Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

 
namkumbuka Ben Kiko (Benedict Kikoti) na kipindi chake cha mambo hayo kutoka kanda ya kati dodoma. bila kumsahau Abdallah Mlawa.

kwa ujumla RTD haikuwa na mchovu hata mmoja. Ndio maana watangazaji wengi wapo ktika radio za mashirika ya nje.

nikikumbuka watangazaji wa mpira akina:
1. Charles Hillary..... Namna gani pale
2. Dominic Chilambo
3. Omary Jongo
3. Ahmed Jongo .... Inakuwa Obstruction pale
4. Na wengineo
5. Wa sasa hovyoooooo...
 
We Pascal ina maana sie mafundi uwa hatukubukwi. Au unataka nife kwanza ndo mtatukumbuka. Umewasahau mafudi kama vile Domitla Urassa, Juma Bungara. Bundala, Mzee Juma Sereka, Konsalva Mwereke nk. Ndio hao waliokufanya usikike na upate umaarufu kwa kukuandalia lineup ya mziki na kurekebisha sauti yako wakati wako pale studio Red na Studio Blue. Bila hao ngoma za ZIPOMPAPOMBA husingetamba nazo wewe
 
Dah! nilikuwa nimemsahau huyu ndugu, aisee RTD ilikuwa kiboko. Uliyeuliza kuhusu malima ndelema, bado yuko hai, mara ya mwisho nilimsikia alikuwa anatangaza matangazo ya moja kwa moja kutoka mbeya, sikumbuki ilikuwa ni sherehe gani
Bujaga Izengo Kadago alikuwa bonge la mtu mwenyeji wa Tinde Shinyanga.
 
Kweli aise, mtangazaji alikuwa hawezi kuanza kipindi hadi amtambulishe fundi mitambo na anapomaliza kipindi lzm amshukuru.... wapi Lando Mabula
 

ben kiko bado yu hai,na mwanae ni swaiba wangu sana,na ben kiko mwenyewe yupo tabora
 
Hii ni taarifa ya habari kutoka Redio Tanzania Dar Es Salaam msomaji Sango Kipozi. Kwanza habari kwa ufupi.
Rais wa jamhuri ya muugano wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere leo amemfukuza kazi Waziri wa Elimu kwa utendaji dhaifu katika wizara hiyo uliosababisha matokeo mabaya sana kwa Wanafunzi waliomaliza kidatu cha nne mwaka jana.
 
NAMJUA ABDU MASUDI na David wakati TUU KWA SURA LAKINI WENGINE SIWAJUI HATA MMOJA KWA SURA hata nikikutana nao new York au Tel Aviv. halafu miaka ya mwanzononi ya 70's, kulikuwa na kipindi cha mbiu za mikoa na mazungumzo baada ya habari. Vipindi hivi vilijaa maneno ya kudanganya umma kuliko kitu chochote duniani. Vilijaa matusi kwa mabepari na uongo wa maendeleo vijijini. Utasikia wakulima wa pamba geita wamepata bilion nane za mauzo ya pamba! au wakulima wa miwato kwimba wamepata milion arobaini ! au wakulima wa pareto njombe wamepata bilion tisini! ukigawana pesa hizo kwa idadi ya kila mmoja utakuta kila mkulima kapata shilingi alfu nane tuu!

nakumbuka mazungumzo baada ya habari yaliyokuwa yanasema,: "weweee, mitaji haramu ya kujijengea mali umeipata wapi weweeee!" au yale ya " baba baba, unafanya nini hapo ulipo"

hawa watangazaji wa iliyokuwa RTD nawapa hongera ya kupotosha umma kuliko kuelimisha watu! Ujamaa ulikuwa ni sumu kwa umma kuliko hata ukimwi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…