa kijana, kuna jambo likatokea ghafla:
Helikopta za jeshi la Israeli zilikuwa zinamfuatilia, na akashushiwa mabomu, akafa pale pale pamoja wote waliokuwa naye, pamoja na wapita njia wengine tisa.
Bahati iliyoje, Ismail hakuwa na 'boss' wake siku hiyo. Hamas wakaiambia dunia kwamba, Israeli wamefungua malango ya kuzimu!
Tangu hivi vita vinavyoendelea vilivyoanza mwezi wa kumi mwa 2023, Ismail Haniyeh ndiye amekuwa akionekana kwenye vyombo vya habari mara nyingi kuiambia dunia 'nyongo' za Wapalestina dhidi ya Israeli.
Tukumbuke pia, Ismail Haniyeh alikuwa akiishi nje ya Gaza. Hakuwa akiishi pale Gaza. Makazi yake yalikuwa nchini Uturuki na lakini hasa Qatar.
Sasa basi twende kwenye mada yetu kuhusu kifo cha Ismail Haniyeh.
Ilikuwa majira ya saa saba usiku na dakika 37, tarehe 31 July 2024, ndani ya jiji la Tehran nchini Iran. Mlipuko mkubwa ulisikika sehemu ambayo daima dumu usingetarajia. Mlipuko ule ukaondoka na maisha ya Ismail Haniyeh.
Ngoja nikurudishe mchana wa tarehe 30 July kabla ya mlipuko huo.
Kuna picha nimekuwekea hapo chini ikionesha Ismail Haniyeh akiwa na rais mpya wa Iran. Tukumbuke, Iran ilikuwa imepata rais mpya, baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo kufariki kwa ajali ya helikopta, ambayo kisababishi chake hakika siku ukijua ukweli halisi utashtuka kabisa.
Baada ya rais huyo kufariki, (utakumbuka alikuwa anaitwa Ibrahim Rais au kwa kirefu Ibrahimu Raisolsadati).
Rais huyu alifariki siku ya tarehe 19 May mwaka 2024).
Sasa basi, baada ya kifo cha Ibrahim uchaguzi ukafanyika, Iran ikapata rais mpya, daktari wa upasuaji wa moyo, ndugu Masoud Pezeshkian.
Ikafika wakati wa kuapishwa kwa rais Masoud.
Tukumbuke tena kwamba, haya makundi ya Hamas na Hezbollah ni 'watoto pendwa' wa Iran. Mafungamano yaliyopo katika Iran na haya makundi mawili ni makubwa mno.
Kama ambavyo tumesisitiza katika makala zetu mbalimbali, Irani ndiye mfadhili mkuu wa haya makundi, wakipewa 'michongo' ya silaha, mabilioni ya fedha, mafunzo ya kijeshi pamoja misaada mingine mingi.
Sasa, kwa kuwa Iran ilikuwa imepata rais mpya, ilikuwa ni lazima mtu kama Ismail Haniyeh ahudhurie tukio la 'baba yake' kuapishwa. Ndio hapa sasa tunamkuta Ismail Haniyeh akiwa nchini Iran ingawa alikuwa akienda huko mara kwa mara.
Kabla ya sikukuu ya uapisho, Ismail Haniyeh akakutana na rais Masoud pale Ikulu, kwa mazungumzo ambayo kwa vyovyote vile watu wazito namna hii wanapokutana, huwa wanakuwa na muda wa kuzungumza mambo mazito.
Katika mazungumzo hayo, ndio ikapigwa hiyo picha niliyokuwekea hapo chini.
Tukumbuke kwamba kipindi hiki Ismail Haniyeh alikuwa kwa namna fulani 'amenyanyua mikono' kutaka vita kati ya Israel na Hamas isitishwe.
Nchi za Qatar na Misri zimekuwa zikitaka vita visimame kutokana na hali kuwa mbaya mno pale Gaza.
Haniyeh alikuwa mstari wa mbele kutaka kufanyike mazungumzo ya kusitisha vita.
Kuonesha kwamba alikuwa serious, hebu ona:
Mwezi wa nne mwaka 2024 polisi wa Israeli walimkamata dada yake Ismail Haniyeh kwa kosa la kuwasiliana na wanaharakati wa Hamas.
Siku tisa baadaye, Israeli ikatajeti watoto watatu wa Ismail Haniyeh, pamoja na wajukuu zake wanne, ambapo majeshi ya Israeli yaliwaua kwa kuwaangushia mabomu.
