Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Kipindi cha kijaluba na Abdalla Mlawa kwenye saa tau usiku
Kipindi cha Philips usiku mida ya saa mbili hivi kama sikosei idhaa ya biashara
Kipindi cha sikiliza Bwana umeme (kwa mwanga safi, mapishi bila moshi) enzi hizo watu wengi tu walikuwa wakimudu kupikia majiko ya umeme hata uswahilini.
 
Wachangiaji woote wa thread hii ni wa 50s, 60s NA 70s NIMEPENDA mmenikumbusha mbali
 
RTD, da mwili unanisisimka ilikuwa raha wakati ule.
 
Kwa vijana wa zamani. Unakumbuka nini unapopitia majina haya? Je, yuko wapi kwa sasa? Unamkumbuka katika kipindi kipi kilichokufurahisha?

1. Bujaga Izengo Kadago
2. Debora Mwenda
3. Sarah Dumba
4. Julius Nyaisanga
5. Charles Hillary
6. Eshe Mhidini
7. Frolian Kaiza
8. Tumbo Risasi
9. David Wakati
10. Halima Kihemba
11. Betty Mkwasa
12. January Costantine
13. Lando Mabula
14. Ben kiko
15. Abubakary Lyongo
16. Sued Mwinyi
17. Abisai Stevin
18. Nswima Ernest
19. Malima Ndelema
20. Richard Leo
21. Ahmed Jongo
22. Christina Chokunogela
23. Shaban Kissu
24. Jacob Tesha
25. Sallim Mbonde
26. Sekion Kitojo
27. Omary Jongo
#Nakumbuka tu #saa mbili kasoro robo ktk kipindi cha/"phillips ndio yenyewe sauti safi sauti kubwa"palikuwa na miziki balaa kama "yekhekhe tu ya yekeyeke"
 
Adul Ngalawa, huyu nilisikia nyerere alitoa masaa 24 amsikie redioni
 
Umenikumbusha mbali sana kaka wakati huo sh. mia inaitwa nyanga. Anyways mnayakumbuka na matangazo ya biashara na vipindi yaliyokuwa yanarushwa RTD kipindi hicho?

1. TANGAZO LA PEDI ZA JESI:
Wanawake kuweni na furahaaa, furahaaa, wakati wote popote na jesi,
Jesi, pedi mpya za kike za njano, ni nyororo raha kuvaa wakati wote......

2. TANGAZO LA DAWANOL
Mgongo wangu waniuma maumivu teleee, dawa ya maumivu dawa yenye nguvu dawa ni dawanol

3. TANGAZO LA SABUNI YA MSHINDI. n.k

MATANGAZO YA VIPINDI:

1. MASHIRIKA YA TAIFA: Mashirika ya taifa Tanzania yapo Mengi... na matangazo mengine mengi. Huwa natamani sana siku moja niende pale RTD nikaombe nipewe hayo matangazo niwe nayasikiliza tu mwenyewe ili niwe nakumbuka utotoni...DA INANIKUMBUSHA MBALI SANA
Ha!ha!ha! mgongo wanguu.........!
 
Dah, kitambo sana enzi za kina Hendrick Maiko Libuda, lakini nasahau jina la yule
Mtangazaji alitangaza mechi ya simba na Atletico sports Aviacao ya Angola ambayo
ilikuwa na wachezaji wakali kama Kanka wemba, Abilio Amanali, Gito, Libenge, Bravo
Yanda, Nero sijui nelo n.k


Wakati huo simba ilikuwa ni kina Abdul Mashine, Mohammed Mwameja, Hussein Masha, Yamadhani Leny
Damian Kimti, Mteze John Rungu, Malota Soma, Edward Chumila n.k


Umenifanya nivikumbuke vipindi maarufu kama HISIA NA MUZIKI, MAHOKA, PWAGU NA PWAGUZI
PITIO LA KITABU NA SAIF D KIANGO N.K

Debora mwenda sitamsahau kamwe kwa kukifanya kipindi cha mama na Mwana
kipendwe hata na watu wazima......... acha Bwana hadithi tamu kama Ua Jekundu,
Binti chura, Kibibi jitu n.k Enzi zimepita sasa watoto wanacheza viduku.

Pia ninawakumbuka waigizaji kama Mzee MUNDU, Mshamu, Matuga n.k
Mshamu alikuwa noma,halafu mzee mundu mbishi kupindukia full mfumo dume! kuna akina sijali ,havijawa!siwema binti mtayaona hadi raha!
 
hapo kwenye pasco mayalla huyihuyu wa ppr na jf au,huyu sio alianzia itv? kawahi kupitia rtd kweli?

Pasco Mayalla huyu huyu wa JF alianzia RTD ...mm pia nilikua nae maana nimepitia RTD kabla ya kuikimbia bongo....ni vijana tuliotoka vyuo tukapewa post za kwanza RTD...zamani bongo raha unamaliza chuo au secondary unasubiri barua ukafanye kazi wapi kama sio kuendelea na masomo,.

