Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu kwelitupu, kiukweli ukweli ni kitu kigumu, ila mimi ni mkweli!. Nilipojiunga, nilielezwa kuhusu uchawi!, bahati mbaya siamini kuwa uchawi upo!. Kiukweli uchawi upo, ila ni kwa wanaoamini tuu kuwa uchawi upo!, kwa sisi tusioamini, kwetu uchawi haupo!.PASCO,
Ili tuelezane ukweli; tangu enzi hizo nimekuwa nikisikia from many different sources kuwa RTD ndio sehemu iliyokua inaongoza kwa fitina, uchawi na kurogana kazini...na hata ufuska...! Could it not be that this high death rate ya wafanyakazi hapo RTD ilichagizwa na hizo factors??
Wanabodi,
Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.
Hii list sio walikufa lini ni random, nikiwakumbuka wengine nitawaongeza!
Tukianzia na
- David Wakati
- Abdul Masudi (Jawewa)
- Eli Mbotto
- Stephen Mlatie
- Siwatu Luanda
- Salama Mfamao
- Salim Seif Nkamba (Mjomba)
- Michael Katembo
- Nelly Kidella
- Halima Mchuka,
- Omar Jongo
- Tumboi Tamimu Risasi
- Mohamed Mombo
- Abisai Stephen (Uronu)
- Stephen Lymo.
- Nadhir Mayoka
- Juma Ngodae
- Rukia Machumu
- Karim Besta
- Henrick Michael Libuda
- Idrissa Sadalah
- Bati Kombwa
Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Pia sio vibaya kuwaulizia wale watangazaji wa siku nyingi ambao hatujui walipo, ili kama nao wametangulia tuyaingize majina yao.
RIP All the Fallen Heroes wa Tasnia ya Utangazaji Tanzania!,
Pascal.
hawa je wapo au?
Suleiman muhogora
mohamed mngombo
eli Mwaipopo
pili said
Rehema Malipula?
jane....
rocas Matipa
ben kiko bado yu hai,na mwanae ni swaiba wangu sana,na ben kiko mwenyewe yupo tabora
Bujaga Izengo Kadago alikuwa bonge la mtu mwenyeji wa Tinde Shinyanga.
yuko sua
Mkuu kwelitupu, kiukweli ukweli ni kitu kigumu, ila mimi ni mkweli!. Nilipojiunga, nilielezwa kuhusu uchawi!, bahati mbaya siamini kuwa uchawi upo!. Kiukweli uchawi upo, ila ni kwa wanaoamini tuu kuwa uchawi upo!, kwa sisi tusioamini, kwetu uchawi haupo!.
Wala siamini sababu ya vifo ni uchawi, ila pia naomba kuutoa ukweli mchungu kuhusu RTD ya enzi hizo!.
Ulikuwa unajua saa tuu ya kuingia kazini, ya kutoka huijui!. Mimi nakumbuka siku nikiingia asubuhi, unafuatwa saa 9 usiku, unapaswa kutoka saa 6 mchana, ila ukitoka ndipo ueanze kuandaa vipindi vyako!, kunawakati unaingia saa 9 usiku, unatoka saa 6 usiku siku inayofuata!.
Tulipoanza kazi Mjomba (SS Mkamba), akatuhusia mkitaka salama hapa, hawa akinadada waangalieni tuu!, msiwasogelee kwa sababu macho yote yako kwao!. Mimi na Abou tukamhakikishia Mjomba kuwa hilo kweli haliwezekani, kwa sababu, hao "wadada" wenyewe tuliwaona wachovu tuu!.
Baada ya kupita miezi 6, kumbe watu mnaokuwa nao kila siku, mara wa kwanza kuanza "kuona" ni Abou!, tukasema kumbe ful;ani ni mzuri hivi!, huku na kule, "akafika mahali!", kufumba kufumbua, Abou kahamidshiwa Nachingwea!.
Huko hata hoteli kuku ni mpaka ulipie kabla ndipo upikiwe!.
Ikaja zamu yangu!, ilikuwa ni balaa!, Mwanzoni tulianzia vile vi gesti Buguruni!, mambo yalipokolea, gesti mbali!, ni kila mahali, kuanzia "washroom!', studio!, juu ya meza ya ofisi!, kwenye ngazi!, hadi Telefon room!.