Wakafa wote!
Katika hali isiyotegemewa, badala ya Ismail 'kupandisha sumu', yeye akaendelea kutaka suluhu na kuitangazia dunia wazi wazi kwamba anataka vita viishe.
Lakini bado Israeli haikumsamehe licha ya nia yake wala haikuzingatia adhabu ya kuua watoto watatu na wajukuu wanne kwa mpigo.
Mossad bado waliendelea kumfuatilia kila hatua aliyopiga.
Mpaka siku ya leo, tarehe 30 July 2024 akiwa ndani ya Ikulu ya Iran, ana kwa ana na rais mteule, bwana Masoud.
Ambacho hawakujua hawa watu wawili, kikao chao kilikuwa ni mwisho wa kuonana kwao.
Wajua jengo la ikulu ya Iran limepakana na jengo maridhawa sana la ghrofa tano. Jengo hili huitwa Sadabad Complex. Ismail Haniyeh alipowasili jijini Tehran hakutafuta hoteli huko mjini au 'safe house' fulani ili aishi hapo siku hizo atakazokuwa hapo Tehran.
Kwa uzito na urafiki kati ya Iran na Hamas, Ismail alipewa chumba ndani ya jengo hili ambalo lipo ndani ya 'campus' ya ikulu ya Iran.
Jengo hili ni hoteli ama guest ambazo huwa zinamilikiwa na kuendeshwa na jeshi la IRGC. Nikitaja hilo jina moja kwa moja unajua nimetaja kitu gani!
IRGC ni Islamic Revolutionary Guards Corps. Hili sio jeshi rasmi la Iran, lakini ajabu ndio limekuwa na nguvu na ushawishi kuliko jeshi rasmi, sio tu ndani ya Iran bali karibu eneo lote la Mashariki ya Kati. Ndio linaloendesha serikali ya Iran.
Hii ina maana, Ismail alikuwa mahali ambapo analindwa na ule ulinzi ambao ni 'top security' wa Iran kupitia makamanda wa IRGC.
Lakini sasa, usiku wa saa saba na dakika 37, mlipuko ukasikika pale kwenye jengo alilokuwa Ismail Haniyeh. Madaktari wa ikulu kukimbilia pale, wakakuta Ismail amefariki pamoja na bodyguard wake Wasim Abu Shaaban.
Maswali ni mengi kuhusu chanzo cha mlipuko huo. Kila linapoulizwa swali la mlipuko huo ulitokana na nini, kumekuwa na majibu mengi yasiyokuwa na uhakika. Lakini kwa vyovyote ni kwamba Israeli ilikuwa ya imefanikiwa kutekeleza operation katika eneo ambalo isingewezekana abadani.
Maswali ni mawili: Israeli wamefanikiwaje kufanya shambulizi hilo mahali hapo?
Swali la pili: kwa nini Israeli hawakumwua Ismail Haniyeh akiwa nchini Qatar ambako aliishi kwa muda mrefu na tena hakuishi kwa uficho? Kwa nini waache kutekeleza operation kama hiyo huko Qatar ambako anaishi na kuzunguka hadharani, lakini wakatekeleze mauaji 'almost' ndani ya kuta za ikulu tena ya Iran? Si ni kitu hatari sana hicho?
Sasa, tuanze na swali la pili:
Kwa nini Israeli haikuwahi kumfanya kitu Ismail Haniyeh akiwa Qatar?
Ni kweli, Israeli wangeamua kumwua Ismail Haniyeh akiwa Qatar ingekuwa jambo rahisi sana. Mossad wangekaa kikao asubuhi saa mbili, kisha baadaye saa tano wangekuwa 'wameshakula roho yake.'
Na kama tujuavyo, Israeli imefanya mauaji ya maadui zake wakiwa nchi mbalimbali duniani.
Lakini kuna shida moja kubwa sana inawakabili Israeli: Iko hivi, NI RAHISI KUMWULIA ADUI YAKO AKIWA NDANI YA NCHI AMBAYO HAMNA MAHUSIANO MAZURI YA KIDIPLOMASIA, KULIKO KUFANYA MAUAJI AU KUTEKELEZA OPERATION ZA NAMNA HIYO KWA NCHI RAFIKI.
Umeelewa?
