LE GAGNANT
JF-Expert Member
- Jan 20, 2011
- 1,241
- 252
Charles hilary na mambo mpwitompwito
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nakumbuka enzi hizo kipindi cha mama na mwana cha Debora Mwenda watoto tulikuwa hatukosi. nakumbuka Jumamosi mchana wakati kipindi kipo hewani watoto mmejikusanya wenyewe kwenye radio mbao yenu kunasa hadithi (ua jekundu) ili jumatatu ukaisimulie darasani.
Watoto wa siku hizi sijui hata kama huwa wanasimuliana hadithi huko mashuleni jamani.
Hivi wakulu, Florian Kaiza na Suleiman Kumchaya pia wapo au wamestaafu kazi?
.
Take a break, na tujikumbushe enzi zile za RTD, ambapo kulikuwa hakuna FMs rado kama sasa. Hakika kulikuwa na watangazaji, vipindi bomba na hata nyimbo za kutambulisha vipindi zilikuwa makini sana. Hebu ngoja niwakumbushe baadhi ya watangazaji wa wakati huo.
1. Nassoro Nsekeli- alikuwa na sauti kama ya mafua hivi alikuwa mtaalamu wa kipindi cha Majira- ndiye aliyetangaza kifo cha Nico Zengekala
2. Bujago Izengo wa Kadago- Kibesi chake kilikuwa safi sana
3. David Wakati (DG) - kipindi cha Nipe habari- Kwaherini wote, mungu awalinde na mmbaki salama, mungu akipenda..............
4, Khalid Ponera- Zilipendwa
5. Ahmed Kipozi- taarifa ya habari
6. Hassan Mkumba- matangazo ya vifo
7. Siwatu Luwanda
8. Salama Mfamao
9. Mohamed Amani (Mohamed Dahman)
10. Salim Seif Nkamba
12. CHisunga Steven- kipindi cha Ugua pole duu
13. Bathoromeo KOmbwa (bati Kombwa) - WAkati wa Kazi
14. Ahmed Jongo- Mpira
15. Christina Chokunogela
16. Dominic Chilambo- Mpira
17. Edda Sanga
18. Debora Mwenda- Mama na Mwana
19. Aloycea Maneno- Ombi lako, cheichei Shangazi, mama na mwana
Duu nawamiss sana hawa watu tofauti na watangazaji wa sasa
hivi hii imekumbukwa kweli kuwekwa kwenye historia? Nasoma mara nyingi ya alipandisha bendera juu ya mlima tu.Hamza kasongo - alitangaza uhuru wa Tanganyika, 1961. Sasa ana kipindi channel 10?
Amestaafu mwaka jana yupo nymbani kwake Msewe anakula bataBaada ya kumaliza na ngwe ya Sumaye kama Press Sec.wake, alirudishwa Maelezo briefly, then amepelekwa wizara ya Habari, nadhari kusubiri kustaafu kwa heshima.
Jamani hivi Jacob Tesha yuko wapi? ukitaka kusikia "bass" ya kufurahisha basi ulikuwa unatakiwa usikilize taarifa za habari.