Tujikumbushe sakata la Rada

Tujikumbushe sakata la Rada

Rada mzigo mzito

na Edward Kinabo

SERIKALI imetangaza zabuni ya ununuzi wa betri mpya ya rada ya kuhifadhia umeme wa dharura ‘UPS’, ambayo inadaiwa kugharimu zaidi ya sh bilioni 10.

Rada hiyo iliyonunuliwa kwa paundi milioni 28, sawa na sh bilioni 40 mwaka 2001, kutoka Shirika la Vifaa vya Ndege la Uingereza, British Aerospace (BAE System), ndiyo inayotumika kuongoza ndege za kiraia na kijeshi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, lakini kwa miezi miwili sasa haifanyi kazi kutokana na ubovu huo.

Hadi sasa makampuni kadhaa ya ndani na nje, yamejitokeza kuomba zabuni hiyo ili kuikwamua rada hiyo.

Vyanzo vyetu vya habari kutoka idara ya rada, vilisema UPS hiyo inagharimu zaidi ya sh bilioni 10 na tayari makampuni kadhaa ya ndani na nje, yamechangamkia zabuni hiyo.

“Kwa miezi miwili sasa rada haifanyi kazi baada ya kuharibika na kifaa kilichoharibika kinaweza kuwa na thamani ya zaidi ya sh bilioni 10 na hivi tunavyosema, tayari makampuni kadhaa ya ndani na nje, yamechangamkia zabuni hiyo,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Ofisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Abel Ngapemba, aliithibitishia Tanzania Daima mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa hivi sasa maombi ya zabuni hiyo yapo katika hatua ya kufanyiwa tathmini ili kumpata mwenye sifa.

Hata hivyo Ngapemba ambaye hakutaka kuzungumzia kwa undani suala hili, alisema, hajui betri hiyo itagharimu kiasi gani, na hakuwa tayari pia kutaja idadi ya makampuni ya ndani na nje yaliyoomba kununua kifaa hicho.

Msemaji huyo, pia hakuweza kusema ni lini hasa mchakato wa ununuzi wa kifaa hicho utakamilika na rada hiyo kuendelea kufanya kazi kama awali.

Taarifa za kuzimwa kwa rada hiyo iliyonunuliwa katika mazingira tatanishi mwaka 2001 kutoka Kampuni ya BAE System, ziliifikia Tanzania Daima kupitia vyanzo vyake vya habari, takriban wiki mbili zilizopita.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Margaret Munyagi, wiki iliyopita alikaririwa akithibitisha kuharibika kwa chombo hicho.

Alisema rada hiyo ilizima baada ya betri yake inayohifadhi na kutoa umeme wa dharura ‘UPS’ pindi umeme unapokatika, kuharibika.

Hata hivyo, Munyagi, alisema tatizo hilo ni la kawaida na dogo na kwamba haliwezi kuathiri huduma za usafiri wa anga na shughuli nyingine uwanjani hapo.

Alisema mafundi wa TCAA, walikuwa wanaangalia uwezekano wa kununuliwa kwa kifaa hicho kutoka nje ya nchi haraka iwezekanavyo.

Ununuzi wa rada hiyo uliofanywa wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, ulipingwa vikali na wabunge wa Uingereza ‘House of Commons’ na wa kambi ya upinzani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa madai kuwa gharama yake ilikuwa kubwa kuliko uwezo wake.

Pia walipinga kwa madai kuwa Tanzania ingeweza kununua rada ya bei ya chini zaidi ya hiyo ambayo ingeweza kukidhi mahitaji.

Wengine waliopinga ununuzi wa rada hiyo ni Benki ya Dunia (WB), Taasisi ya Fedha ya Kimataifa (IMF) na Shirika la Huduma za Usafiri wa Anga (ICAO), zikisema gharama yake haikuwa halali.

ICAO, iliwahi kusema wazi kuwa teknolojia iliyotumika kutengeneza rada hiyo ni ya zamani na ni ghali, na kwamba ingeweza kutumika kwa muda mfupi na isingefanikisha uongozaji wa ndege kwa maendeleo ya sekta ya utalii nchini.

Wabunge wa Uingereza walikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa kulikuwa na rushwa katika mchakato wa ununuzi wake.