Yaani, jaribu kufikiri: fikiri tu kirahisi, Ismail yupo jijini Uingereza alafu unaenda kulipua hoteli aliyopo na kumwua. Ndio utamwua, lakini Uingereza itakuelewaje? Upo tayari kupoteza mahusiano yako na nchi hiyo?
Mwanzoni Israeli ilikuwa ikitekeleza operations za mauaji ya maadui zake bila kujali wako nchi gani. Wakawa wanajikuta wanakosana na nchi marafiki zake. Kuna operations ambazo Israeli imefanya zikaishia kuwaletea aibu na fedheha kubwa.
Lakini pia usisahau, operations za namna hii sio zote huenda sawa. Kuna wakati 'hit team' wanaweza kuua mtu mwingine kimakosa au kuua mhusika lakini wakalazimika kuua na watu wengine zaidi ya yule mhusika anayetafutwa.
Fikiri huo mfano niliotoa hapo juu wa jinsi Imamu Ahmed Yassin alivyouawa. Ni yeye peke yake alikuwa mlengwa, lakini walikufa watu zaidi ya kumi na wengine kuishia kujeruhiwa vibaya na hata kupata vilema vya maisha.
Sasa, ukifanya operation ya namna hii kwa nchi rafiki, ukaua watu, ukaharibu miundombinu, ukatumia passports zao feki, uwe tayari kwa matokeo yenye athari kubwa kuliko hiyo ya kumwua adui yako.
Na kumbuka, si lazima hata usababishe madhara kama hayo. Unaweza usisababishe madhara yoyote. Lakini kile kitendo tu cha kufanya operation ndani ya nchi yao, hilo ni kosa baya kabisa la kutosha hata kutangaza vita.
Kipindi kama hiki, Israeli inahitaji nchi marafiki kuliko muda wowote ule katika historia yake. Wanahitaji kulinda mahusiano yao, tena wanahakikisha yanaimarika kuliko hapa yalipo. Haitaki kufanya chochote cha kuhatarisha mahusiano ya kidiplomasia.
Israel inahitaji hata kuungwa mkono na nchi za Kiarabu.
Nchi ya Qatar kwa mfano: kwanza ni rafiki mkubwa wa Marekani ambaye ni 'baba mpendwa' wa Israeli. Marekani ana kambi ya kijeshi pale Qatar. Sio kambi unayoijua wewe, ni kambi kubwa kuliko kambi zote za kijeshi eneo lote la Mashariki ya Kati. Inaitwa AI Udeid Air Base.
Mwaka 1999, aliyekuwa Emiri wa Qatar Sheikh Hamad alisema angependa kuona maafisa hata elfu kumi wakifanya kazi katika kambi hiyo.
Hakika urafiki wa Qatar na Marekani ni wa kushibana!
Israeli naye anahitaji sana urafiki kati yake na Qatar. Israeli imekuwa ikijitahidi sana kuwa na mahusiano mazuri na Qatar kwa manufaa yake na ili pia kulinda uhusiano wake na Marekani, kwa maana kwamba Israeli ikigombana na Qatar maana yake inagombana na Marekani.
Kumbuka pia, Qatar ni nchi ya Kiarabu, na ndio kabisa Israeli inatamani angalao kuwe na nchi za Kiarabu ambazo zinaitetea na kuponda Waarabu wenzake.
Kwenye nchi kama hii ya Qatar, huwezi kuamka asubuhi ukatuma majasusi kwenda kutekeleza operation ya kuua mtu. Au huwezi kutuma 'drone' ukaenda kudondosha mabomu mitaa ya jiji la Doha kisa unataka kuua mtu fulani. Ndio maana Ismail Haniyeh akiwa Qatar alikuwa anaishi kwa kujidai na kujiachia anavyotaka.
Anajua Mossad wanamwona kabisa, lakini anajua hawawezi kumfanya lolote zaidi ya kumng'atia kidole!
Ambacho Israel anafanya ni kumvizia adui asafiri, aende kwenye nchi adui, kisha itumie weledi walionao kupenyeza 'hit team' kwenda 'kumzimisha' huyo wanayetaka asiishi.
Mpaka hapo naamini umeelewa. Kuulia adui kwenye nchi-maadui ni rahisi kwa sababu hujali chochote. Hujali mahusiano ya kidiplomasia.
