Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Aiondoka RTD 1995 akajiunga na Channel Ten, yeye, Kipozi, Bujaga na Betty Mkwasa chini ya bosi Godfrey Mngondo.
1999 Besta na Bujaga wakatimkia Aboud TV Morogoro, Betty na Kipozi wakajiunga ITV.
Mpaka sasa, Bujaga yuko Sokoine TV, Kipozi anajitegemea, Betty kaula U=DC na
2007 Besta alitangulia mbele ya Haki.
RIP Karim Besta.

N.B Karim Besta, alisoma Tambaza miaka ile ya 80's enzi za Tambaza, Tambaza kweli!.
mmmh sikuwa na taarifa hii, thanks for info
mix with yours
 
BILA KUMSAHAU SAMADU HASSAN na Mzee PAUL SOZIGWA nadhani hawa pia walikuwa RTD au nimekosea?

BILA SHAKA SAUTI ILIYOKUWA INAVUMA KWA USOMAJI WA HABARI ILIKUWA NI YA ABAS KIHEMBA hivi yuko wapi huyu muzee? nadhani sauti yake inaweza fananishwa na ya ALI SALEH wa BBC
 
Pia viashiria vya kuanza vipindi vilikuwa vimetulia sana; mfano kipindi cha Ombi Lako, Mchana Mwema, Nipe Habari(ingawa wakati huo nilikuwa sipendi ..kama Gospel hivi), Jibu Lako, kulikuwa na Mikingamo, Kumekucha etc.......enzi hakuna EPA, Ukimwi, Udini, Mauaji ya Albino (ya uwazi) etc .............
 
Wakurugenzi wa RTD je?
  1. David Wakati
  2. Ngw'nakilala
  3. nani vile?
  4. Edda Sanga
  5. Mshana
 
JULIUS NYAISANGA 'UNCLE J' - Misakato
BETTY CHALAMILA baadaye BETTY MKWASA
FAUZIAT ABOOD
IDRISA SADDALA-Nyanda za Juu Kusini

Bila kumsahau Mzee wa 'kuegzagireti' BEN KIKO.
 
  • Salim Mbonde
  • Juma Ngamia
  • Halima Mchuka
  • Bujaga Izengo Kadago
  • Ahmed Jongo
  • Dominic Chilambo
 
Mie hawa walikuwa wananikosha kinoma kwa utangazaji wa mahiri....


15. Christina Chokunogela

16. Dominic Chilambo- Mpira

17. Edda Sanga
18. Debora Mwenda- Mama na Mwana
19. Aloycea Maneno- Ombi lako, cheichei Shangazi..
 
Kuna mtangazaji alikuwa anaitwa Frank Kirumbi. Alitangaza kidogo miaka ya 80 mwanzoni. Aliishia wapi?
 
Jacob Tesha, alipokuwa akisoma habari nilikuw nageuka kumtazama Baba. Sauti nzito. Debora Mwenda enzi za Mama na Mwana, hadithi ya Ua jekundu na Binti Chura. Ah! Watu wamesahau Adili na Nduguze. Saa nane na dakika 2 kila jumapili. Acha tu, wakati huo Nyerere alikuwa hai.
 
Duh wakuu nimekumbuka enzi hizo tunasikiliza kipindi cha jioni njema.
 
Issue haikua watangazaji tu,,hata redio zenyewe,,,kwetu sisi kulikua na Panasonic fulani acha kabisa,,
 
Tumbuizo asilia na Michael Katembo.
Lazima nisikilize sana mijigoma ya kienyeji enzi hizo za UJAMAA NA KUJITEGEMEA
 
Tunawaenzi vipi watangazaji hawa?
take a break, na tujikumbushe enzi zile za rtd, ambapo kulikuwa hakuna fms rado kama sasa. Hakika kulikuwa na watangazaji, vipindi bomba na hata nyimbo za kutambulisha vipindi zilikuwa makini sana. Hebu ngoja niwakumbushe baadhi ya watangazaji wa wakati huo.

1. Nassoro nsekeli- alikuwa na sauti kama ya mafua hivi alikuwa mtaalamu wa kipindi cha majira- ndiye aliyetangaza kifo cha nico zengekala

2. Bujago izengo wa kadago- kibesi chake kilikuwa safi sana

3. David wakati (dg) - kipindi cha nipe habari- kwaherini wote, mungu awalinde na mmbaki salama, mungu akipenda..............

4, khalid ponera- zilipendwa

5. Ahmed kipozi- taarifa ya habari

6. Hassan mkumba- matangazo ya vifo

7. Siwatu luwanda

8. Salama mfamao
9. Mohamed amani (mohamed dahman)

10. Salim seif nkamba

12. Chisunga steven- kipindi cha ugua pole duu

13. Bathoromeo kombwa (bati kombwa) - wakati wa kazi

14. Ahmed jongo- mpira

15. Christina chokunogela

16. Dominic chilambo- mpira

17. Edda sanga
18. Debora mwenda- mama na mwana
19. Aloycea maneno- ombi lako, cheichei shangazi, mama na mwana

duu nawamiss sana hawa watu tofauti na watangazaji wa sasa
 
Back
Top Bottom