Mi nakumbuka taarifa ya habari ikianza tu ile kusikia sauti ya mtangazaji tunaanza kukisia jina lake kabla hajajitambulisha. Yaani ilikuwa kama mchezo fulani hivi burudani tupu enzi hizo.
watoto wadogo tulikuwa tumekariri ratiba ya redio tanzania karibu ya wiki nzima!!huulizi kuwa ikitoka taarifa ya habari inakuja nini?? unajua tu ni mazungumzo baada ya habari(taarifa ya habari ya saa mbili usiku)!!maneno hayo,ilikuwa ni kabla au baada ya kipindi cha michezo,sikumbuki vizuri!!Mazungumzo baada ya habari ilikuwa ni mpaka ufikirie kidogo kwa muda ndo utaelewa anazungumza nini......................!!dah i liked those moment,we cherished