Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mama na Mwana,
Huyu jamaa hata kama mko na mambo yenu mlikuwa mnalazimika kuacha na kumsikiliza , ole wao watoto wapige kelele wakati Tesha ananguruma!
me too, kumbe utoto sio mbali 25 yrs back naona niko pembeni ya redio baada ya mama na mwana mpira........
Where is Salama Mfamao??
U see may be we can always love our country kwa kukumbushana enzi hizo,,,,,...sio leo!
Yap huyo alikuwa anaitwa Benjamini Kikorongo (BENKIKO)
Wengi wametajwa mbona wafuatao hamjawatendea haki? Wapi Suleiman Hegga wapi Suleiman Kumchaya wapi Suleiman Muhogora .... Ongezeni
Jacob Tesha, alipokuwa akisoma habari nilikuw nageuka kumtazama Baba. Sauti nzito. Debora Mwenda enzi za Mama na Mwana, hadithi ya Ua jekundu na Binti Chura. Ah! Watu wamesahau Adili na Nduguze. Saa nane na dakika 2 kila jumapili. Acha tu, wakati huo Nyerere alikuwa hai.
Nikipindi cha pili cha pili hapa wao sifuri sisi moja na utamsikia tukifungwa timu ya taifa alikuwa hata hasemi goooooooooooo utasikia washatufunga. namna gani hapa jamaa alitakiwa kutumia hata ulimi kuweka ule mpira kimiani. Ahmedi Kampira na mpira lalalalalalalalalaaaaa ah namna gani Juma Mgunda anashindwa kuona milingoti mitatu hapa.
Kwenye maguu kumi nane ana weka mpira ule Edward Chumila na na simba wanafanya mabadiliko namuona kocha mchezaji anaingia hapa heeeee he Chumila kwa guu lake la kushoto anapiga mpira ule anaingiza majalo moja pale ile inaitwa banana chop gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo a namna gani hapa mpira unagonga mtambaaaaa panya wasikilizaji ..................... nikikumbuka enzi hizo sipati jibu
safi sana Mkuu - memory nzuri - tumewakumbuka wengi sababu wakati huo Radio ilikuwa moja tu - mi nilipenda kipindi cha michezo - mbili kasoro robo na majira saa tatu na jambo asubuhi----
Sikonge kuna wimbo huu nafikiri utaukumbuka
--- kumekuchaa jamaa kumekuchaaa ----majogoo vijijini wanawikaa----wananchi amkeni tufanye kazi sasaaa......tusonge mbeleee - tosonge mbeleee
Nikisikia unapigwa basi najua tayari kumekucha kweli - kujiandaa kwenda shule....Hapa nakumbuka ujamaa ujamaa vile duh.
Bila kumsahau fundi mitambo Domitila Urassa (RIP)