Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mama Debora Mwenda
Unakumbuka zile hadithi? jumamosi ikifika saa nane mchana watoto wote tuko kwenye radio, na mashuleni tulikuwa na club za mama na mwana
Wanabodi,
Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.
...............Huyu Mungu TUNAMSINGIZIAGA SANA. Nadhani muda mwingi huwa anacheka tu! We Paschal shukuru umeondoka pale bado mdogo. Ungemkuta alieanzisha haya maafa labda na wewe usingekuwepo leo. Mtoto wa kizaramo kaifyeka RTD si mchezo. Na hii mifano imo maofisi mengi ya serikali, mashirika ya umma na hata binafsi. Kitendo cha kuzungukana na kung'ang'ania mtu mmoja. Kinatekeza sana watu hapa Tanzania.
Bujaga Izengo Kadago alikuwa bonge la mtu mwenyeji wa Tinde Shinyanga.
Kutokuwa na taarifa za hawa watu sio kwamba wametangulia mbele za haki. Mleta mada kasema waliotangulia mbele za haki.Jacob Tesha
Sekioni Kitojo
Godfrey Mghodo
Muhamed Abdulrahman
Chisunga Steven
n.k
We Pascal ina maana sie
mafundi uwa hatukubukwi. Au unataka nife kwanza ndo mtatukumbuka.
Umewasahau mafudi kama vile Domitla Urassa, Juma Bungara. Bundala, Mzee
Juma Sereka, Konsalva Mwereke nk. Ndio hao waliokufanya usikike na upate
umaarufu kwa kukuandalia lineup ya mziki na kurekebisha sauti yako
wakati wako pale studio Red na Studio Blue. Bila hao ngoma za
ZIPOMPAPOMBA husingetamba nazo wewe
Ben Kiko, sijui yuko wapi huyu jamani
Alesia maneno na Alesia Isabula nadhani bado wapo TBC taifa
Watangazaji wa zamani walikuwa watangazaji kweli
Chezea Michael Katembo na Kipindi cha mkoa kwa mkoa
Nilikuwa nampenda Siwatu Luanda(RIP)nakumbuka alifariki nikiwa drs la tano miaka hiyo
ben kiko bado yu hai,na mwanae ni swaiba wangu sana,na ben kiko mwenyewe yupo tabora
NAMJUA ABDU MASUDI na David wakati TUU KWA SURA LAKINI WENGINE SIWAJUI HATA MMOJA KWA SURA hata nikikutana nao new York au Tel Aviv. halafu miaka ya mwanzononi ya 70's, kulikuwa na kipindi cha mbiu za mikoa na mazungumzo baada ya habari. Vipindi hivi vilijaa maneno ya kudanganya umma kuliko kitu chochote duniani. Vilijaa matusi kwa mabepari na uongo wa maendeleo vijijini. Utasikia wakulima wa pamba geita wamepata bilion nane za mauzo ya pamba! au wakulima wa miwato kwimba wamepata milion arobaini ! au wakulima wa pareto njombe wamepata bilion tisini! ukigawana pesa hizo kwa idadi ya kila mmoja utakuta kila mkulima kapata shilingi alfu nane tuu!Wanabodi,
Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.
Hii list sio walikufa lini ni random, nikiwakumbuka wengine nitawaongeza!
Tukianzia na
- David Wakati
- Abdul Masudi (Jawewa)
- Eli Mbotto
- Stephen Mlatie
- Siwatu Luanda
- Salama Mfamao
- Salim Seif Nkamba (Mjomba)
- Michael Katembo
- Nelly Kidella
- Halima Mchuka,
- Omar Jongo
- Tumboi Tamimu Risasi
- Mohamed Mombo
- Abisai Stephen (Uronu)
- Stephen Lymo.
- Nadhir Mayoka
- Juma Ngodae
- Rukia Machumu
- Karim Besta
- Henrick Michael Libuda
- Idrissa Sadalah
- Bati Kombwa
Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Pia sio vibaya kuwaulizia wale watangazaji wa siku nyingi ambao hatujui walipo, ili kama nao wametangulia tuyaingize majina yao.
RIP All the Fallen Heroes wa Tasnia ya Utangazaji Tanzania!,
Pascal.
Mama Deborah Mwenda na wakati mwingine Aloycea Maneno
Pascal unaweza
kujua kama Angalieni Mpendu tunae? Na kuna kile kipindi cha 'Hisia na
Muziki' kilikuwa poa sana