Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 129
Rada mzigo mzito
na Edward Kinabo
SERIKALI imetangaza zabuni ya ununuzi wa betri mpya ya rada ya kuhifadhia umeme wa dharura UPS, ambayo inadaiwa kugharimu zaidi ya sh bilioni 10.
Rada hiyo iliyonunuliwa kwa paundi milioni 28, sawa na sh bilioni 40 mwaka 2001, kutoka Shirika la Vifaa vya Ndege la Uingereza, British Aerospace (BAE System), ndiyo inayotumika kuongoza ndege za kiraia na kijeshi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, lakini kwa miezi miwili sasa haifanyi kazi kutokana na ubovu huo.
Hadi sasa makampuni kadhaa ya ndani na nje, yamejitokeza kuomba zabuni hiyo ili kuikwamua rada hiyo.
Vyanzo vyetu vya habari kutoka idara ya rada, vilisema UPS hiyo inagharimu zaidi ya sh bilioni 10 na tayari makampuni kadhaa ya ndani na nje, yamechangamkia zabuni hiyo.
Kwa miezi miwili sasa rada haifanyi kazi baada ya kuharibika na kifaa kilichoharibika kinaweza kuwa na thamani ya zaidi ya sh bilioni 10 na hivi tunavyosema, tayari makampuni kadhaa ya ndani na nje, yamechangamkia zabuni hiyo, kilisema chanzo chetu cha habari.
Ofisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Abel Ngapemba, aliithibitishia Tanzania Daima mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa hivi sasa maombi ya zabuni hiyo yapo katika hatua ya kufanyiwa tathmini ili kumpata mwenye sifa.
Hata hivyo Ngapemba ambaye hakutaka kuzungumzia kwa undani suala hili, alisema, hajui betri hiyo itagharimu kiasi gani, na hakuwa tayari pia kutaja idadi ya makampuni ya ndani na nje yaliyoomba kununua kifaa hicho.
Msemaji huyo, pia hakuweza kusema ni lini hasa mchakato wa ununuzi wa kifaa hicho utakamilika na rada hiyo kuendelea kufanya kazi kama awali.
Taarifa za kuzimwa kwa rada hiyo iliyonunuliwa katika mazingira tatanishi mwaka 2001 kutoka Kampuni ya BAE System, ziliifikia Tanzania Daima kupitia vyanzo vyake vya habari, takriban wiki mbili zilizopita.
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Margaret Munyagi, wiki iliyopita alikaririwa akithibitisha kuharibika kwa chombo hicho.
Alisema rada hiyo ilizima baada ya betri yake inayohifadhi na kutoa umeme wa dharura UPS pindi umeme unapokatika, kuharibika.
Hata hivyo, Munyagi, alisema tatizo hilo ni la kawaida na dogo na kwamba haliwezi kuathiri huduma za usafiri wa anga na shughuli nyingine uwanjani hapo.
Alisema mafundi wa TCAA, walikuwa wanaangalia uwezekano wa kununuliwa kwa kifaa hicho kutoka nje ya nchi haraka iwezekanavyo.
Ununuzi wa rada hiyo uliofanywa wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, ulipingwa vikali na wabunge wa Uingereza House of Commons na wa kambi ya upinzani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa madai kuwa gharama yake ilikuwa kubwa kuliko uwezo wake.
Pia walipinga kwa madai kuwa Tanzania ingeweza kununua rada ya bei ya chini zaidi ya hiyo ambayo ingeweza kukidhi mahitaji.
Wengine waliopinga ununuzi wa rada hiyo ni Benki ya Dunia (WB), Taasisi ya Fedha ya Kimataifa (IMF) na Shirika la Huduma za Usafiri wa Anga (ICAO), zikisema gharama yake haikuwa halali.
ICAO, iliwahi kusema wazi kuwa teknolojia iliyotumika kutengeneza rada hiyo ni ya zamani na ni ghali, na kwamba ingeweza kutumika kwa muda mfupi na isingefanikisha uongozaji wa ndege kwa maendeleo ya sekta ya utalii nchini.
Wabunge wa Uingereza walikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa kulikuwa na rushwa katika mchakato wa ununuzi wake.
Ofisi ya kuchunguza rushwa kubwa ya Uingereza, Serious Fraud Office (SFO), iligundua kuwa Kampuni ya BAE System, ililipa dola milioni 12 kwa mfanyabiashara Sailesh Vithlani, mzaliwa wa Mwanza, katika akaunti yake ya Uswisi.
Mfanyabiashara huyo ambaye sasa ni raia wa Uingereza, ndiye aliyekuwa wakala wa Serikali ya Tanzania katika ununuzi wa rada hiyo.
Makachero wa SFO waliifahamisha Serikali ya Tanzania kuhusu akaunti za Vithlani na uhusiano wake na BAE System na walimhoji mfanyabiashara huyo nchini, mbele ya maofisa wa Taasisi ya Kudhibiti na Kuchunguza Rushwa nchini (Takukuru).
Hata hivyo, Vithlani aliondoka nchini na baadaye, Takukuru ilipeleka kesi mahakamani Novemba 2007 na kutoa wito kuwa mfanyabiashara huyo, atafutwe.
Hapa nchini, kashfa ya rada imemgusa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, ambaye aliamua kujiuzulu nafasi yake baada ya kukabiliwa na tuhuma za kumiliki zaidi ya dola milioni moja za Marekani katika akaunti yake iliyopo Kisiwa cha Jersey, nchini Uingereza.
SFO bado inafanya uchunguzi kuhusu fedha za Chenge, kuangalia iwapo zina uhusiano na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada hiyo.
Wakati rada hiyo inanunuliwa, Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Wiki iliyopita, Mkurungezi wa Mashitaka nchini, (DPP), Eliezer Feleshi, alisema kesi hiyo bado iko mahakamani na mfanyabiashara Vithlani, anatafutwa.