 
Duuh nimekumbuka wakati niko dogo...ilikua Simba wanacheza na Yanga...wadhamini alikuwa Said Salim Bakhresa alipofungua hotel yake ya kwanza anaingia jijini toka Pemba....Nawaz na Azam!!!!half time baada ya tangazo.. ile kurudi uwanjani Ahmed Jongo anatutangazia kijana mfupi, maji ya kunde aliyeshiba Omaar Husseeein "Keegan" anaipatia Yanga bao la kuongoza...zamani bongo raha sana sio siku hizi..kila sehemu matindikali haahaaha.....Nawaz na Azam karibu na kituo cha mabasi ya Temeke zamani hizo kiko hapo oppsite na shule ya uhuru na kota!
 
Duuh nimekumbuka wakati niko dogo...ilikua Simba wanacheza na Yanga...wadhamini alikuwa Said Salim Bakhresa alipofungua hotel yake ya kwanza anaingia jijini toka Pemba....Nawaz na Azam!!!!half time baada ya tangazo.. ile kurudi uwanjani Ahmed Jongo anatutangazia kijana mfupi, maji ya kunde aliyeshiba Omaar Husseeein "Keegan" anaipatia Yanga bao la kuongoza...zamani bongo raha sana sio siku hizi..kila sehemu matindikali haahaaha.....Nawaz na Azam karibu na kituo cha mabasi ya Temeke zamani hizo kiko hapo oppsite na shule ya uhuru na kota!

Kumbe Nawaz ilikuwa ni ya huyu Bakhresa! nakumbuka mjomba wangu alikuwa akinipeleka pale kupata Ice creamn, nakumbuka ukiingia unajitilia mwenyewe ice cream kwenye vimashine fulani hivi. inatoka kwenye vibomba.
 
Tutumie kibukuu ni pombe bora x2
Tumia kibuku ni pombe bora, tumia kibuku ni pombe bora

Ahahahhh, those days I wish zijirudie kwekweli, mkiwa mnasikiliza mchezo wa redio hata kukohoa hamna, attention masikio yote kwenye radio


Jangala pia unamkumbuka? Kipindi Chao cha maigizo kilikuwa kinarushwa hewani saa tatu usiku kikifadhiliwa na kibuku kila jumapili usiku. Kuna siku mshamu alimvamia Baba yake jangala na wenzake wakampiga na kumwacha akimbie wenzake mshamu wakasema acha masiala bwana dingi lake mshamu linayeya kama pajero kesho take ikawa gumzo kitaa. Je na hili tangazo la bp pia una unalikumbuka? Mazungumzo baaada ya habari mmeletewa kutoka radio Tanzania dar es salaam. Enzi hizo tunaishi kota za Wazo hili tukicheza na watoto wa nizar karamagi wanakaa magorofani. Am 33 years now.
 
Hahahaha:A S 2152:, hii inatufanya tukumbuke matukio mengi; mimi kuna tangazo la chibuku nilikuwa nalipenda sana! Kutumia chibuku.... ni kikombe boraaa... Pia kipindi cha "maneno hayoo" sijui kilipotelea wapi
 
Hebu nikumbusheni, baada ya kipind cha jambo kuisha kulikuwaga kinafuatia kipindi cha tuimbe sote (kwaya za kuhamsisha maendeleo) halafu kulikuwa na kipindi walimu walikuwa wanafundisha, nakumbuka sie darasa la sita na lasaba vipindi hivyo vikianza kama ni sayansi basi mwalimu wa sayansi anakuja na redio darasani mnaanza kusikiliza, (shuleni kwetu kulikuwa na redio) kipindi kikiisha maswali, ole wako ushindwe kujibu. Naomba mnikumbushe hicho kipindi kilikuwa kinaitwaje.
Baada ya hicho kipindi ilikuwa inafuata taarifa ya habari saa nne

Nilikuwa nawajua watangazaji wote wa RTD kwa sauti zao, akianza tu najua huyu ni nani, nilikuwa najua vipindi vyote vya RTD kuanzia jumatatu hadi jumapili, najua kikiisha kipindi hiki basi kinachofuata ni hiki, lol!
 
Nilikuwaga nampenda sana huyu dada, siku waliyotangaza amefariki dunia nililia sana siku hiyo, kweli vizuri havidumu, miaka hiyo thamanini na kitu

Nakumbuka RTD walikuwaga wanafanya mashindano ya bendi zetu za muziki wa dansi,
Top 10 sasa Vijana jazz, mlima park, Juwata jazz, washirika tanzania stars, tankati almasi, Mk group, mk beats, super matimila na Orchester Maquiz du zaire lol, nilikasirikaga mwaka 1988 eti waipa ushindi bendi ya vada arts na wimbo wao wa Tanzania


Salama Mfamao RIP
Aloysia Isabula
Aloysia Maneno
Peter Makorongo
Suleiman Kumchaya
Juma Ngondae RIP
Mshindo Mkeyenge
Abdallah Mlawa
Siwatu Luanda RIP
Salim Mbonde
Omary Masoud RIP
Pascal Mayalla
Adam Mwaibabile
etc....
 
Dah! enzi za kuunganisha betri ili uweze kusikiliza redio, nakumbuka zaidi 'club raha leo show' mtu akitambulishwa anapiga chombo chake kidogo au anaimba kidogo basi anashangiliwa na umati
Pia kulikuwa na tangazo la baiskeli ya 'Shengshang' sijui km nimepatia spelling, dah!
 
Back
Top Bottom