Ofisi ya kuchunguza rushwa kubwa ya Uingereza, Serious Fraud Office (SFO), iligundua kuwa Kampuni ya BAE System, ililipa dola milioni 12 kwa mfanyabiashara Sailesh Vithlani, mzaliwa wa Mwanza, katika akaunti yake ya Uswisi.

Mfanyabiashara huyo ambaye sasa ni raia wa Uingereza, ndiye aliyekuwa wakala wa Serikali ya Tanzania katika ununuzi wa rada hiyo.

Makachero wa SFO waliifahamisha Serikali ya Tanzania kuhusu akaunti za Vithlani na uhusiano wake na BAE System na walimhoji mfanyabiashara huyo nchini, mbele ya maofisa wa Taasisi ya Kudhibiti na Kuchunguza Rushwa nchini (Takukuru).

Hata hivyo, Vithlani aliondoka nchini na baadaye, Takukuru ilipeleka kesi mahakamani Novemba 2007 na kutoa wito kuwa mfanyabiashara huyo, atafutwe.

Hapa nchini, kashfa ya rada imemgusa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, ambaye aliamua kujiuzulu nafasi yake baada ya kukabiliwa na tuhuma za kumiliki zaidi ya dola milioni moja za Marekani katika akaunti yake iliyopo Kisiwa cha Jersey, nchini Uingereza.

SFO bado inafanya uchunguzi kuhusu fedha za Chenge, kuangalia iwapo zina uhusiano na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada hiyo.

Wakati rada hiyo inanunuliwa, Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Wiki iliyopita, Mkurungezi wa Mashitaka nchini, (DPP), Eliezer Feleshi, alisema kesi hiyo bado iko mahakamani na mfanyabiashara Vithlani, anatafutwa.

Kama UPS tu inacost 10 bil basi vichwa vya waliotuingiza kwenye huu mkenge ni halali yetu! 10 Bil inaweza kuokoa wakinamama wajawazito wangapi kwa kuwapelekea huduma za zahanati karibu na makazi yao (vijijini) inauwezo wa kujenga barabara kilometa ngapi?nyumba za waalimu ngapi? hawa waliotuingiza kwenye huu mkenge ni wale wanaolindwa na sheria za haki za binadamu. Hawa ndio binadamu kuliko sisi Binadamu hawa leo wanayaweka maisha ya watanzania milioni 40 korokoroni maana tunaambiwa rada ni mbovu hii ina amanisha nchi si salama na tunaweza kuvamiwa muda wowote ee Mungu tulinde waja wako. Amin.
 
Isije kuwa wamenunua kwa ajili ya kuongozea Private Jet zao ambazo kwa vijisenti walivyonavyo wanakuwa na uwezo kamili wa kumiliki vitu hivyo.
 
Rada mzigo mzito

na Edward Kinabo

SERIKALI imetangaza zabuni ya ununuzi wa betri mpya ya rada ya kuhifadhia umeme wa dharura ‘UPS’, ambayo inadaiwa kugharimu zaidi ya sh bilioni 10.

Rada hiyo iliyonunuliwa kwa paundi milioni 28, sawa na sh bilioni 40 mwaka 2001, kutoka Shirika la Vifaa vya Ndege la Uingereza, British Aerospace (BAE System), ndiyo inayotumika kuongoza ndege za kiraia na kijeshi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, lakini kwa miezi miwili sasa haifanyi kazi kutokana na ubovu huo.

Hadi sasa makampuni kadhaa ya ndani na nje, yamejitokeza kuomba zabuni hiyo ili kuikwamua rada hiyo.

Vyanzo vyetu vya habari kutoka idara ya rada, vilisema UPS hiyo inagharimu zaidi ya sh bilioni 10 na tayari makampuni kadhaa ya ndani na nje, yamechangamkia zabuni hiyo.

“Kwa miezi miwili sasa rada haifanyi kazi baada ya kuharibika na kifaa kilichoharibika kinaweza kuwa na thamani ya zaidi ya sh bilioni 10 na hivi tunavyosema, tayari makampuni kadhaa ya ndani na nje, yamechangamkia zabuni hiyo,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Ofisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Abel Ngapemba, aliithibitishia Tanzania Daima mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa hivi sasa maombi ya zabuni hiyo yapo katika hatua ya kufanyiwa tathmini ili kumpata mwenye sifa.

Hata hivyo Ngapemba ambaye hakutaka kuzungumzia kwa undani suala hili, alisema, hajui betri hiyo itagharimu kiasi gani, na hakuwa tayari pia kutaja idadi ya makampuni ya ndani na nje yaliyoomba kununua kifaa hicho.

