Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Na hii ndio taarifa ya habari kutoka Redio Tanzania Dar es Salaam na msomaji ni David Wakati. Kwanza habari kwa ufupi. Rais Nyerere amemstaafisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo nchini NDC ( hamna hii kitu siku hizi jamaa ni muoga ile mbaya!!! hajiamini hata kidogo hata mtu akivurunda vipi ataunda tume lakini yeye hahusiki!!!!? niliwahi kusikia katika mazungumzo ya wakubwa nyakati hizo huyu David Wakati alikuwa hasomi taarifa za habari mara kwa mara na siku alizokuwa akifanya hivyo basi ni lazima kulikuwa na habari nzito sana.
 
Yuko wapi Chrisanta Kulaya aliyekuwa akitangaza kipindi cha Kahawa ni Mali RTD enzi zile? Nakumbuka utulivu na umakini wake akiendesha kipindi kile na kiswahili chenye lahaja ya kichaga.
 
DOMINICK CHILAMBO - Kanda ya ziwa, kumbuka alivyokuwa akitangaza mpira Pamba maybe na simba/yanga au malindi ya zanzibar, utapenda utadhani na wewe uko uwanjani
Siku hizi sipendi hata kusikiliza mpira unaotangazwa redioni hauna mvuto kabisa

Ahmed Jongo - Arusha
 
Majira duh kipindi poa sana hivi bado kipo,MAMA NA MWANA,MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI,VIFO,MICHEZO ,KIBUKU,SALAAM etc
 
habari wadau wa JF, sahau kuhusu TBC taifa ambayo imepoteza dira siku hizi, unakumbuka kitu gani iwe kuhusu watangazaji au vipindi vyao enzi hizo, redio tanzania (RTD) haina upinzani!
 
me binafsi nilikuwa napenda sana matangazo ya mpira wa miguu, watangazaji akina halima mchuka (r.i.p)
sued mwinyi, juma nkamia
 
me binafsi nilikuwa napenda sana matangazo ya mpira wa miguu, watangazaji akina halima mchuka (r.i.p)
sued mwinyi, juma nkamia


mbona una msahau Ezekiel Malongo
kwenye kipind cha michezo 1:30 jion kama sikosei
 
Enzi za Mafundi Mitambo kama. 1 Juma kengere 2 Noel Namalowe 3 Ally Said Tunku 4 Kayanda. 5 Jakob Ayimba 6 Konsalva Mweleke nk
 
komboraaaaaa!hiki kilikua kipindi cha alfajiri kikiwa na miziki kabambe,kikifuatiwa na taarifa ya habari na kisha kipindi cha majira!
 
Me nakumbuka mwaka 1996 na 1997 nilikuwa darasa la 1 na 97 nilikuwa darasa la 2, kulikuwa na kipind kinaitwa SAA TANO WAKATI WA KAZI basi ndo ilikuwa saa yangu yakuanza kuna kwenda mixer bi mkubwa kunikumbusha "wewe saa tano hiyo kaanze kuna uende shule" nilikuwa napata moto coz nilikuwa nimenogewa michezo!
 
Me nakumbuka mwaka 1996 na 1997 nilikuwa darasa la 1 na 97 nilikuwa darasa la 2, kulikuwa na kipind kinaitwa SAA TANO WAKATI WA KAZI basi ndo ilikuwa saa yangu yakuanza kuna kwenda mixer bi mkubwa kunikumbusha "wewe saa tano hiyo kaanze kuna uende shule" nilikuwa napata moto coz nilikuwa nimenogewa michezo!
Khaa!kumbe humu ndani kuna vitoto vingi namna hii lol!!
 
Namkumbuka sana Ahmed Jongo, Ben Kiko, Malima Ndelema, Richard Leo, Salim Mbonde, et al. By that time RTD ilivutia sana.
 
Kwa upande wa vipindi nilipenda sana Chaguo la msikilizaji j3 hadi ij sa8 mchana, mama na mwana j1 sa9 alasiri, Salaam za wagonjwa j2 sa4 asubuhi, Igizo la Twende na wakati wakiwemo kina Kidawa j4 sa3 usiku.
 
Mchezo wa radio wenye maadili ya kutosha saa 2:30 usiku kama sikosei hivi!
TWENDE NA WAKATI mixer ka mdundo fulani hivi nduuu! nduuuu! nduuu!
nilikuwa skai mbali na radio ya mkuliwa
NATIONAL!
 
Back
Top Bottom