Tujikumbushe MV Bukoba enzi za uhai wake

Tujikumbushe MV Bukoba enzi za uhai wake

!
!
Nia nzuri huenda alikuwa nayo ila uwezo wake wa kufikiri na kitendea ulikuwa mdogo mno. Maamuzi yake yalizamisha meli nayeye sidhani kama alipona.
Ingekuwa ni kipindi hiki Cha kushamiri kwa social media Sijui Hali ingekuwa...malalamiko na shutuma kwa serikali zingekuwa za kutisha...kipindi hicho Mr. 'Clean' Alikuwa na muda mfupi tu madarakani yaani chini ya mwaka mmoja...Nyerere Alikuwa Yuko hai..Nyerere alikwenda Hadi Mwanza kumpa pole Mr. 'Clean' kwa msiba huu wa taifa
 
Nimewahi kufanya safari na hii meli mara kadhaa siku za hapo nyuma, Ukweli hii meli ilikuwa si chakavu, Mimi ni mvuvi wa siku nyingi sana, moja ya mambo ambayo avitakiwi ukiwa ziwani ni vitendo vyovyote vya kufanya ngono majini, binafsi ktk safari ndani ya meli hiyo nikiwa ninasafiri nimeshuhudia mara kadhaa abiria wakitenda matendo hayo! Majini huwa kuna majini awapendi huo uchafu, Pia mbali ya idadi kubwa ya watu siku ya tukio la kuzama hiyo meli, Abiria kuelekea upande mmoja nayo ni moja ya sababu ya kutokea maafa siku ile ya tukio la MV Bukoba,pamoja na kwamba siku ile ya tukio hali ya ziwa ilikuwa shwali.
Mmh
 
Alinusurika mmoja aliepanda meli ile lakini alikua mbali na wenzetu kwaiyo si rahisi kujua kama ni kweli walishikana au la. Na katika wanafunzi wote watatu ndio walipatikana, mmoja alizikwa kwao na wawili walizikwa Igoma.
Shangazi yangu alifariki alkuwa anaitwa Tabu,sijui shuleni alkuwa anatumia jina gani?
 
Nakumbuka hii siku ilikuwa jumatano kama sikosei nikiwa darasa la Pili, nikiwa tayari nimeshajiandaa kwenda shule mida ya saa nne asubuhi ndipo niliposikia habari Mvunjiko kutoka Radio Free Africa, nikamuita dada angu aje asikilize.

Hakuweza kuvumilia, akapiga ukunga, watu wakaja kujua nini kimetokea, mmoja wa waliokuja alikuwa ni mke wa mwalimu wetu wa tuition alikuwa ni mhaya. Kumbe yule mama alikuwa anamsubiri mgeni wake kutoka Bukoba na alikuwa ndani ya ile meli. Yule mama alipagawa, wala hata hakufunga ofisi yake akakimbia kwenda Custom. Tuliokuwa Mwanza kipindi hiko tunajua namna mji ulivyozizima kwa Majonzi kipindi kile
Form V mwaka huo. Tunajiandaa na mitihani ya 2nd term. Nililazimisha akili isiamini Dada yangu kuwemo kwenye meli. Wiki tatu kabla nilikuwa Mwanza. Mzee alikwenda Rugambwa kuhudhuria Graduation ya FVI. Dadangu akampa mabegi karibu yote ya nguo zake atangulie nazo Mwanza maana anataka ajielekeze kupambana na National Exams. Mitihani alifanya ila safari yake kurudi kwa wazazi alikotanguliza mizigo iliishia Bwiru ziwani. Kumbukumbu mbaya kabisa.

Mungu huyu aliyeumba mbingu na nchi ni mwema sana. Anajua kutufuta machozi. Anajua kutufurahisha. Sifa na utukufu kwa Yesu Kristo.
 
Mkuu hii meli ndo wanasemaga muwa uliizamisha si ndo hii mkuu
Tesla, halafu kweli Fizikia inasemaje hapa? Ulishawahi kukuta ndege imeanguka matairi yako juu? Meli je inaweza ku-overturn? Kama inaweza, ni kwa namna gani?
 
Nimewahi kufanya safari na hii meli mara kadhaa siku za hapo nyuma, Ukweli hii meli ilikuwa si chakavu, Mimi ni mvuvi wa siku nyingi sana, moja ya mambo ambayo avitakiwi ukiwa ziwani ni vitendo vyovyote vya kufanya ngono majini, binafsi ktk safari ndani ya meli hiyo nikiwa ninasafiri nimeshuhudia mara kadhaa abiria wakitenda matendo hayo! Majini huwa kuna majini awapendi huo uchafu, Pia mbali ya idadi kubwa ya watu siku ya tukio la kuzama hiyo meli, Abiria kuelekea upande mmoja nayo ni moja ya sababu ya kutokea maafa siku ile ya tukio la MV Bukoba,pamoja na kwamba siku ile ya tukio hali ya ziwa ilikuwa shwali.
Uongo mwingine bhana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Form V mwaka huo. Tunajiandaa na mitihani ya 2nd term. Nililazimisha akili isiamini Dada yangu kuwemo kwenye meli. Wiki tatu kabla nilikuwa Mwanza. Mzee alikwenda Rugambwa kuhudhuria Graduation ya FVI. Dadangu akampa mabegi karibu yote ya nguo zake atangulie nazo Mwanza maana anataka ajielekeze kupambana na National Exams. Mitihani alifanya ila safari yake kurudi kwa wazazi alikotanguliza mizigo iliishia Bwiru ziwani. Kumbukumbu mbaya kabisa.

Mungu huyu aliyeumba mbingu na nchi ni mwema sana. Anajua kutufuta machozi. Anajua kutufurahisha. Sifa na utukufu kwa Yesu Kristo.
Pole sana mkuu,samahani lakini kwa hili swali, vipi marehemu alipatikana??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nisaidie citation ya hiyo case

Nilikuja kufahamu kiundani kilichotokea siku ya ajali ya meli hii pale niliposoma hukumu ya walioshitakiwa kusababisha ajali hiyo. Miongoni mwao alikuwemo captain..

Mashahidi waliotoa ushahidi mahakamani walinipa picha kamili ya kile kilichotokea. Lilikuwa janga kubwa sana.
 
49084f27b80275392537b418022a96b5.jpg
f4604464002f7be1e1669c1df1b6359f.jpg
MV Bukoba ilikuwa moja ya meli kubwa katika ziwa Victoria. Ilikuwa ina uwezo wa kusafirisha watu zaidi ya 400 na tani zaidi ya 100.

Meli hii ilikuwa ikiondoka Bukoba siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Meli hii sio kongwe kama ilivyokuwa MV Victoria iliyojengwa mwaka 1961; hii ilijengwa mwaka 1979 lakini ilikuwa chini viwango na mbovu kuliko MV Victoria.

Meli iliua watu zaidi ya 800 siku ya Jumanne ya tarehe 21 ya mwezi wa tano mwaka 1996 eneo la Bwiru KM 30 kutoka bandari ya Mwanza.

Basi nawakaribisheni mwenye kujua chochote kuhusu meli hii au alishasafiri na meli hii au aliponea chupuchupu ajali atupe experience.

Karibuni
Hii ajali iliua mamdogo zangu wawili.............uncle wangu alinusurika may be kwasababu ni diver... Japo bado hyo sio sababu ya kupona kwake,Ni Mungu tu.
 
Back
Top Bottom