Tujikumbushe penzi la Juma Nature na Sinta

Tujikumbushe penzi la Juma Nature na Sinta

Ebhanaa eee daaah hapo tupo mikoani tunawaza dar tutafika lini? Enzi izo tunanunua kanda ambazo zina bongo fleva mchanganyiko, nature nilikua namkubali mpaka basi, hio inaniuma sanaa hadi leo nnayo kwenye simu yangu.
 
Kwenye ngoma inaitwa Taswira yumo Dojo, Domo na Inspecta kuna mstari unasema..

"..namuona Juma Nature ufukweni namuona Sinta,

Namuona P Diddy analilia penzi la Jenifa..."
yap...hiyo line naikumbuka mkuu..daahh ila sinta alikuwa balaa aiseee huwa nazifananisha drama zake na Elizabeth michael
 
Necha ana ile nyimbo yake..anasema " akatokea jamaa sijui anautahira gani.."
Yaani huwa nacheka sana mistari yake ilikuwa imekaa kiswahili sana...yaani lazima ufurahi....
Juma alichange alivyotoa mgambo lakini Bado alikuwa na love...kutoka kwa fans...kosa lilikuwa kuendelea na style ile ile ya mgambo ikamfanya asiwe kibishara...+ bifu na kina Tale wakambania ktk media na isingekuwa umaarufu wake hata zile show asingepata
 
Mademu tuliokuwa tunawaona wakali zamani kwenye TV ukiwaangalia kwenye marudio ya hizo tamthilia zao za nyuma unamuona mlugaluga sana wakati kipindi hicho alikuwa anakamata,labda wakati huu kuna kila dizaini ya urembo so mademu wengi wakare hata wa uswazi.
 
Kwenye ngoma inaitwa Taswira yumo Dojo, Domo na Inspecta kuna mstari unasema..

"..namuona Juma Nature ufukweni namuona Sinta,

Namuona P Diddy analilia penzi la Jenifa..."
Hili lilikuwa Dis kwa Nature, sema hawa watoto wa mjini walivyo lipindua pindua zaidi ya kifurushi cha vod, Nature alitoka kapa hakujua kama walimaanisha ni yeye. Na jamaa kuohifia povu la Nature ikabidi waiweke vile.
 
Back
Top Bottom