Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Mahokaaaaa We mama mbavu zangu weeee we mama mbavu zangu weeee we mama mbavu zangu weee ha ha ha haaaaaaaaaa! Duh noma hapo jumapili napiga pasi uniform kwa ajili ya jumatatu pasi ni ya mkaa kama ya dobi mara mkaa au jivu linadondokea kwenye shati jeupe unaanza kufua kola upya enzi hizo electric iron ni luxurious item!
 
Inakimbia kama farasi, inabeba mizigo kama punda, kwa madaha ndio yenyewe..
 
Kitu RTD bana duh!

Kipindi hicho mkoa unaisikiliza mitaa ya Dar kupitia salam za asubuhi, nayakumbuka maeneo niliyokuwa najiuliza yakoje yakoje na nilikuwa na hamu ya kuyaona kama Magomeni Mapipa, Buguruni Malapa, Manzese kwa Mfuga Mbwa, Kiwalani etc.

Kulikuwa na kipindi cha ngano za mziki sikumbuki ni nani alikuwa anakitangaza, stori inatungwa kwa mziki mwanzo mwisho hafu mi najua kweli walioimba ni wale wahusika wa stori.

Naukumbuka wimbo wa kipindi cha Jumapili cha salamu za wagonjwa:-

Wakati umewadia wa salamu za wagonjwa hospitalini leo tunawapa pole,
Ajuaye bwana Mungu kwa mzima kuwa mfu mgonjwa kuwa salama leo tunawapa pole,

...
 
GAZETI hilo jina la libuda lilileta tabu sana pale kanda ya kati
 
Last edited by a moderator:
1. BIMA yako kwa maisha, BIMA yako kwa ajali, BIMA yako kwa ...

2. Idara yetu ya uhamiaji inalo jukumu kubwa sana, kuwakaribisha, kuwa..., na kulinda mipaka yetu.

3. Kuna wimbo kwenye kipindi cha usalama barabarani aliimba mnyamwezi (kama sio msukuma) mmoja:-
"Eti dreva kagonga treni ni sawa hiyo? Haaata, hiyo si dereva wacha vituko!"

Ha ha ha, maisha bana, enzi hizo presha ya betri hainihusu, mi nikusikiliza radio tu.
 
Kiukweli wakati ule RTD ilifanyakaz sana. Kulikuwa na Idhaa ya Taifa na Idhaa ya Biashara yaani had raha. Baadae ikaja Idhaa ya Taifa na Idhaa ya nje(External Services) pale EPZA kwa sasa. Baadae ikaja RTD ya kawaida na Powerful Realistic Trustworthy(PRT).Ndipo baada ya Tido Mhando alivyostaafu BBC akaunganisha TVT na radio za RTD yaani RTD na PRT pamoja na TVT KUUNDATBC
 
Yote tisa, kumi MIKINGAMO!
Kipindi hiki kingekuwepo leo, tungesikia mengi hususan sisi wa vijijini. Maana wengine hawana uwezo wa kuingia kwenye mitandao. Ila mafisadi wa siku hizi wagumu! Hata uwaseme vipi, wanakauka tu, hawabadiliki na bado watang'ang'ania madaraka. Shame.
 
Mahokaaaaa We mama mbavu zangu weeee we mama mbavu zangu weeee we mama mbavu zangu weee ha ha ha haaaaaaaaaa! Duh noma hapo jumapili napiga pasi uniform kwa ajili ya jumatatu pasi ni ya mkaa kama ya dobi mara mkaa au jivu linadondokea kwenye shati jeupe unaanza kufua kola upya enzi hizo electric iron ni luxurious item!

wewe ndio umenitachi maana mimi jumapili mida ya saa nane kulikuwa kipindi cha biblia yatuambia nini kuna kale kawimbo (kiashiria cha kipindi) nilikuwa nikisikia tu basi naanza kuandaa nguo za shule, kutafuta fagio kwa ajili ya shuleni kesho.
 
Umemshau,Salama Mpamao,si mbaya nikiwataja na hawa,Mzee Jangala,Kiatu,Tomato,Mshamu,Igunanilo,Mzee Mundu na wengineo ongezea.
 
Kiukweli wakati ule RTD ilifanyakaz sana. Kulikuwa na Idhaa ya Taifa na Idhaa ya Biashara yaani had raha. Baadae ikaja Idhaa ya Taifa na Idhaa ya nje(External Services) pale EPZA kwa sasa. Baadae ikaja RTD ya kawaida na Powerful Realistic Trustworthy(PRT).Ndipo baada ya Tido Mhando alivyostaafu BBC akaunganisha TVT na radio za RTD yaani RTD na PRT pamoja na TVT KUUNDATBC

Sasa turudi hapo kwenye TBC, mimi hili jina la TBC linanichefua sana kwa sababu ni kifupi cha maneno ya kiingereza, kwanini tusitafute maneno ya kiswahili? tunaendelea kuwa watumwa wa lugha? angalia Zanzibar nao wamebadili wanaiita ZBC kwanini isiwe Shirika la Utangazaji Zanzibar, au wangeacha tu iwe Sauti ya Tanzania Zanzibar, ambayo hata kuitamka inaleta raha, haya maneneo ya kiingereza hadi lini? tunakitupa kiswahili. Huyu Tido katoka huko BBC kaja huku kaondoa hiyo B moja ya mwanzo kaweka T. imekuwa TBC. Nakumbuka kulikuwa na shirika la habari Tanzania maarufu SHIHATA bila shaka na hii ilibadilisha na kupewa jina la kiingereza.
 
Mahokaaaaa We mama mbavu zangu weeee we mama mbavu zangu weeee we mama mbavu zangu weee ha ha ha haaaaaaaaaa! Duh noma hapo jumapili napiga pasi uniform kwa ajili ya jumatatu pasi ni ya mkaa kama ya dobi mara mkaa au jivu linadondokea kwenye shati jeupe unaanza kufua kola upya enzi hizo electric iron ni luxurious item!

Yaani we ndo umenikumbusha enzi hizooooo............Kwa kweli siku zikipita na mambo yanapita. Kumbuka hilo shati la shule umeweka wanga au blue ling'ae.......!!!! halafu linadondokewa jivu...!!
 
mi nilikua navutiwa na ezekiel malongo na fundi mitambo lando mabula.
 
Kitu RTD bana duh!

Kipindi hicho mkoa unaisikiliza mitaa ya Dar kupitia salam za asubuhi, nayakumbuka maeneo niliyokuwa najiuliza yakoje yakoje na nilikuwa na hamu ya kuyaona kama Magomeni Mapipa, Buguruni Malapa, Manzese kwa Mfuga Mbwa, Kiwalani etc.

Kulikuwa na kipindi cha ngano za mziki sikumbuki ni nani alikuwa anakitangaza, stori inatungwa kwa mziki mwanzo mwisho hafu mi najua kweli walioimba ni wale wahusika wa stori.

Naukumbuka wimbo wa kipindi cha Jumapili cha salamu za wagonjwa:-

Wakati umewadia wa salamu za wagonjwa hospitalini leo tunawapa pole,
Ajuaye bwana Mungu kwa mzima kuwa mfu mgonjwa kuwa salama leo tunawapa pole,

...

Mzee Kungumanga aliyeimba huo wimbo wa wagonjwa anazurura na gitaa lake maeneo ya Mbezi akipiga kinywaji kama kawaida.
 
Back
Top Bottom