Ganda la ushuru
Senior Member
- Mar 18, 2020
- 132
- 112
ngoja niitazame na kusindikiza jumamosi yangu ki 'utulivu'
GLU™
GLU™
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu hiyo movie inaitwaje?Daa naikumbuka hiyo ajali niliiona documentary yake na movie pia. Yaani walikula kila kitu mpaka pombe zote na mwisho wakaanza Kula mpaka dawa za mswaki, na mwisho kuanza kula nyama za wenzao.
Nakumbuka mmoja wa abiria alimwambia rafiki yake “niahidi nikifa hutakula nyama yangu”
Bahati mbaya mmoja wapo alifariki
Hiki kisa kilinisikitisha sana kuzidi hata vita ya pili ambapo majeshi ya Japan walipokuwa wanawala wenzao baada ya kukosa chakula
Sent from my iPhone using Tapatalk
Mkuu hiyo movie inaitwaje?
Movie yake inaitwaje mkuu?
Sent from my iPhone using JamiiForums
Walipata wapi karatasi na peni?
Mpumbavu kabisa wewe Yani hili swali limeulizwa Mara kibao na wajinga watupu hebu someni post msituharibie Uzi.Mkuu hiyo movie inaitwaje?
Hii movie niliipenda maana walikua awahozi ndiyo maana walionusurika wakawa wanakula nyama zaoUtakumbuka kisa cha ajali ya ndege iliyotokea mwaka 1972 iliyoanguka Amerika ya Kusini kwenye milima ya barafu ya Andes iliyo Argentina na Chile, kati ya abiria na waendeshaji 50 wakiwemo wachezaji wa mpira wa Rugby kutoka Uruguay walitoka hai abiria 16 tu ambao walipatikana siku ya 72 tangu kutokea kwa ajali hiyo katika umbali na ukubwa wa maelfu ya kilometa za milima ya barafu iliyoungana.
Kipindi ajali inatokea abiria waliotoka hai walikuwa 27 lakini baadaye wengine wachache kupoteza maisha kwa majeraha na baridi kali na wengine 08 zaidi walikufa kwa kufunikwa na maporomoko ya barafu Avalanches.
Siku zote waliishi kwenye mabaki ya ndege hiyo wakiamini wangepatikana na kuokolewa lakini haikuwa hivyo kwani siku chache baadae waliishiwa mabaki ya chakula na kuanza kukata nyama za maiti na kula wakianza na mwili wa rubani.
Wachache walikataa mwanzo lakini baadae hali ilizidi kuwa mbaya na kujiunga kula ili kuongeza siku za kuishi.
Baadae moja aliruhusu mwili wa ndugu yake ukatwe na kuliwa.
Baada ya kuingia mwezi wa pili wawili kati yao walijitoa muhanga kutoka kutembea mamia ya kilometa wakipanda na kushuka milima ya barafu kwa kubahatisha huku wakiwa wamepakia vipande vya nyama ya maiti ili wasife njaa.
Walitembea safari ya kifo mkononi kwa muda wa siku 08 hadi walipoona mto na kuufuata kwa bahati nzuri walikuta mtu akiwa na farasi ng'ambo ya mto huo na kuwasiliana nae kwa kuandika ujumbe kwenye karatasi na kufunguka kwenye jiwe kisha kumrushia.
Hapo ikawa sababu ya kupona kwao na kuokoa wengine waliobaki kwenye tukio baada ya kusambaa habari kuna wahanga wa ajali hiyo wamepatikana hai.
Wanasema sababu ilikuwa ni uzembe wa marubani kujaribu kukatisha 'shortcut' kwenye milima hiyo na kujikuta katika milima iliyochomoza kuliko usawa wa ndege ilipokuwa inapaa na kugonga.
Ni moja katika ajali mbaya iliyosababishwa na makosa ya kibinadamu.