Sasa basi, twende swali la pili:
Israeli ilifanikiwaje kumwulia Ismail Haniyeh akiwa eneo la ikulu ya Iran?
Tuseme hivi: siku ile ile Israeli ilipopata uhuru, (14 May 1948) Israeli ilitangaza kuanza rasmi kutafuta maadui wake popote pale walipo ulimwenguni.
Israeli haijawahi kupumzika bila kuwa na watu mbalimbali wanaotafutwa dunia nzima 'wamalizwe!' Israeli imetekeleza operations nyingi sana maeneo mbalimbali, na ninataka kuamini kwamba uwewahi kusoma angalao tano tu kama wewe sio mpenzi wa kusoma.
Kila uchwao, Israeli inafanya operations nyingi, nyingine huchukua miaka mingi mno kukamilika, lakini lazima ikamilike. Israeli haijawahi kuamini kwamba wanashindwa kumpata adui yao na kumwondosha duniani.
Israeli walijiwekea malengo kwamba, lazima wahakikishe wanamfanya kila adui wa Israeli ajisikie hofu ya kuuawa muda wowote mahali popote alipo, na ajisikie hana mahali pa kujichimbia bila kukamatwa na kuuawa na 'manjagu' wa Mossad.
Hata operation ya kumwua Ismail Haniyeh akiwa kwenye ikulu ya Iran walitaka kuwaambia maadui zake ujumbe ule ule kwamba hawana uwezo wa kuukwepa mkono wa Mossad, na kwamba watapatikana na kuuawa haijalishi wako wapi.
Dakika zile zile Ismail alipouawa, dunia ilifahamu kwamba ni Israeli wametekeleza mauaji hayo, ingawa Israeli 'walijikausha' pale mwanzoni.
Sasa waliwezaje, haijajulikana hasa, ila habari zinasema mara tu baada ya kifo cha rais Ibrahim Rais, Mossad walijua hakika Ismail Haniyeh atasafiri kwenda Tehran kuhudhuria uapisho wa huyo atakayechaguliwa kushika nafasi yake. Inasemekana mipango ilianza ya kumtegeshea bomu chini ya kitanda atakacholala siku akija.
Hata tusipokuwa na uhakika huo, uhakika tulionao ni kwamba Israeli waliweka bomu kwenye kitanda atakacholala Ismail. Hata tusipojua ilikuwa lini na kivipi, lakini tujue waliweza.
Walimtuma nani aweke, hapo ndio tunakuja tena kwenye ile stori ya mapandikizi. Kwa vyovyote vile, Mossad walikuwa wana mtu mzito kwenye system ya IRGC wa pale ikulu.
Tukumbuke maafisa wa IRGC walisema kwamba kulikuwa na mabomu matatu yaliyokuwa yametegwa kwenye vyumba vitatu vya guest ile na wakasema yalitegwa na afisa anayeitumikia Mossad akiwa ndani ya IRGC!
Usishangae, ndio mambo ya ujasusi yalivyo. Mnaweza kuwa hata na makamu wa rais ambaye ni mwajiriwa wa siri wa nchi maadui, ingawa anaonekana yupo mstari wa mbele kwenye mapambano dhidi ya maadui.
Wakati tunaandika makala ya kuuawa kwa Hassan Nasrallah kiongozi mkuu wa Hezbollah, tuliweza kuona Israeli ina 'mole' ambaye ni mtu 'high profile' kiasi kwamba anaweza kupata taarifa sahihi za siri za daraja la kwanza.
Ndio maana 'mole' huyo aliweza kujua siku fulani, mahali fulani, muda fulani, Hassan Nasrallah atakuwa anafanya kikao.
Sasa, huyu mtu aliyeajiriwa na Mossad, IRGC inasema ni mtu yupo kwenye kikosi maalumu kinacholinda viongozi wa juu wa Iran!
Ndio maana unaona baada ya mauaji yale,
watu zaidi ya 12 walikamatwa. Watu hao ni maafisa wa ngazi za juu kabisa (seniour officials) waliopo kwenye 'units' za Intelijensia hapo jijini Tehran.
Pia, IRGC ilivamia guest ile na kuwaweka chini ya ulinzi wafanyakazi wote wa ile guest na kuwaweka 'karantini' kwa ajili ya uchunguzi 'heavy' na wakiwa pia wamepokonywa simu zao kwa ajili ya kuzichunguza.
Raphael Mtui 0762731869