Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Mimi na marehemu baba yangu tulikuwa washabiki kisawasawa wa Pamba ya Mwanza TP Lindanda wanakawekamo!
Kupitia Pamba FC nilikuwa shabiki mkubwa sana wa Dominic Chilambo!!! RIP my father , RIP Dominic Chilambo , RIP Pius Nyamko (mnamjua?)
 
Reactions: ram
Mkuu kwelitupu, kiukweli ukweli ni kitu kigumu, ila mimi ni mkweli!. Nilipojiunga, nilielezwa kuhusu uchawi!, bahati mbaya siamini kuwa uchawi upo!. Kiukweli uchawi upo, ila ni kwa wanaoamini tuu kuwa uchawi upo!, kwa sisi tusioamini, kwetu uchawi haupo!.

Wala siamini sababu ya vifo ni uchawi, ila pia naomba kuutoa ukweli mchungu kuhusu RTD ya enzi hizo!.

Ulikuwa unajua saa tuu ya kuingia kazini, ya kutoka huijui!. Mimi nakumbuka siku nikiingia asubuhi, unafuatwa saa 9 usiku, unapaswa kutoka saa 6 mchana, ila ukitoka ndipo ueanze kuandaa vipindi vyako!, kunawakati unaingia saa 9 usiku, unatoka saa 6 usiku siku inayofuata!.

Tulipoanza kazi Mjomba (SS Mkamba), akatuhusia mkitaka salama hapa, hawa akinadada waangalieni tuu!, msiwasogelee kwa sababu macho yote yako kwao!. Mimi na Abou tukamhakikishia Mjomba kuwa hilo kweli haliwezekani, kwa sababu, hao "wadada" wenyewe tuliwaona wachovu tuu!.

Baada ya kupita miezi 6, kumbe watu mnaokuwa nao kila siku, mara wa kwanza kuanza "kuona" ni Abou!, tukasema kumbe ful;ani ni mzuri hivi!, huku na kule, "akafika mahali!", kufumba kufumbua, Abou kahamidshiwa Nachingwea!.
Huko hata hoteli kuku ni mpaka ulipie kabla ndipo upikiwe!.

Ikaja zamu yangu!, ilikuwa ni balaa!, Mwanzoni tulianzia vile vi gesti Buguruni!, mambo yalipokolea, gesti mbali!, ni kila mahali, kuanzia "washroom!', studio!, juu ya meza ya ofisi!, kwenye ngazi!, hadi Telefon room!.

Mwanzo mwanzo tulitumia!, tulipozoeana, hatukukumbuka tena!. Wengi wa watumishi wa RTD wenye watoto, baba zao wako hapo hapo!. Kuna wengine wetu tumesurvive kwa kudra tuu ya Mwenyeezi Mungu!, tatizo kubwa la watangazaji wa zamani ni kuponzwa na umaarufu!, kujifungia studio kwa masaa mengi na watu wale wale hadi kujikuta kwenye Zero Grazing!, Ukisikia mtangazaji wa kike kaolewa, ujue aliyependa ni huyo mtangazaji wa kike!, yaani ili uoe mtangazaji, lazima kwanza mtangazaji huyo ndio akupende wewe!, vinginevyo! ukipenda wewe! jua.. ( japo nakiri sio wote).

Hii "zero graizing!" could be the main cause!.

Ila pia naomba kuwahakikishieni, pamoja na yote hayo, chanzo cha vifo sio UKIMWI!, kwa sababu Ukimwi ni "ukosefu tuu wa kinga mwilini!, yaani mtu hawezi kufa kwa "ukimwi" kwa kasabu ukimwi sio ugonjwa!, ila ukishakosa hiyo kinga mwilini, mwili wako unakuwa dhaifu na kuwa rahisi kushikwa na ugonjwa ambao ndio hupelekea kifo!.

Pasco.
 

hawa je wapo au?

Suleiman muhogora

mohamed mngombo

eli Mwaipopo

pili said
 
idrisa sadala nyanda za juu kusini mbeya
hicho ni kipindi cha majira saa 3 usiku
hizi radio za fm zina faida zake ila zimekosa watangazaji wenye weledi na kazi zao
 
Nakumbuka Omar jongo na Ahmed Jongo walipokuwa wakitangaza mashindano ya kombe la afrika mashariki kule Kampala, Jongo akisema ''Wasikilizaji...wakati mkisikiliza wadhamini wetu...Saidi Mwamba Kizota anafunga bao hapa. Yanga 3 Express 0, nadhaniilikuwa ni ama 1991 au 1992 vile, pale nakivubo.
 
Mzee Dominic Chilambo (RIP) nakumbuka akitangaza mechi CCM Kirumba ambapo timu ta Tanzania "Kakakuona" ikicheza, ila kiukweli Pamba ilikuwa ni kiboko. Chilambo alifariki na faniyake maskini.
 
du namkumbuka fundi mitambo mmoja somebody URASSA rip nae kwa sasa alikuwa anakaa sinza mori
 
Hili la kuchukuana wenyewe kwa wenyewe nalo lipo.kuna mtangazi nguli mmoja amezaa na mtangazi mwenzake wote walikuwa wanakaa sinza mori , ila kwa sasa wote wameoa na kuolewa na mtu mwingine duu nimeamini vya hekaluni huliwa na watu wa hekaluni
 
Hivi kile kipindi cha......mahokaaaaaaa.......nani alikuwa anakitangaza........?
 

Nalazimika kukuheshimu sana mkuu Pasco japo kuna mengi tunayopishana!! Kama bado hujafikia to the highest digree ya kuwa mkweli basi unajitahidi kuwa mkweli at your best,Mungu akuongezee maisha mkuu!! Ili tukibarikiwa kufikia umri wako utufundishe How to walk your walk, ila si kwenye uwanja wa siasa!! Hapo tutakuwa tofauti mkuu.
 
Last edited by a moderator:
mkuu umewasahau;
suleiman Hegga
John Makongoro
Salim Mbonde
na yule wa mazungumzo baada ya habari
 

hiyo list radio one ilikua kiboko.
 
Mkuu Capt Tamar, japo umechanganya kidogo majina, mimi ndiye mwenyewe haswa!, verified, nilikuwa mtangazaji wa vipindi vya burudani kwenye redio, nilipoingia kwenye TV nilijikita kwenyue siasa, na huko ndiko ninaelekeza nguvu zangu zote kulisadia taifa langu!. Amini nakuambia, kwenye sisa ndiko utapatana sana na mimi kama unapenda siasa za ukweli, na sio hizi za uwongo, unafiki, fitna, majungu na ushabiki wa watu/vyama bila substance behind!. Najipanga kutoa somo la siasa za kweli!. Soon!.
Pascal.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…