Msemaji huyo, pia hakuweza kusema ni lini hasa mchakato wa ununuzi wa kifaa hicho utakamilika na rada hiyo kuendelea kufanya kazi kama awali.

Taarifa za kuzimwa kwa rada hiyo iliyonunuliwa katika mazingira tatanishi mwaka 2001 kutoka Kampuni ya BAE System, ziliifikia Tanzania Daima kupitia vyanzo vyake vya habari, takriban wiki mbili zilizopita.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Margaret Munyagi, wiki iliyopita alikaririwa akithibitisha kuharibika kwa chombo hicho.

Alisema rada hiyo ilizima baada ya betri yake inayohifadhi na kutoa umeme wa dharura ‘UPS’ pindi umeme unapokatika, kuharibika.

Hata hivyo, Munyagi, alisema tatizo hilo ni la kawaida na dogo na kwamba haliwezi kuathiri huduma za usafiri wa anga na shughuli nyingine uwanjani hapo.

Alisema mafundi wa TCAA, walikuwa wanaangalia uwezekano wa kununuliwa kwa kifaa hicho kutoka nje ya nchi haraka iwezekanavyo.

Ununuzi wa rada hiyo uliofanywa wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, ulipingwa vikali na wabunge wa Uingereza ‘House of Commons’ na wa kambi ya upinzani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa madai kuwa gharama yake ilikuwa kubwa kuliko uwezo wake.

Pia walipinga kwa madai kuwa Tanzania ingeweza kununua rada ya bei ya chini zaidi ya hiyo ambayo ingeweza kukidhi mahitaji.

Wengine waliopinga ununuzi wa rada hiyo ni Benki ya Dunia (WB), Taasisi ya Fedha ya Kimataifa (IMF) na Shirika la Huduma za Usafiri wa Anga (ICAO), zikisema gharama yake haikuwa halali.

ICAO, iliwahi kusema wazi kuwa teknolojia iliyotumika kutengeneza rada hiyo ni ya zamani na ni ghali, na kwamba ingeweza kutumika kwa muda mfupi na isingefanikisha uongozaji wa ndege kwa maendeleo ya sekta ya utalii nchini.

Wabunge wa Uingereza walikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa kulikuwa na rushwa katika mchakato wa ununuzi wake.

Ofisi ya kuchunguza rushwa kubwa ya Uingereza, Serious Fraud Office (SFO), iligundua kuwa Kampuni ya BAE System, ililipa dola milioni 12 kwa mfanyabiashara Sailesh Vithlani, mzaliwa wa Mwanza, katika akaunti yake ya Uswisi.

Mfanyabiashara huyo ambaye sasa ni raia wa Uingereza, ndiye aliyekuwa wakala wa Serikali ya Tanzania katika ununuzi wa rada hiyo.

Makachero wa SFO waliifahamisha Serikali ya Tanzania kuhusu akaunti za Vithlani na uhusiano wake na BAE System na walimhoji mfanyabiashara huyo nchini, mbele ya maofisa wa Taasisi ya Kudhibiti na Kuchunguza Rushwa nchini (Takukuru).

Hata hivyo, Vithlani aliondoka nchini na baadaye, Takukuru ilipeleka kesi mahakamani Novemba 2007 na kutoa wito kuwa mfanyabiashara huyo, atafutwe.

Hapa nchini, kashfa ya rada imemgusa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, ambaye aliamua kujiuzulu nafasi yake baada ya kukabiliwa na tuhuma za kumiliki zaidi ya dola milioni moja za Marekani katika akaunti yake iliyopo Kisiwa cha Jersey, nchini Uingereza.

SFO bado inafanya uchunguzi kuhusu fedha za Chenge, kuangalia iwapo zina uhusiano na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada hiyo.

Wakati rada hiyo inanunuliwa, Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Wiki iliyopita, Mkurungezi wa Mashitaka nchini, (DPP), Eliezer Feleshi, alisema kesi hiyo bado iko mahakamani na mfanyabiashara Vithlani, anatafutwa.

