Mimi nilisoma AzaJangwa (Form I hadi Form VI) miaka ya 47, BANGI hazikuwepo kabisa enzi hizo. Nasikitika kusikia kuwa walikuja kuwepo wavuta Bangi. Namkumbuka Meja, Kisamo, Dathy, Mwl. Amos ( yeye alikuwa anashughulika na Miradi ya shule enzi hizo). ilikuwa raha tupu, mkimaliza la saba sel form zote za wavulana chaguo la kwanza AZANIA. Meja akiona shati tu wewe jisalimishe alikuwa anauwezo mkubwa sana huyu mzee na pia matani mengi hasa kwa rafikiye Mwl. Amos
Nyati, hizo ndo enzi nlizokuwepo, ingawa Baada ya Muda Mr. Kwayu akampokea Kisamo, huyo Kisamo alikuwa katili kweli siku moja nusura amtoe kichwa kijana mmoja baada ya kumlenga na Fyekeo (Kwanja) kule jikoni baada ya kijana kuwa nje ya mstari.
Azania ilikuwa cool sana, mambo ya mibangi tuliwaachia Tambaza ingawa kulikuwa na vijana walioshirikiana na wale wa Tambaza waliounda kundi la Barcelona, Azania ilikuwa shule tu, intake yetu ndo ilikuwa ya kwanza kuzindua ule mpango wa double session (zamu za kuingia asubuhi na mchana) Baadhi ya waalimu walikuwa hawa:-
Mwl. Kisamo (H/ Master)
Mwl. Meja (Assitant H/M) baadaye alihamia Same Secondary
Mwl. Amos, baadaye alipelekwa Wizarani
Mama Semguruka (Nidhamu) Sikumbuki jiana sawasawa ila alikuwa teacher wa Kiswahili na alikuwa safi sana kwenye maonyo.
Mwl. Mashanga (aliongozaga mgomo wa kwanza wa Waalimu enzi za Mzee Ruksa)
Mwl. Bulemo
Baadhi ya Wachezaji maarufu wa Azania enzi hizo walikua:-
Robert Mwampemwa aka Vimvi (baada alikuja kuwa cartoonist mzuri kwenye magazeti, sijui yuko api sasa)
Sasi
Lucky
Cecil (huyu alikuwa full back left mnene lakini mwepesi sana)
Edward Mpandang'ong'o (Ball dancer)
Geofey Nyange (KAburu) M/ Mwenyekiti wa Simba pia alikuwepo wakati huo yuko A' level mimi niko O'Level.