Tujikumbushe MV Bukoba enzi za uhai wake

!
!
Nia nzuri huenda alikuwa nayo ila uwezo wake wa kufikiri na kitendea ulikuwa mdogo mno. Maamuzi yake yalizamisha meli nayeye sidhani kama alipona.
Ingekuwa ni kipindi hiki Cha kushamiri kwa social media Sijui Hali ingekuwa...malalamiko na shutuma kwa serikali zingekuwa za kutisha...kipindi hicho Mr. 'Clean' Alikuwa na muda mfupi tu madarakani yaani chini ya mwaka mmoja...Nyerere Alikuwa Yuko hai..Nyerere alikwenda Hadi Mwanza kumpa pole Mr. 'Clean' kwa msiba huu wa taifa
 
Mmh
 
Alinusurika mmoja aliepanda meli ile lakini alikua mbali na wenzetu kwaiyo si rahisi kujua kama ni kweli walishikana au la. Na katika wanafunzi wote watatu ndio walipatikana, mmoja alizikwa kwao na wawili walizikwa Igoma.
Shangazi yangu alifariki alkuwa anaitwa Tabu,sijui shuleni alkuwa anatumia jina gani?
 
Form V mwaka huo. Tunajiandaa na mitihani ya 2nd term. Nililazimisha akili isiamini Dada yangu kuwemo kwenye meli. Wiki tatu kabla nilikuwa Mwanza. Mzee alikwenda Rugambwa kuhudhuria Graduation ya FVI. Dadangu akampa mabegi karibu yote ya nguo zake atangulie nazo Mwanza maana anataka ajielekeze kupambana na National Exams. Mitihani alifanya ila safari yake kurudi kwa wazazi alikotanguliza mizigo iliishia Bwiru ziwani. Kumbukumbu mbaya kabisa.

Mungu huyu aliyeumba mbingu na nchi ni mwema sana. Anajua kutufuta machozi. Anajua kutufurahisha. Sifa na utukufu kwa Yesu Kristo.
 
Mkuu hii meli ndo wanasemaga muwa uliizamisha si ndo hii mkuu
Tesla, halafu kweli Fizikia inasemaje hapa? Ulishawahi kukuta ndege imeanguka matairi yako juu? Meli je inaweza ku-overturn? Kama inaweza, ni kwa namna gani?
 
Uongo mwingine bhana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu,samahani lakini kwa hili swali, vipi marehemu alipatikana??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nisaidie citation ya hiyo case

 
Hii ajali iliua mamdogo zangu wawili.............uncle wangu alinusurika may be kwasababu ni diver... Japo bado hyo sio sababu ya kupona kwake,Ni Mungu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…