Mwanzo mwanzo tulitumia!, tulipozoeana, hatukukumbuka tena!. Wengi wa watumishi wa RTD wenye watoto, baba zao wako hapo hapo!. Kuna wengine wetu tumesurvive kwa kudra tuu ya Mwenyeezi Mungu!, tatizo kubwa la watangazaji wa zamani ni kuponzwa na umaarufu!, kujifungia studio kwa masaa mengi na watu wale wale hadi kujikuta kwenye Zero Grazing!, Ukisikia mtangazaji wa kike kaolewa, ujue aliyependa ni huyo mtangazaji wa kike!, yaani ili uoe mtangazaji, lazima kwanza mtangazaji huyo ndio akupende wewe!, vinginevyo! ukipenda wewe! jua.. ( japo nakiri sio wote).
Hii "zero graizing!" could be the main cause!.
Ila pia naomba kuwahakikishieni, pamoja na yote hayo, chanzo cha vifo sio UKIMWI!, kwa sababu Ukimwi ni "ukosefu tuu wa kinga mwilini!, yaani mtu hawezi kufa kwa "ukimwi" kwa kasabu ukimwi sio ugonjwa!, ila ukishakosa hiyo kinga mwilini, mwili wako unakuwa dhaifu na kuwa rahisi kushikwa na ugonjwa ambao ndio hupelekea kifo!.
Pasco.
mkuu umewasahau;Wanabodi,
Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.
Hii list sio walikufa lini ni random, nikiwakumbuka wengine nitawaongeza!
Tukianzia na
- David Wakati
- Abdul Masudi (Jawewa)
- Eli Mbotto
- Stephen Mlatie
- Siwatu Luanda
- Salama Mfamao
- Salim Seif Nkamba (Mjomba)
- Michael Katembo
- Nelly Kidella
- Halima Mchuka,
- Omar Jongo
- Tumboi Tamimu Risasi
- Mohamed Ng'ombo
- Abisai Stephen (Uronu)
- Stephen Lymo.
- Nadhir Mayoka
- Juma Ngodae
- Rukia Machumu
- Karim Besta
- Henrick Michael Libuda
- Idrissa Sadalah
- Bati Kombwa
- Iddi Rashid Mchatta
- Dominic Chilambo
Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Pia sio vibaya kuwaulizia wale watangazaji wa siku nyingi ambao hatujui walipo, ili kama nao wametangulia tuyaingize majina yao.
RIP All the Fallen Heroes wa Tasnia ya Utangazaji Tanzania!,
Pascal.
Hiki ni kikosi cha first 11 ya Radio One.
Waliokaa kutoka Kushoto ni Charles Hilary kwa sasa yuko BBC-London
Mikidadi Mahamod (Brother) sasa ni Mkurugenzi wa Radio Uhuru, Mzungu Mike Ross, na Uncle J. Nyaisangah.
Waliosimama toka kushoto, Deo Mshigeni yuko US, Monica Mfumia yuko UK, Florah Nducha ni Mkuu wa UN Radio New York, Vicky Msina, ni PRO wa BOT, Aboubakar Liongo yuko DW-Radio ya Ujerumani, Lilian Mbaga sasa ni Mkurugenzi wa TGNP, Sunday Shomari yuko VOA na Taji Liundi sasa ni Meneja wa PRT ya TBC.
Mkuu Capt Tamar, japo umechanganya kidogo majina, mimi ndiye mwenyewe haswa!, verified, nilikuwa mtangazaji wa vipindi vya burudani kwenye redio, nilipoingia kwenye TV nilijikita kwenyue siasa, na huko ndiko ninaelekeza nguvu zangu zote kulisadia taifa langu!. Amini nakuambia, kwenye sisa ndiko utapatana sana na mimi kama unapenda siasa za ukweli, na sio hizi za uwongo, unafiki, fitna, majungu na ushabiki wa watu/vyama bila substance behind!. Najipanga kutoa somo la siasa za kweli!. Soon!.Nalazimika kukuheshimu sana mkuu Pasco japo kuna mengi tunayopishana!! Kama bado hujafikia to the highest digree ya kuwa mkweli basi unajitahidi kuwa mkweli at your best,Mungu akuongezee maisha mkuu!! Ili tukibarikiwa kufikia umri wako utufundishe How to walk your walk, ila si kwenye uwanja wa siasa!! Hapo tutakuwa tofauti mkuu.