Utakumbuka kisa cha ajali ya ndege iliyotokea mwaka 1972 iliyoanguka Amerika ya Kusini kwenye milima ya barafu ya Andes iliyo Argentina na Chile, kati ya abiria na waendeshaji 50 wakiwemo wachezaji wa mpira wa Rugby kutoka Uruguay walitoka hai abiria 16 tu ambao walipatikana siku ya 72 tangu kutokea kwa ajali hiyo katika umbali na ukubwa wa maelfu ya kilometa za milima ya barafu iliyoungana.
Kipindi ajali inatokea abiria waliotoka hai walikuwa 27 lakini baadaye wengine wachache kupoteza maisha kwa majeraha na baridi kali na wengine 08 zaidi walikufa kwa kufunikwa na maporomoko ya barafu Avalanches.
Siku zote waliishi kwenye mabaki ya ndege hiyo wakiamini wangepatikana na kuokolewa lakini haikuwa hivyo kwani siku chache baadae waliishiwa mabaki ya chakula na kuanza kukata nyama za maiti na kula wakianza na mwili wa rubani.
Wachache walikataa mwanzo lakini baadae hali ilizidi kuwa mbaya na kujiunga kula ili kuongeza siku za kuishi.
Baadae moja aliruhusu mwili wa ndugu yake ukatwe na kuliwa.
Baada ya kuingia mwezi wa pili wawili kati yao walijitoa muhanga kutoka kutembea mamia ya kilometa wakipanda na kushuka milima ya barafu kwa kubahatisha huku wakiwa wamepakia vipande vya nyama ya maiti ili wasife njaa.
Walitembea safari ya kifo mkononi kwa muda wa siku 08 hadi walipoona mto na kuufuata kwa bahati nzuri walikuta mtu akiwa na farasi ng'ambo ya mto huo na kuwasiliana nae kwa kuandika ujumbe kwenye karatasi na kufunguka kwenye jiwe kisha kumrushia.
Hapo ikawa sababu ya kupona kwao na kuokoa wengine waliobaki kwenye tukio baada ya kusambaa habari kuna wahanga wa ajali hiyo wamepatikana hai.
Wanasema sababu ilikuwa ni uzembe wa marubani kujaribu kukatisha 'shortcut' kwenye milima hiyo na kujikuta katika milima iliyochomoza kuliko usawa wa ndege ilipokuwa inapaa na kugonga.
Ni moja katika ajali mbaya iliyosababishwa na makosa ya kibinadamu.