Tujikumbushe vya zamani kidogo, vimepotelea wapi hivi?

Umeona ehhee..Hapo unaweza kuniteta wala nisishike hata moja..Sisi tulikuwa na ya kuongea Kinyume, pamoja na ya kuondoa herufi za mwisho na kuweka "psi"....Mapsi vipsi kapsi(mambo vipi kaka)

Dah aisee kweli kila zama na kitabu chake ,hili la kombolela bi mkubwa alinikataza kucheza sasa siku hiyo jioni namkuta sebuleni ,anaiuliza umetoka wapi nikamwambia kwa rafiki yangu kumbe nimetoka kucheza kombolela ,nlikua nimevaa converse all star sijui Siafu waliingia saa ngapi si ndio wakaanza kuning'ata ,bi mkubwa anashangaa natoa tu machozi kumbe navumilia balaa la siafu ,yule siafu nilimuua kwa nyundo kwa maumivu aliyonipa na kidogo aniumbue nimetoka kwenye kombolela
 

Ingependeza kama ungetumia picha ili tujikumbushe kwa uzuri zaidi
 

Hahaha...!!!
 
Enzi zetu kulikuwa na:

Nago
Mdako
Kipande
Ndiki (mpira wa miguu au netiboli)
Ukuti
Kidali
Gololi
Pia

Na mingineyo, kuikumbuka yote yataka wasaa.

Bi FaizaFoxy mimi naona miaka inavyozidi kwenda ndio utamu wa maisha unapungua,seriously.
 
Last edited by a moderator:

Hao fukufuku ni wadudu wanaopenda sana kujificha pembezoni mwa kuta za nyumba.....unamwimbia kwanza kabla hujamfukua
 
Mkuu kwa kweli tumetoka mbali sana mnacheza mpira wengne wanavua shati wanacheza vifua wazi hadi raha

Watakaoanza kufungwa ni sharti wavue mashati wabaki kifua wazi.
 
Hao fukufuku ni wadudu wanaopenda sana kujificha pembezoni mwa kuta za nyumba.....unamwimbia kwanza kabla hujamfukua

Hahaha unaimba fukufuku tokeaa...baba yako kaaja...kaleta donge la sukari!!!!
 
kuna hili songi nimekumbuka

Mungu mkubwa, bwa bwabwa na samaki, ki king majuto, to tone la maji, ji jitu la kale, le lenye midevu, vu vumbua dhahabu........Nimesahau linaendeleaje

Aisee... Nimezeeka
Wimbo waliouimba wanangu nao umeshakua wa zamani
 
-Panki
-Fidodido
-Kiparangoto
-kukata way


Umenikumbusha nilivyokuwa mdogo nilikuwa mwembamba sana mpaka nickname yangu ikawa Fidodido. Mpaka leo hii mama yangu mdogo ananiiita Fidido (sijui kwa nini hasemi Fidodido). Good memories.
 
Reactions: Art
Daah Mabumunda aise, alafu iyo doba ngumi dadeq, pale kitu kamgonoko ukiinama tu unapigwa teke la maana,Kitu kupapuana walah aise mwisho wa yote One touch iyo ndio funga kazi
 

Last month nilikua maeneo flani nikaona vjishimo vya fukufuku ikabidi niwatoe niangalie duh! nikajikuta nacheka mwenyewe kwakweli matoto ya sasa yamepitwa na vngi
 
Eti mvua ikinyesha na huku jua likiwa linawaka...eti Simba anazaa.

Kuna alishawahi kuhakikisha au kuthibitisha hiyo dhana.
 
Kibaba baba na kimama mama ndo nilikua napenda na nijlikuwa nafanya kweli ila kila nikifika home bi mkubwa anashtuka nachezea kichapo balaa
 
kuna hili songi nimekumbuka

Mungu mkubwa, bwa bwabwa na samaki, ki king majuto, to tone la maji, ji jitu la kale, le lenye midevu, vu vumbua dhahabu........Nimesahau linaendeleaje

vumbua dhahabu, bu bubu hasemi, mi mimi mdogo, go gogo la mti, ti tingisha mlango, kwingine nimesahau pia
 
Igizo ilikua la kina bishanga na rich rich enzi hzo
mkuu kina bishanga na rich rich ni wajuzi tu hawa,na kina wema wa enzi izo walikuwa kina waridi na aisha(black flani ivi amazing)mimi nakumbuka enzi za maigizo ya ITV kitambo icho tulianza na kina BOCHA na SUMBI hawa jamaa cjui ata wapogo wapi aisee!thn wakaja kina mzee jongo,halafu DTV walikuwa wanaigizo moja ivi la ZIMWI dah kitambo saaaana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…