Tujikumbushe wana Azania

Mimi nilisoma AzaJangwa (Form I hadi Form VI) miaka ya 47, BANGI hazikuwepo kabisa enzi hizo. Nasikitika kusikia kuwa walikuja kuwepo wavuta Bangi. Namkumbuka Meja, Kisamo, Dathy, Mwl. Amos ( yeye alikuwa anashughulika na Miradi ya shule enzi hizo). ilikuwa raha tupu, mkimaliza la saba sel form zote za wavulana chaguo la kwanza AZANIA. Meja akiona shati tu wewe jisalimishe alikuwa anauwezo mkubwa sana huyu mzee na pia matani mengi hasa kwa rafikiye Mwl. Amos
 
Haya nyie wakina dogo , sie tulisoma Azania enzi za Joshua Mwambungu halafu akaja Bagenda na msaidizi wake marehemu Mnyamuru na meja alikuwepo pia enzi hizo!! Hakukuwa na wavuta bangi enzi zetu ; watu walikuwa wanapiga book tu ndio siri ya mafanikio yetu!!
 

Mkubwa ndo mwaka wangu huo mi nilikuwa IV- F na nilikuwa fine arts vile vile sitomsahau Mrope alivyotuincourage kuwa artists sema tatizo art hailipi ndio maana wengi hatukuendelea na art.Mr Kente umenikumbusha mbali ndugu yangu yule mzee amenifanya mpaka leo hii kuwa the best historian na sitomsahau alivyokuwa akitembea kila siku toka magomeni mpaka fire sijui alikuwa anasave nauli au anafanya mazoezi.Ukuta waliowekewa enzi zetu haukuwepo naona waliweka ila kudhibiti nidhamu.Ila kwenye matembe umenimaliza maana mimi nilikuwa memba mzuri tu pamoja na kina Zinjanthropas sijui kama unamkumbuka
 

Mkubwa pokea heshima yako maana bila nyie mliopita miaka mingi iliyopita Azania isingekuwa jinsi ilivyo.Anyway kila kizazi kinapita na madoido yake na wale tuliokuwa kipindi mageuzi yanaingia ndio tuliona fujo zote za uvutaji bangi wizi na mambo mengi ya ajabu lakini ilibidi akili kuwa kichwani ujue umefuata nini pale otherwise zero ilikuwa unakusubiri.
 

long live azania
 

Nakubaliana na wewe 100% you can be the person you want to be na masuala ya tuition yalikuwa hayakwepeki sababu wakati huo ndio Azania walimu waliongoza mgomo baridi kudai nyongeza ya mishahara ilifikia wakati unakaa darasani the whole week mwalimu hajatokea ilibidi tujichanganye na tuition tu vipi mzee Mkichwe wa Jangwani kuna wanaomkumbuka kwa tuition ya Physics.Anyway that experience made me able to survive in any part of the world now.
 
makitaja Azania sijui najisikiaje, mdogo wangu alimaliza pale 2003 ila hizo bangi anazopuliza ni balaa, na anasema walikuwa wanavuta hadi class

Pole dada yangu na kwa mdogo wako maana katika mjumuiko kuna mengi lakini ukweli unabaki wazi kuwa most of X-Azania they did well.Na kama ilitokea hivyo basi kulikuwa na matatizo katika ufuatiliaji especially katika familia maana katika jamii kuna wabaya na wazuri.Na ikitokea wa kwako akawa sio mzuri basi ni vizuri kumtizama yeye zaidi kuliko kuiangalia vibaya Azania yetu
 

Nyati, hizo ndo enzi nlizokuwepo, ingawa Baada ya Muda Mr. Kwayu akampokea Kisamo, huyo Kisamo alikuwa katili kweli siku moja nusura amtoe kichwa kijana mmoja baada ya kumlenga na Fyekeo (Kwanja) kule jikoni baada ya kijana kuwa nje ya mstari.

Azania ilikuwa cool sana, mambo ya mibangi tuliwaachia Tambaza ingawa kulikuwa na vijana walioshirikiana na wale wa Tambaza waliounda kundi la Barcelona, Azania ilikuwa shule tu, intake yetu ndo ilikuwa ya kwanza kuzindua ule mpango wa double session (zamu za kuingia asubuhi na mchana) Baadhi ya waalimu walikuwa hawa:-

Mwl. Kisamo (H/ Master)
Mwl. Meja (Assitant H/M) baadaye alihamia Same Secondary
Mwl. Amos, baadaye alipelekwa Wizarani
Mama Semguruka (Nidhamu) Sikumbuki jiana sawasawa ila alikuwa teacher wa Kiswahili na alikuwa safi sana kwenye maonyo.
Mwl. Mashanga (aliongozaga mgomo wa kwanza wa Waalimu enzi za Mzee Ruksa)
Mwl. Bulemo

Baadhi ya Wachezaji maarufu wa Azania enzi hizo walikua:-
Robert Mwampemwa aka Vimvi (baada alikuja kuwa cartoonist mzuri kwenye magazeti, sijui yuko api sasa)
Sasi
Lucky
Cecil (huyu alikuwa full back left mnene lakini mwepesi sana)
Edward Mpandang'ong'o (Ball dancer)

Geofey Nyange (KAburu) M/ Mwenyekiti wa Simba pia alikuwepo wakati huo yuko A' level mimi niko O'Level.
 
