Ahaa Kweli hiyo stori ya Mchwa-Mpaka ilikuwepo tehe tehe tehe
Huyu alikuwa discipiline master matata sana kipindi chake ,alikuwa na kigugumizi pia bigwa wa reverse stori zake ukihadithiwa unaweza kudhani ni za kubuni ila ni amini na kweli maana alinifundisha Geoghaphy.Ilikuwa akimwita head master wa Azania enzi hizo Mr.Kwayu kaka!.
Habari yake nyingine nayokumbuka ni baada mechi ya mpira kuisha jioni kunako Pugu na giza ukingia alimkimbizwa na kuchapa bakora sana ila cha ajabu hakuhadithia kesho yake alibaki kumsifia kipa wetu kuwa "alikuwa anapiga mpira kisha anadoka huku akionyesha kudaka ndio kupiga na kupiga ndio kudaka" alikuwa bigwa wa reverse hakika.
Namkumbuka Mwl.Mkongo alikuwa safi sana,kulikuwepo na walimu walevi kama Mushi wa Physcics,.........kulikuweko na Huyu aliyekuwa anaitwa primus ,na Tokyo kwa kupenda kuvaa suruali za chata la tokyo ahaaaaaaaaa.Kulikuwepo na Hatibu nadhani huyu alikuwa anapenda sana michezo.Tulikuwa na mama huyu wa kihindi (Dhasi)alikuwa mzuri sana kwenye chemistry bila kusahau mama Shija mzuri mno kwenye chemistry alikuwa akifundisha A'level.Kulikuwa na mama kiarabu pia akifundisha Math.
Kuna yeyote anakumbuka maneno haya
msuli kitanda,msuli tamaa,sodoma ,gomora,masaki,mirembe
Nakumbuka kipindi chetu tulikuwa na umoja sana pale,we have a lot of funy things also kuna watu nimewakumbuka sijuhi wako hapi kuna haja kutafutana .