Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Nikiripoti kutoka Iringa , Chisunga Steven kanda ya kusini.
 
...nikiripoti kutona Nyanda za juu kusini, Nswima Ernest wa Redio Tanzania.......halafu hapo umemsahau....tunawaletea tumbuizo asilia....Malima Nderema...
 
Kutoka hapa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam niliyewatangazieni mpambano huu katika ya Simba ya Dar na Majimaji ya Songea ni mimi sports lady wako HALIMA MCHUKA
 
Nakumbuka kipindi vya Pwagu na pwaguzi cha Batholomeo Milulu na Rajab Hatia, Kipindi vya maigizo vya mzee Jongo, mama Haambiliki, Zena Dilip, Mazungumzo baada ya habari, mziki wa kuanza kipindi cha matangazo ya vifo, kipinidi cha zilipendwa chini ya Mohamed Besta ... ya kale ni dhahabu
 
Umenikumbusha mbali sana, naongezea kidogo vp kuhusu mafundi mitambo? kama EDMUND MLIYA n.k
 
Wengi kati ya hao uliowataja sasa ni marehemu: Salama Mfamao, Bati Kombwa, Omary Jongo, Dominic Chilambo, Michael Katembo, Khalid Ponera. Nadhir Mayoka. Wengine ambao hukuwataja lakini walishatangulia mbele ya haki ni pamoja na Abdul Omar Masoud, Leonard Mtawa, Juma Ngondaye, Michael Hendrich Libuda, Karim Besta, na wengine wengi.
 
Tufurahi jama tufurahi wiki endie............................................. ..... Baba naomba ruhusa niende wiki endi niende nikafurahi na wana milimanieee. Asante sana mwanangu kwa ombi lako siku kwa siku za wiki endi ni siku ya furaha mwanangu.

Uwiii inanikumbusha mambali kweli.
 
Last edited by a moderator:
Sina uhakika kama wameshatajwa hawa watu,

Kassim Mikongolo
Salum Mbonde
Zainabu Bongii,
Martha Ngwira,
Resistuta Bukoli - Shinyanga


Mafundi mitambo

Fundi Juma Kengele
James Muhilu,
Noel Namalowe
Crispin Lugongo
Saidi Tunku
Abdallah Mkosolwa

Maderva gari la utangazaji na OB Van

Abdallah Mgeni
Saidi Njiwa
 
Uncle J, Julia Nyeisanga na Misakato pamoja na Club raha leo show
 
Mzee Paul Sozigwa - Mazungumzo baada ya habari
Marehemu Abdul Omar Masudi 'Mjawa'
Maria Ulimwengu
Betty Mkwasa
 
Back
Top Bottom