Tujikumbushe MV Bukoba enzi za uhai wake

Tujikumbushe MV Bukoba enzi za uhai wake

Hatari, nasikia huyo jamaa alipigiwa simu na tajiri aliyekuwa kwenye meli kwamba huyo tajiri alikuwa na million 80 na ambaye angemuokoa angechukuwaa hizo pesa. Ndo jamaa wakapagawa wakabeba mitungi ya gesi wakaenda kutoboa ili wamtoe tajiri wapate pesa. Ttizo lilikuwa elimu maana walisombwa wote kungizwa kwenye meli maana maji yaliingia kwa pressure kali nao wakafa.
Hii ni kweli au?
 
Hii ajali ilibadili kabisa mwelekeo WA maisha yangu maana nilimpoteza baba yangu kipenzi, yeye ndo alikuwa kila kitu katika kulea familia hivyo baada ya ajali kila kitu kikasimama ghafla. Shukrani kwa mama yetu aliyeweza kusimama kidete na kutupa nuru mpya.
Pole sana
 
MV-Bukoba.jpg
 
kiliniuma sana wale wanafunzi wasichana wa Rugabwa waliokuwa wamemaliza kidato cha sita wote waliteketea; walivyoona sasa wanakufa walishikana wote kuagana kwa safari ya milele - too sad.
Tena mwezi wa tano ndo form six inaisha poleni sana
 
Hii ajali ilibadili kabisa mwelekeo WA maisha yangu maana nilimpoteza baba yangu kipenzi, yeye ndo alikuwa kila kitu katika kulea familia hivyo baada ya ajali kila kitu kikasimama ghafla. Shukrani kwa mama yetu aliyeweza kusimama kidete na kutupa nuru mpya.
pole sana
 
Sijui watanzania tuna tatizo gani na kuoverweight hata kwenye gar imeandikwa tan moja gar inabeba tan na nusu siti za watu wa tano tunakaa 9
Inatubidi tubadilike ajali nyingi ni uzembe wetu
 
Hatari, nasikia huyo jamaa alipigiwa simu na tajiri aliyekuwa kwenye meli kwamba huyo tajiri alikuwa na million 80 na ambaye angemuokoa angechukuwaa hizo pesa. Ndo jamaa wakapagawa wakabeba mitungi ya gesi wakaenda kutoboa ili wamtoe tajiri wapate pesa. Ttizo lilikuwa elimu maana walisombwa wote kungizwa kwenye meli maana maji yaliingia kwa pressure kali nao wakafa.

!
!
Yule jamaa alikuwa kiazi kwelikweli
 
Kweli kuna kitu hakipo sawa na sehemu ilipozamia km 30 toka bandarini ukiangalia ni chini ya m 10 kwa mujibu ya hivyo vipimo.....inamaana ilizama sehemu ambayo yenyewe ni ndefu kuliko kina?
Tatizo ni kwamba, ilitumika akili ndogo za wanasiasa in attempt to rescue the victims, they refused to heed to professional advise.
 
Inasikitisha sana uwezo wa meli ni watu 400 ila Siku ya tukio imeua zaidi ya watu 800 huu ulikuwa uzembe wa hali ya juu kwa wahusika wa hiyo meli..
Matukio mengine ni ya kuyaepuka kama sio kuyazuia kabisa ila katika hili tujifunze ili yasitokee ya wakati huo..

Kwa mtini jifunzeni
 
Hii ilimkosakosa baba yangu mpenzi, nakumbuka siku hiyo alienda bandari ya bk kupanda hii meli kwa safari ya Mwanza......... na ilikua dingi akisafiri ni full shangwe nyumbani mixer kujiachia sana kwa makelele, ghafla tunasikia mtu anakohoa chumbani ile kuchungulia ni mshua kalala na hatukujua karudi saa ngapi jioni ile. Baadae akatuambia kwa masikitiko kwamba meli imejaa sana hivo hakupata usafiri. Kesho yake yakawa haya........
Duh, story yako imefanana na Ya mshkaji wangu sana, na yeye Mzee wake ilimkosakosa hivyo hivyo kwasababu ya kujaa!
 
Mkuu hii meli ndo wanasemaga muwa uliizamisha si ndo hii mkuu
Hapana siyo hii...
Nakumbuka baada ya hiyo ajali wakati maiti zinaletwa kwa MV serengeti kutoka mwanza kuja Bukoba nilienda kushuhudia, aisee Mv Serengeti ilikuwa inanuka harufu ya uozo tu, na majeneza yakikuwa makubwa kutokana na amaiti kuvimba matumbo.
Pia siku hiyo ndipo niliacha kutaman kazi ya Red Cross maana wao ndiyo walikuwa wakibeba ma kupakia yale majeneza.
Sikuweza kula kwa siku kadhaa aisee
 
Back
Top Bottom