Bei ya UPS inayoweza kufanya kazi kama hiyo ya Rada Gharama yake si zaidi ya $200,000.00. Wakati niko GE (General Electric) tuliuzia state of California (LA International Airport) UPS kwa ajili ya Control ya RADA ambazo ziko hapo Los Angeles (LA) kwa siku ndege zaidi ya 300 zinatua na kuondoka. Na gharama ya hiyo UPS ilikuwa $178,000.00 tu. Ingia kwenye website ya GE wapigiye simu au website hii hapa wapigiye simu. http://www.custom-power.com/cp_prodlines.htm

CCM wanajiandaa kwa ajili ya Uchaguzi wa mwaka 2010 kwa hiyo hizo gharama wanafanya makusudi ili ifikapo mwaka 2010 wawe na Pesa za kutosha kwa kampeni ya uchaguzi.

Zunguka dunia nzima uwezi kununua UPS ya rada kwa Tshs 10 billion ambazo ni sawa na USD 10 million. Pili hiyo Rada nafikiri ilikuwa na Warrant, haiwezekani Rada ya 40 billion isiwe na warrant ya miaka 10 au 5. kwa siku mbili tu unasema UPS imekufa na unataka kununua kwa 10 billion (mother https://jamii.app/JFUserGuide). Watoto wanakufa kwa magonjwa wanawake wanakufa kwa kukosa dawa na huduma muhimu, kwa watu 3-5 wanaua mamillion ya vizazi vijavyo kwa sababu ya 10% ukiangalia hata umri wao karibu wanapelekwa kaburini.

Very sad. Very sad.

Angalia hii attachment, hiyo UPS ni kama hiyo waliyonayo hapo. kwa nini gharama iwe 10billion (shit).
 
Attachments

Kokolo,

Ndio wizi wa mchana huo, halafu tunaambiwa kuwa mambo ni kawaida. Swali hiyo tenda imetangazwa wapi? maana niko tayari kuingia na kuwapa UPS kwa gharama rahisi tena si moja tano za ziada na wanilipe kamisheni yangu 10% of the cost!
 
Kokolo Duh.,...umemaliza Mkuu...Huu WIZI Kweupe.....
 
Nimekwenda www.ppra.go.tz kuangalia ni vipi hii zabuni imetangazwa ili nami niingie kwenye uzabuni, tender hii ya UPS kwa ajili ya Radar haipo!

Nimetumia kila ujanja hata kuongeza wigo wa kutafuta tenda zote tangu May 1 2008 hakuna hii tenda.

Mwenye kujua mahali ilipotangazwa atuambie!
 
Aa,bwana wee, hatujui kama kweli imeharibika au vipi.Kuna methali moja ya kiswahili isemayo wajinga ndio waliwao.Ina wezekana hata haijaharibika,ila wanaendelea kutula tu,si unajua tenaa.

Naam hawa mafisadi wanaweza kufanya lolote lile kuhakikisha wanaendelea na ufisadi wao.
 
radar 40 billion, UPS 10! yaani robo ya thamani ya radar ni ups?! hii figa ya kweli jamani?

Naam kuna ufisadi bab kubwa hapa, haiwezekani kabisa Rada iliyonunuliwa kwa shilingi 28 bilioni (12 bilioni alipewa yule mhindi wakala aliyewagawia mafisadi mbali mbali akiwemo mzee wa vijisenti kupitia kwenye bank accounts zao nchi za nje) iharibike miaka michache baada ya kununuliwa kusiwe hata na warranty halafu chombo chenyewe kilichoharibika kinagharimu karibu nusu ya bei ya rada hiyo. WanaJF tulivalie njuga hili, kuna ufisadi hapa unataka kufanywa na mafisadi walio madarakani.
 
Nimekwenda www.ppra.go.tz kuangalia ni vipi hii zabuni imetangazwa ili nami niingie kwenye uzabuni, tender hii ya UPS kwa ajili ya Radar haipo!

Nimetumia kila ujanja hata kuongeza wigo wa kutafuta tenda zote tangu May 1 2008 hakuna hii tenda.

Mwenye kujua mahali ilipotangazwa atuambie!

Rev, Tenda za kifisadi zinatolewa chini ya uvungu kamwe huwezi kuiona hii.
 
Bubu,

Mara nyingine kuna watu wanaamini Serikali yetu ni safi, hapana Serikali ni chafu na imejaa wezi, wahujumu na wabangaizaji!

Yaani leo mnatuambia tumekaa miezi zaidi ya mitatu bila hii Rada tulioambiwa ni lazima tuwe nayo?
 
Back
Top Bottom