Azania imechanganyika na mademu? Hii kweli balaa! Yani hamna hata fleva tena ya chama letu!! Mimi nakumbuka kiunganishi mashuhuri cha mwalimu Mitimingi hasa, akiongea kiingereza. Badala ya kusema kiufasaha 'another thing' alikuwa akitumia sana neno 'anaza sing' , basi kwetu ikawa kila akija skuli balaza inakuwa tunamwita anaza sing.
Halafu kulikuwa na nunda fulani pale shule linaitwa "batman", sijui bado lipo maana nakumbuka kuna siku lilimzaba Mchwa bonge la kofi kwenye school baraza.I wonder litakuwa lina shughuli gani siku hizi.
Mwalimu Kijazi wa Biolojia sijui bado yuko au vipi. NIlikuwa nammaindi sana, sema basi tu!
Mwalimu Dathi yule mhindi, sijui bado yuko hai, alikuwa mzuri sana wa Chemistry. NIkimuona tena lazima nimpe zawadi.
"Azania, Azania, Azania our school, we look at you with pride, you are known far and wide, you are always our best, we will never forget you",
Wana wa Azania mnakumbuka hii school anthem??
BIla kumsahau Mheshimiwa sana, mwalimu Kente mzee wa Mabuga!!