Tujikumbushe wachezaji waliotamba AFCON miaka ya nyuma

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2015
Posts
1,479
Reaction score
3,788
Nafatilia Afcon ya mwaka huu inayofanyika Gabon, nimegundua Michuano imepoteza mvuto, haina msisimko kama zamani, viwanja ni vitupu, hakuna vikundi vya ushangiliaji kama ngoma nk ambao ni utamaduni wetu Afrika.

Leo hii Cameroon haina hata mchezaji staa anayejulikana, wengi wao wamekataa kuja kucheza michuano hii. Tofauti na zamani wachezaji walijitolea kuja kupambana kwa ajili ya mataifa yao, kama ni mpira ulipigwa mwingi sana tofauti na leo.

Tukumbushane timu na baadhi ya wachezaji waliosumbua Afcon za miaka ya nyuma kiasi cha kufanya michuano inoge sana.

Mimi naanza na hawa, Steven Appiah wa Ghana, Sunday Oliseh, Patrick Mboma, Sibosiso Zuma, Mohamed Aboutrika, Wael Gomaa, Amr Zaki, Khalilu Fadiga wa Senegal
 
Hapa nina uchungu na Uganda Cranes kupigwa 1 naisubiri gemu ya Mali na Egypt napenda waarabu wapigwe! Naomba uzi huu tupeane pia updates kwa tutaokuwa tunaangalia mechi inayotaka kuanza!
 
Mkuu kabumbu lilisakatwa zamani, siku hizi ni kubutua tu na kufanyabiashara.
Wazungu wametuulia vipaji hatuna ubavu tena wa kutoa vizazi kama hivyo.
 
Hapa nina uchungu na Uganda Cranes kupigwa 1 naisubiri gemu ya Mali na Egypt napenda waarabu wapigwe! Naomba uzi huu tupeane pia updates kwa tutaokuwa tunaangalia mechi inayotaka kuanza!
Sema dk za mwisho Uganda walimtafuta Ghana balaa
 
Nwanko KANU
Taribo west
Daniel amokachi
Uche ikwechuku
Celestine babayaro
Tijan babangida
Mustafa el haj
Patrick mbona
Henry camara
El haj diouf
Papaa bouba diop
"Vyuma" vilioitisha mpaka Brazil ya kina Dunga, mamaee


Uche Okechukwu
Rigbert Song
Ahmed Hassan Mido
Jay Jay Okocha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…