mchumia tumbo
JF-Expert Member
- Jun 19, 2012
- 1,458
- 471
Mmemsahau Chris katembo wa kipindi cha mkoa kwa mkoa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sitawasahau CHILAMBO, HILLARY na JONGO. Kwanini? Nisikilize.....
Kwa kutambua umuhimu wa kila mmoja katika maendeleo ya soka au michezo kwa ujumla, leo nitawazungumzia watangazaji waliokuwa wakitangaza wakati huo ambao ufanisi wa kazi yao ulichangia kwa kiasi kikubwa msisimko wa soka.
Ninapokumbuka umahiri wa Chilambo, naishia kusema, Mungu amuweke mahali pema peponi! Amina.
Huku majina ya Khalfani Ngassa, Raphael Paul, Ali Bushiri, Hussein Marsha, Abdalah Bori, Kitwana Suleiman, David Mwakalebela, Rajabu Risasi, Rashidi Abdalah, Ibrahim Magongo, George Masatu, Nico Bambaga, Beya Simba na wengineo wa Pamba, yakipambwa vilivyo na Chilambo.
Chilambo, alikuwa na uwezo wa kumpatia picha kamili ya mchezaji kiumbo, kiuchezaji, kitabia, kitu ambacho ni watangazaji wachache wamejaliwa katika kutimiza wajibu na kazi zao.
Dah, kitambo sana enzi za kina Hendrick Maiko Libuda, lakini nasahau jina la yule
Mtangazaji alitangaza mechi ya simba na Atletico sports Aviacao ya Angola ambayo
ilikuwa na wachezaji wakali kama Kanka wemba, Abilio Amanali, Gito, Libenge, Bravo
Yanda, Nero sijui nelo n.k
Wakati huo simba ilikuwa ni kina Abdul Mashine, Mohammed Mwameja, Hussein Masha, Yamadhani Leny
Damian Kimti, Mteze John Rungu, Malota Soma, Edward Chumila n.k
Umenifanya nivikumbuke vipindi maarufu kama HISIA NA MUZIKI, MAHOKA, PWAGU NA PWAGUZI
PITIO LA KITABU NA SAIF D KIANGO N.K
Debora mwenda sitamsahau kamwe kwa kukifanya kipindi cha mama na Mwana
kipendwe hata na watu wazima......... acha Bwana hadithi tamu kama Ua Jekundu,
Binti chura, Kibibi jitu n.k Enzi zimepita sasa watoto wanacheza viduku.
Pia ninawakumbuka waigizaji kama Mzee MUNDU, Mshamu, Matuga n.k
CRDB ni benki ya wakulima kama..... Vijijini unalikumbuka hili tangazo? Tegemea bp ni nini...trekta meli ndege na vyombo vinginevyo...bp Tanzania limited ni zaidiiii! Je unakumbuka? Vikoromboso vinavyoendelea sasa iv kwenye radio ni aibu tupu. Damn I miss my childhood!!!Kwa vijana wa zamani. Unakumbuka nini unapopitia majina haya? Je, yuko wapi kwa sasa? Unamkumbuka katika kipindi kipi kilichokufurahisha?
1. Bujaga Izengo Kadago
2. Debora Mwenda
3. Sarah Dumba
4. Julius Nyaisanga
5. Charles Hillary
6. Eshe Mhidini
7. Frolian Kaiza
8. Tumbo Risasi
9. David Wakati
10. Halima Kihemba
11. Betty Mkwasa
12. January Costantine
13. Lando Mabula
14. Ben kiko
15. Abubakary Lyongo
16. Sued Mwinyi
17. Abisai Stevin
18. Nswima Ernest
19. Malima Ndelema
20. Richard Leo
21. Ahmed Jongo
22. Christina Chokunogela
23. Shaban Kissu
24. Jacob Tesha
25. Sallim Mbonde
26. Sekion
27. Omary
28. Abdalla Majura
Umenikumbusha mbali sana kaka wakati huo sh. mia inaitwa nyanga. Anyways mnayakumbuka na matangazo ya biashara na vipindi yaliyokuwa yanarushwa RTD kipindi hicho?
1. TANGAZO LA PEDI ZA JESI:
Wanawake kuweni na furahaaa, furahaaa, wakati wote popote na jesi,
Jesi, pedi mpya za kike za njano, ni nyororo raha kuvaa wakati wote......
2. TANGAZO LA DAWANOL
Mgongo wangu waniuma maumivu teleee, dawa ya maumivu dawa yenye nguvu dawa ni dawanol
3. TANGAZO LA SABUNI YA MSHINDI. n.k
MATANGAZO YA VIPINDI:
1. MASHIRIKA YA TAIFA: Mashirika ya taifa Tanzania yapo Mengi... na matangazo mengine mengi. Huwa natamani sana siku moja niende pale RTD nikaombe nipewe hayo matangazo niwe nayasikiliza tu mwenyewe ili niwe nakumbuka utotoni...DA INANIKUMBUSHA MBALI SANA
Ulikuwa unaamshwa na kipindi cha Tumsifu Mungu, kipindi kilichokuwa kinatayarishwa na padre Antony Chilumba
Nakumbuka kulikuwa na mzee Khalid Ponella na kipindi chake cha "Zilipendwa" kila Jumapili saa nne asubuhi na baadae jioni kipindi chake kingine cha "Klabu Raha Leo Show".
Tangazo la kodrai nilikuwa nalipenda jinsi sauti walivyozipangilia.kuna tangazo la sabuni ya kodrai, kondraiiiiiiiiiii,....... lilikuwalinapigwa baada ya kipindi cha majira asbh.likinikuta nyumbani hili tangazo nilikuwa najua hapo tayari nimeshachelewa no skonga,maana kwa dk 4 au 5 zilizobaki nisingeweza kuwahi skonga.
singing; posta na simu kweliiii,kweli
barua na posta, zifike haraka,tena kwa uhakika,litumie sasa,shirika la posta na simu tanzaniaaaaa.......
Sent from my blackberry 9780 using jamiiforums