Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV


duuh...kweli wakati ni ukuta! Siku hizi watangazaji utawasikia tutumie maoni yako kupitia facebook page yetu
 
Sekeoni Kitojo
Jackob Tesha
Halima Kihemba
Julius Nyaisanga
David wakati
Ni baadhi ya watangazaji niliyowapenda.
Vipindi kama "Club raha leo show"
"Wakati wa kazi"
"Mazungumzo baada ya habari"
Ni vipindi ninavyovikumbuka .
Nyimbo kama :
"Geza ulole, twendeni Kigubumo na Mwanadilatu kwenye makao mapya" (UDA JAZZ wana BAYANKATA)
"Zuwena na ajali ya salender" (DAR INTERNATIONAL)
Bendi za URAFIKI (KWA NGULI WA NGULIMBA)
BIMA LEE (JARY NATION DUDUMIZI)
MSONDO NGOMA AU JUWATA
Ni bendi nizikumbukazo sana.
 
Michezo ya kuigiza ilikuwa: Wema Hauozi, Mkataa Pema Pabaya Panamwita, Mapenzi Kitovu cha Uzembe. Tulikuwa tunasikiliza, familia yote tukiwa pamoja na pengine hata majirani maana si kila familia ilikuwa na uwezo wa kumiliki redio. Michezo haikuleta ukakasi wa masikio, ilikuwa na maadili. Tulielimika na tuliburudishwa kupitia RTD. Rip RTD. Nitakukumbuka daima.
 
habari wadau wa JF, sahau kuhusu TBC taifa ambayo imepoteza dira siku hizi, unakumbuka kitu gani iwe kuhusu watangazaji au vipindi vyao enzi hizo, redio tanzania (RTD) haina upinzani!

Club Raha Leo show (Jmosi mchana-miziki live na kujua wanamuziki na nafasi zao ktk bendi). Mkulima wa Kisasa-kipindi cha kilimo!
 

Unakumbuka wimbo wa wadhamini wa michezo hiyo? kipindi fulani ilikuwa "Kibuku"..
...Utumie Kibukuu ni pombe boraa...,
...tumia kibuku ni pombe boraa..*2
 

kweli kabisa R.I.P rtd
 
Mama na mwana nadhani host alikua Eddah Sanga au Deborah Mwenda, zile hadithi za Ua Jekundu nilikua sizikosi...
Kipindi cha wakati wa kazi nacho kilikua burudani.
 
habari wadau wa JF, sahau kuhusu TBC taifa ambayo imepoteza dira siku hizi, unakumbuka kitu gani iwe kuhusu watangazaji au vipindi vyao enzi hizo, redio tanzania (RTD) haina upinzani!

Kipindi cha wakati wa kazi (mahojiano na wafanyakazi wakiwa kazini),
Ukumbi wa kinamama,
Mwito kwa waalimu,
From me to you kwenye 'RTD external service'.
 

Maamuma umenikuna umenikumbusha mbali sana...usisahau mama na mwana na hadithi ya Mbalamwezi nyota Begani it was 1981,82 hii hadithi ili futa watoto wengi sana wa enzi zile...RTD nitakukumbuka huku moyo unauma...
 
....mwaka 93 kama sikosei... Gulamali akiwa Rahisi wa YANGA...
RTD ilitangaza final game ..Afrika Mashariki na Kati"... YANGA walishinda... Cant forget this...
 
....mwaka 93 kama sikosei... Gulamali akiwa Rahisi wa YANGA...
RTD ilitangaza final game ..Afrika Mashariki na Kati"... YANGA walishinda... Cant forget this...

nakumbuka marehemu pepe kale ndipo alipowatungia nyimbo yanga mara baada ya kuchukua ubingwa ule.
 
Mimi namkumbuka christian katembo.ngoma za kwetu anaingia studio na manyanga na akianza kutaja jina lake utasikia mnyama tembo,na ndugu zake komba,mbawala,mapunda wapo studio leo! Na anaongea kwa lugha za makabila yote yaan unataman kipindi kiwe kila siku
 
nakumbuka kipindi cha watoto shangazi alikua anasimulia hadithi za abunuwasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…