Tujikumbushe MV Bukoba enzi za uhai wake

Yaani pamoja na kukutana na huyo mtu muhimu kwa hii taarifa ukaishia kupiga nae stori kuhusu ukubwa Wa usukani tu? Ulipaswa utuletee episode kadhaa juu ya ile ajali ndugu. Au kama alikueleza zaidi tupe na sisi
 
Duuuu
 

Kwaiyo watu waache kutianaa kisa majini ? Ingekuwa Mungu sawa, ila majini nop, waendelee tu kukazana ... Dunia ni ya Mungu sio majini.. Akikataa Mungu sawa ila sio jini
 
Yaani pamoja na kukutana na huyo mtu muhimu kwa hii taarifa ukaishia kupiga nae stori kuhusu ukubwa Wa usukani tu? Ulipaswa utuletee episode kadhaa juu ya ile ajali ndugu. Au kama alikueleza zaidi tupe na sisi
Kwanza kabisa alikuwa ni mtu wangu wa karibu kipindi hicho nakutana naye, alikiwa ni miongoni mwa wenyeji wangu. Sikuwa na haraka ya kumuuliza kisa cha Meli kuzama maana nilijua atanisimulia siku za mbeleni wakati nikiendelea kuishi sehemu hizo.

Kabla sijafanya ajizi nikaanza mishe zangu sehemu fulani hapo jijini Mwanza na yeye ghafla akaanza kuugua na akaanza kupata matibabu pale Bugando. Nikawa naenda kimsalimia nikiwa na mawazo ya kufikiria juu ya kuugua kwake na nikaelekeza fikra zangu kumliwaza kama ilivyo kawaida ya wagonjwa kuliwazwa na kufarijiwa.

Kadri siku zinavyozidi kwenda hali ikawa mbaya zaidi, kufika mwezi wa 6 mwaka 2009 akawa ameaga Dunia.

Kutopata simulizi ya kisa cha Meli kuzama ni kosa ambalo limelifanya baada ya kukutana na Marehemu mzee Rume.
 
We jamaa umesoma nyanza na umekaa nera?!!the same to me


96 ulikua darasa la ngapi kama la pili itakua we ni classmate wangu tena from the same neighborhood!!!

Nakumbuka tulikua tunakaa kwenye kile kimlima juu(nera)kinachoangalia ziwani kuangalia zoez la uokoaji coz shule ilifungwa due to huo msiba wa kitaifa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Doooh Sawa ndugu,pole pia kwa kuondokewa na jamaa aisee japo ni kitambo.
 
Kwa dar mobitel ilianza mwaka gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani pamoja na kukutana na huyo mtu muhimu kwa hii taarifa ukaishia kupiga nae stori kuhusu ukubwa Wa usukani tu? Ulipaswa utuletee episode kadhaa juu ya ile ajali ndugu. Au kama alikueleza zaidi tupe na sisi
Ile meli nilikuwa naipanda toka niko form one had kidato cha nne ilipozama haikuwa kubwa kihivyo.Meli kubwa zaidi ni MV Victoria.Zote nimezipanda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kiliniuma sana wale wanafunzi wasichana wa Rugabwa waliokuwa wamemaliza kidato cha sita wote waliteketea; walivyoona sasa wanakufa walishikana wote kuagana kwa safari ya milele - too sad.
Tulisalia wachache ambao hatukupanda meli ile
 
Tupe historia Kidogo ilkuaje na vipi maisha baada ya ajali, kwan naambiwa mtihani ulipoteaa ikabdii kuurudia

Sent using Jamii Forums mobile app
Yes tulirudia mitihani kwa sababu ya awali ilizama katika meli. Katika darasa la watu 58 tulibaki 26. Tulirudi shule kabla hawajafungua likizo ya June. Kufanya mitihani ukiwa kwenye tension ya kupoteza wenzio na kwamba huna materials za kujisomea na wakati huo mko wachache sana shuleni ilikua changamoto lakini lilipita na maisha yanaendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…