AZABOYS!! mi nilikuwa hapo 1994 - 1997 enzi za kwanyu na Mchwampaka!! enzi hizo Mchwampaka anamuita KWAYU KAKA!! . Kwenye Mihoga kuna jaamaa anaitwa nyuki!!!! enzi hizo wakina Mcheni wanandoto za kwenda SOUTH wakaishia Jela huko!!! wimbo wa AZANIA AZANIA!!! Ezi za kina COOL SOUP!!! WAKINA BATMAN waanzilishi wa vita ya AZANIA NA TAMBANZA!!! Enzi zile ukila chips unaitwa Bishoo!!!
 

Zinja namkumbuka, F mlikua na makundi mawili mnapambana kweli mamluki na nimesahau lile jingine ( nafikiri wafarisayo not sure) wakina Spoiler, Kwame na yule monita wenu form 2 mlikua mnamtania kiuno, LOL. nakumbuka skonz za brake tukiwa tunaingia asubuhi si mchezo washkaji wa F walitokomea na skonz za darasa zima ilikua balaa, unamkumbuka yule mkorea alikuja kusoma azania ikawa balaa kila siku ilikua kukimbizana na kutoa kichapo? Goodluck alimchokoza siku moja basi ilikua balaa. Alafu kuna ticha mmoja tulikua tunamwita kicheche LOL. ila nilikua nampenda mwalimu isaya wa hesabu alikua makini sana. I really enjoyed Azania.
 

Mkuu kabla ya hapo kulikua na biff kati ya Tambaza na Azania around 91-92, wakati huo kulikua na kikundi kinaitwa Barcelona na jamaa mmoja alikua anaitwa Puza RIP. baada ya kauhasama flani tukawa shwari na Tambaza baada ya kuwachapa kwenye mechi moja ilifanyika pale kwetu. Azania kulikua na vichwa kwelikweli.
 
 
Teh teh teh this so funny!!!!!!!!! sasa mbona hamjaongelea ile juice pale kwa mkemia na mihogo manake ndio yalikuwa maisha yetu pale Azaboy kasoro mabishoo na watoto wa mama (matajiri)wachache waliokuwa wanakula chips
 

Huyu Mwampembwa yuko juu anafanya kazi Nation ya Kenya anaendeleza kuchora Katuni kuna wakati alipata tuzo ya CNN.
Katika wachezaji umemsahau Jamaa anaitwa Hamisi, yeye bahati mbaya alifariki miaka ya mwishoni mwa 1999 / ama 2000 hivi alikuwa mchezaji wa hail ya juu.
Mpandang'on'go alikuwa mzuri pia. sijui yupo wapi siku hizi?
Wauza mihogo waliendelea kuwepo pale muda mrefu na wanakumbukumbu kweli nikipita pale wananisalimia ingawa sikuwa maarufu pale Azania. Vile vile wana "intergrate" vizuri kuna wakati kulitokea msiba katika familia ya Mwalimu mmoja pale, katika mazishi ( Kinondoni) niliwaona wakishiriki - miaka miwili mitatu iliyopita

Enzi zile wasichana wa Jangwani wakituita NATO ( No Action Talking Only)
 

Hata wewe Bulesi bado dogo saana. Sisi ndio vikongwe wakati Headmaster alikuwa Mr. K.R. Jones(British), halafu akaja Mr. Abdirahaman Mwalongo (mjalukolo) akafuatwa Joshua Mwambungu (mwanafiale).

Enzi hizo tulipiga kitabu kama vile hatuna akili nzuri na mitihani ya University of Cambridge kwa ajili ya Form 4 na 6 ilitukoma. Kwa taarifa yako Gavana/Professor Benno Ndulu ni product ya Azania enzi hizo. Vijana walikuwa hawachakachu vitabu bali walikuwa nyomi kwa sana.
 



I like this when I see the real people who made Azania the way it is cause without you guys there wouldnt be any respect in our school, that time every talented boy s dream was Azania.And not these days the boys are just competing in smoking Marijuana shameful
 
 
 
inasikitisha kuona aliyekuwa mvuta bangi na fegi darasani ... mpaka leo hii mnamsifia ... :confused2:
 
inasikitisha kuona aliyekuwa mvuta bangi na fegi darasani ... mpaka leo hii mnamsifia ... :confused2:



Mjomba wewe wa wapi lakini maana unarukia topic bila kuzielewa.Kule kwa wazanzibari umejidai kuchokoza umenikimbia sasa na huku tena na kwa taarifa tu huyu tunayemsema alikuwa mwalimu wetu na sio mwanafunzi kama unavyofikiri wewe na alikuwa havuti bangi elewa mjomba hapa watu unaoongea nao si kama unavyofikiria wale wa skuli ya kiembe samaki.Hapa ni vichwa makini toka Azania boys
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…