Tujikumbushe MV Bukoba enzi za uhai wake

Tujikumbushe MV Bukoba enzi za uhai wake

Hapana siyo hii...
Nakumbuka baada ya hiyo ajali wakati maiti zinaletwa kwa MV serengeti kutoka mwanza kuja Bukoba nilienda kushuhudia, aisee Mv Serengeti ilikuwa inanuka harufu ya uozo tu, na majeneza yakikuwa makubwa kutokana na amaiti kuvimba matumbo.
Pia siku hiyo ndipo niliacha kutaman kazi ya Red Cross maana wao ndiyo walikuwa wakibeba ma kupakia yale majeneza.
Sikuweza kula kwa siku kadhaa aisee
Red Cross inahitaji moyo
 
Sitaisahau hii ajali maana watanzania wenzangu wengi walipoteza maisha.

Nilikuwa Paris, France kikazi. Yaani, siku hiyo wanetu wawili na mke wangu walilia sana.

Hadi leo, wanetu hawapendi kabisa kupanda meli au boat.

Tatizo, kubwa ni kuweka vichwa maji kwenye nafasi za professionals.

Hadi leo hizo MV Seregenti na MV Victoria bado zinazidisha abiri na mizigo.
Yaani, mara nyingi sana Africa hatujifunzi kutoka na na makosa.
 
Marehemu baba mjomba na mdogo wangu walinusurika baada ya kuchelewa kufika na kukuta meli inang'oa nanga wakakimbia kemondo wakaona meli imejaa haswaa ikawabidi warudi nyumbani huku wanahuzunika kukosa usafiri kesho yake ndo yakatokea yaliyotokea, poleni sana sana wote walioachwa na vidonda katika ajali ile
 
Mkuu vp suala hili:Kwamba serikal waliambiwa wataitolewa kule ziwani wakakataa NI KWEL??
 
Hatari, nasikia huyo jamaa alipigiwa simu na tajiri aliyekuwa kwenye meli kwamba huyo tajiri alikuwa na million 80 na ambaye angemuokoa angechukuwaa hizo pesa. Ndo jamaa wakapagawa wakabeba mitungi ya gesi wakaenda kutoboa ili wamtoe tajiri wapate pesa. Ttizo lilikuwa elimu maana walisombwa wote kungizwa kwenye meli maana maji yaliingia kwa pressure kali nao wakafa.
Kipindi hicho Mwanza hakukua na simu za mkononi, mobitel ilianza huku mwaka 1997 na Mwanza nzima walikuwa na mnara mmoja tu kule juu ya ghorofa la 10 Bugando. Hao waliobeba mitungi ilikuwa ni timu ya uokoaji iliyokuwa na baraka za mamlaka husika.

Siku hiyo tukiwa tumetoka mapumziko ya saa 4 shule ya msingi Bugando tuliona magari mengi yakiwa yamebeba watu yakipanda mlima kuwahi Bugando hospital na tukasikia watu wakubwa wakisema kuna meli imezama.

Tulipotoka darasani saa 8 mchana mwisho wa vipindi darasani mimi sikusubili mpaka tutawanyishwe nilikimbia mpaka Kastam kwa maana ya bandarini kwenda kushuhudia kinachojili. Pale nilikuta watu wengi sana na wengine wanamitungi ya gas iliyokuwa imepelekwa kutobolea meli wakiwatangazia watu kuwa wametoka eneo la ajari wakiacha meli imezama na kutoonekana kabisa. Hapo umati ulianza kutawanyika na wengine kukimbilia Bugando hospital kuona maiti na walionusurika.

Maiti zilizo oza liliwekwa pale Nyamagana stadium ili ndugu waende kuzitambua na zile zilizokosa ndugu zilipelekwa kuzikwa Igoma kwenye kiwanja maarum.
Duh kumbe haikuwa deep kihivyo mie nlikuwa nafikiria sijui mtr 500 kwenda chini duh ahsante kwa taarifa
 
Kiukweli ile ajali ni ya kihistoria. Inatisha mno! Mkoa wa Kagera karibia kila mtu alifiwa ...kama si ndugu kuna mtu unamfahamu! Teknolojia mbovu ilitutia hasara kubwa sana. Meli ilizama pole pole hadi inapotea hakuna anayejua la kufanya! Afadhali hata "magenius" waliofikiria kuitoboa ili kuokoa watu ingawa ndio iliongeza kasi ya meli kuzama ikiwa na watu zaidi ya mia nane! Dah!
 
kiliniuma sana wale wanafunzi wasichana wa Rugabwa waliokuwa wamemaliza kidato cha sita wote waliteketea; walivyoona sasa wanakufa walishikana wote kuagana kwa safari ya milele - too sad.
mh!
 
Nilikuja kufahamu kiundani kilichotokea siku ya ajali ya meli hii pale niliposoma hukumu ya walioshitakiwa kusababisha ajali hiyo. Miongoni mwao alikuwemo captain..

Mashahidi waliotoa ushahidi mahakamani walinipa picha kamili ya kile kilichotokea. Lilikuwa janga kubwa sana.
 
Sisi wengine tulikuwa hatujui kinachoendelea duniani wakati huo ingawa tayari tulikuwa wakubwa kidogo,kama miaka 7 kuelekea 8. Sijui kwakuwa tuliishi vijijini au kwakuwa tulikuwa kanda ya mbali na kanda ya ziwa.
Naufuatilia huu uzi ili nijue kwa undani zaidi nipate ya kujifunza ingawa inauma sana.
 
Back
Top Bottom